Ghazaly" kama mzungumzaji katika Kongamano la kwanza la kila mwaka la mashauriano kwa viongozi vijana waafrika huko Ufalme wa Morocco
Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, na Makamu wa Mkuu wa zamani sana wa Umoja wa Vijana wa Afrika, alishiriki kama mtaalamu wa bara katika nyanja za vijana, utamaduni, na vyombo vya habari katika Kongamano la kwanza la kila mwaka la viongozi vijana waafrika kwa mwaka wa 2022, lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Afrika (PYU), huko Rabat, likiwa na Ufadhili wa Mfalme Mohammed wa sita, Mfalme wa Ufalme wa Morocco, mnamo Julai 20 hadi 24, akiwakilisha Misri miongoni mwa viongozi vijana 100 kutoka kwa wakuu wa mashirikisho na mabaraza ya vijana ya kitaifa, yanayowakilisha takriban nchi 52 za Afrika.
Hayo yametokea kwa mahudhurio ya kundi la mawaziri, viongozi na watoaji wa maamuzi katika ngazi ya kikanda na kimataifa, wakiwemo: Mheshimiwa Momeni Diala, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Afrika, Bw. Ahmed Ping, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Afrika, Silvia Lopez-Icra, Mratibu wa Umoja wa Mataifa akaaye Morocco, Bi. Nardos Bekele-Thomas, Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Afrika kwa Maendeleo (NEPAD), Waziri Mehdi Bin Said, Waziri wa Vijana, Utamaduni na Mawasiliano wa Ufalme wa Morocco, Bi. Raymond Oching, Katibu wa Wizara ya Huduma za Umma, Vijana na Masuala ya Jinsia katika Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Fathallah Al-Zeini, Waziri wa Vijana nchini Libya, Mheshimiwa Eric Simio Fafuku, Naibu Waziri wa Hazina ya Kitaifa na Mipango ya Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Mohamed Benjoura, Waziri wa Masuala ya Vijana wa Jamhuri ya Sierra Leone, na Mheshimiwa Tahyana Rotovoson, Naibu Waziri wa Vijana na Michezo wa Jamhuri ya Madagaska.
Katika muktadha unaohusiana, Kongamano hilo lilishughulikia idadi ya vikao vya mjadala, semina, na mikutano ya mashauriano, kuhusu mada kadhaa na maswala muhimu, ikijumuisha; Kikao chenye kichwa “Kuunganisha Mafanikio Yetu: Kuunda Ubia Kuelekea Programu ya Ufufuo wa Kiafrika”, pamoja na kushughulikia suala la uhamiaji Barani Afrika, pamoja na kichwa: “Kurahisisha Mgogoro wa Uhamiaji Barani Afrika; Kuweka mtindo wa sekta mbalimbali ili kukabiliana na changamoto,” licha ya kujadili njia za kukuza uadilifu wa kijamii, amani na usalama, ili kuja na mapendekezo yanayotekelezeka katika maandalizi ya kuyawasilisha kwa watoaji wa maamuzi katika Umoja wa Afrika.
Kwa upande wake, Ghazaly wakati wa mikutano ya kikanda na ya mashauriano, amesisitiza umuhimu wa kuweka Ajenda ya Afrika ya mwaka wa 2063 kama nyaraka rejea ya shughuli, matukio na programu zozote zinazoanzishwa na viongozi vijana na wakuu wa mabaraza ya vijana ya kitaifa katika nchi mbalimbali za Afrika,pia kuongeza uelewa mpana na kuhamasisha makundi ya jamii ya kiafrika inayoizunguka, na pia alisisitiza umuhimu wa kufanya kazi ili kuanzisha Mkataba wa Vijana wa Kiafrika kama nyaraka rejea yenye hatua na taratibu kwa manufaa ya vijana.
Ghazaly alihitimisha maneno yake akitoa Shukrani zake za dhati kwa Ufalme wa Morocco kwa kuunga mkono kwa Makao makuu ya Umoja wa Afrika, pia kwa mchango wa Taasisi za kiutekelezaji za kufanyika na kufanikiwa Kongamano hilo, akisisitiza uungaji mkono na imani yake katika uwezo wa viongozi wa sasa wa Umoja wa Vijana wa Afrika (PYU), akieleza umuhimu wa Muungano wa Vijana wa Afrika upate viti vya kudumu katika vikao vya kamati maalumu za Utamaduni, Vijana na Michezo ndani ya Umoja wa Afrika, akiashiria kuwa cheo cha Mjumbe wa Vijana wa Afrika kilianzishwa kutokana na pendekezo moja la Muungano wa Vijana wa Afrika, kufuatia mojawapo ya mashauriano yake mwaka wa 2016, yanayothibitisha kikubwa uwezo wa Muungano huo kushiriki katika kufanya maamuzi na sera muhimu ndani ya Umoja wa Afrika.
 
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
                         
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
                                        
                                     
            
            