Manuel Scorza ... Mshairi , mwandishi wa riwaya na mwanamapinduzi
Manuel Scorza alizaliwa mnamo Septemba 7,1928 AD, katika mji wa Lima, mji mkuu wa Peru, na alikaa miaka kadhaa ya utoto wake katika mji wa Acurea katika jimbo la Huancapilica baada ya familia yake ilihamia huko.
Manuel Scorza alisoma katika Shule ya Kijeshi ya Leoncio Prado, na mnamo 1945 aliingia Chuo Kikuu cha Kitaifa cha San Marcos.
Scorza alianza shughuli zake za kisiasa wakati wa enzi ya Rais Manuel Udrea, ambapo alichapisha kitabu chake cha kwanza pamoja na kichwa "Faili za Mbali", ambacho kilisimamishwa na mamlaka ya Peru, na kumhamisha kwa Mexico mnamo 1949. Scorza alikaa miaka kumi Uhamishoni, hiyo miaka ilikuwa migumu ambayo mvulana huyo alijifunza masomo ya utu wakati hali ngumu ambayo iliacha alama za nguvu zake katika maisha yake kwa ujumla na ya kifasihi, ambapo aliweza kuigeuza kwa vipande vya mashairi venye Uhai na hamasa , ambavyo alividhihirisha kwenye mkusanyiko wake wa mashairi "Laana", ambayo aliichapisha akiwa uhamishoni mwaka wa 1955 AD.
Mnamo 1959, Scorza alipata Tuzo la Kitaifa la Ushairi kwa kitabu chake cha kwanza na hiyo baada ya kurudi kwake kutoka uhamisho, baada ya udikteta ulisitishwa . Tangu wakati huo huo, alianza awamu wa kiutamaduni mashuhuri na mpya huko Amerika Kusini ambapo alifikiria mradi wa kiutamaduni, unaolenga kuufanya utamaduni upatikane kwa kila mtu, kupitia kufanya maonyesho ya vitabu na kuviuza kwa bei nafuu. mnamo muda wa chini ya wiki moja, mkusanyiko wa vitabu vya elfu kumi na tano vilivyotolewa kwa ajili ya kuuzwa kwenye maduka , vilivyopo katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu, uliishauzwa . Uzoefu huo huo ulirudiwa kwa mafanikio sawa sawa huko Colombia, Venezuela na Cuba, ambapo vitabu vilikuwa vikichapishwa kwa bei nafuu na jukumu la wakala wa kuuza kukomeshwa, kutokana na hayo Scorza akawa mchapishaji maarufu .
Mnamo 1968, Manuel aliondoka Peru tena wakati wa migogoro iliongezeka ukali ambayo milima ya Peru ya Kati, ambapo aliingia ndani yake kwa lengo la kupata sera inayoheshimu wakazi wa asili wa India na kuwapa haki zao .
ingawa Scorza ni mshairi, ila alipata ubora wa kweli wa kifasihi kwake katika riwaya , ambayo ilimpa nafasi pana ya kuzungumzia upinzani wa wakulima wa Peru kwa hivi Riwaya yake ya kwanza " Ngoma zinapigwa kwa ajili ya Ranks " ilikuja kuwa kipindi cha kwanza cha makundi ya riwaya yanayopewa kauli mbiu mbili: "Palada" na "Vita Kimya." Riwaya hizo zilijumuisha: "Hadithi ya Garabombo Aliyefichwa", " bingwa anaye wasiwasi ", "Wimbo wa Agapito Robles", na " kaburi ya matumaini", kupitia hizo, Scorza aliweza kuchanganya ngano za kale na hadithi kwa mtazamo wa kishairi wa juu na kwa mtindo uliozifanya kuimarika hadi kiwango cha fasihi ya ulimwengu wakati wa miaka saba kuanzia (1972-1979 BK), vilevile ,zimetafsiriwa kwa lugha zaidi ya arobaini.
Mnamo 1982, Manuel Scorza alichapisha riwaya yake ya mwisho pamoja na kichwa " Ngoma isiyo na kifani." Riwaya hii ilikuwa peke yake kabisa na zilizopita. Na zinaonesha hatua mpya na mtindo mpya wa uandishi, lakini kifo kilizuia hilo, ambapo Scorza aliaga Dunia katika ajali ya ndege ya Avianca safari ya 011, ilipokaribia Uwanja wa Ndege wa Barajas katika mji mkuu wa Uhispania, Madrid, baada ya kugongana na makundi ya vilima mnamo tarehe 27 Novemba 1983 BK , ajali hiyo ilisababisha kifo cha Abiria 181, wakiwemo mhakiki wa fasihi Uruguayan Angel Rama na mwandishi wa Mexico Jorge Ibargüengoitia.