Twasherehekea maadhimisho ya miaka 20 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, sambamba na maadhimisho ya miaka 10 ya kuanzishwa kwa mfumo wa Uigaji

Agenda ya Afrika 2063 ilitegemea matarajio ya saba, ya kufikia Afrika (kama mchezaji na mshirika wa kimataifa mwenye nguvu na ushawishi), pamoja na lengo la sita linalolenga (Afrika ambapo watu wanaongoza maendeleo: kwa kutoa uwezo unaooneshwa wazi katika Wanawake na Vijana), Kwa hiyo, Mfumo wa Uigaji wa Umoja wa Afrika wa Misri unafanya kazi juu ya umuhimu wa kuelimisha vizazi vijavyo kuhusu historia ya taasisi kuu ya Umoja na kuimarisha ujuzi wao kwa taasisi na mashirika ya bara, katika jaribio la kuamsha mipango yao ya maendeleo, na kuimarisha kanuni ambazo Baba Waanzilishi wa Umoja wa Afrika walikuwa wakifanya kazi kuziimarisha.
Kulingana na uangalizi wa mfumo wa Uigaji wa Umoja wa Afrika kwa kushirikiana na Harakati ya Nasser kwa Vijana, kwa kuwashirikisha vijana na kuimarisha jukumu lao, na katika ukumbusho wa kumbukumbu ya miaka kumi ya kuanzishwa kwa mfumo huo 2012 kama mfumo wa kwanza wa kuiga kwa Umoja wa Afrika nchini Misri, na yanayosambamba na maadhimisho ya miaka ishirini ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, kama upanuzi wa shirika la Umoja wa Afrika lililoanzishwa mnamo 1963, na jukumu lake kubwa la kihistoria wakati wa harakati za ukombozi wa Afrika, hadi sasa, tunafurahi tushirikiane kuadhimisha tukio hilo kupitia kupeleka makala kwa kiasi cha maneno 1000 au aya fupi kwa kiasi cha maneno 200 kwa moja ya lugha unazozijua vizuri (Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, Kihispania), kwenye barua pepe ifuatayo:
modelafricanunionegypt@gmail.com
Aya inapaswa kushughulikia moja ya maudhui zifuatazo:
• Kwa makala (maneno 1000)
1. Mtizamo wenu katika jukumu la siasa na maendeleo la Umoja wa Afrika.
2. Kusimulia maelezo ya kihistoria, kuhusu Umoja wa Afrika, na Shirika la Umoja wa Nchi huru za Afrika.
3. Uandike juu ya mmoja wa baba waanzilishi wa Umoja wa Afrika kama vile, (Kwame Nkrumah, Julius Nyerere, Gamal Abdel Nasser, Haile Selassie, Nk…)
4. Ufafanue mtazamo wako jinsi vijana wanavyoweza kuchangia Umoja wa Bara la Afrika.
5. Jinsi ya kuimarisha jukumu la Vijana katika kuanzisha na kuhamasisha makundi ya umati karibu na mipango ya maendeleo ya Umoja wa Afrika, ambayo inaongozwa na Ajenda ya Afrika 2063.
6. Jukumu la nchi yako katika Umoja wa Afrika.
Kwa Aya (maneno 200) •
Inawezakana kujibu moja ya maswali yafuatayo:
1. Unaonaje Ajenda ya Afrika 2063?
2. Unaposikia neno la Afrika, unaonaje?
3. Unahisi nini wakati wa kusikia neno la Umoja wa Afrika?
4. Vipi unaweza kuongeza jukumu la vijana katika Umoja wa Afrika?
5. Je, ni Kauli Mbiu gani bora ya kiafrika unayopenda kusema?
Zingatio:
- Tutashiriki mtazamo wenu kupitia vipindi vyetu kwenye majukwaa yetu rasmi ya mitandao ya kijamii, kwa hiyo unapaswa kuambatisha na yaliyo juu ; picha yako binafsi, jina na nchi.
Misri ni kijiji changu … Afrika ni mji wa nyumbani kwangu