"Mama wa Wamisri" Safia Zaghloul

"Mama wa Wamisri" Safia Zaghloul

Safia Zaghloul, ni mfano wa juu wa wanawake wa Misri, shujaa wa historia katika ukombozi wa wanawake wa Misri, wa kwanza kutoka katika orodha ya mapinduzi ya Misri na mapambano dhidi ya wakoloni, akibeba bendera ya taifa,akitafutia uhuru, alikuwa na jukumu kubwa katika maisha ya kisiasa, na hakuizuia katika maisha yake yote, alibaki miaka 20 baada ya kifo cha mumewe, Saad Zaghloul, mwaka wa 1927, na amekuwa akifanya kazi yake ya kitaifa ili kuunga mkono masuala yake na kusaidia wanawake wenzake.

"Mama wa Wamisri," jina hilo la kitaifa lililoimbwa na mmoja wa viongozi walioandamana, katika umati mkubwa wa watu waliokusanyika mbele ya nyumba ya taifa, baada ya kuhamishwa kwa Kiongozi Marehemu Saad Zaghloul katika kisiwa cha Shelisheli, baada ha mapinduzi ya 1919, yale mapinduzi ya kina ya madhehebu yote ya watu yalishiriki kama wazee na vijana, wanaume na wanawake, waislamu na wakopti, na kufuatia uhamisho wake, Bi. Safia alibeba bendera ya mapinduzi kwa niaba yake, na alikuwa na taarifa katika umati huo uliotolewa na katibu wake kwa niaba yake, akisema: "Ikiwa mamlaka ya kikatili ya Kiingereza ingemkamata Saad, basi mwenzi wake wa maisha, Bi. Safia Zaghloul Mwenyezi Mungu na taifa  zima ni shahidi kubwa kwa kujiweka  nafsi yake katika mahali hapo hapo pa mume wake pa kujitoa mhanga na kuhangaika kwa ajili ya nchi, na Bi. Safia katika nafasi hiyo anajiona kuwa mama wa wana wale wote waliotoka nje wakikabiliwa na risasi za uhuru" na tangu siku hiyo alijulikana na  jina hilo, kama onesho la upendo wa watu kwake, kwa kutambua juhudi zake katika kuunga mkono waandamanaji, kuimarisha uungaji mkono wao, na kuunga mkono kazi ya kitaifa.

Katika muktadha huu, gazeti la Marekani, "Grace Thomson", lilisifu jukumu la Safia Zaghloul, likimuelezea kama "mtu mwenye nguvu, mwenye kiburi na upole". Pia lilichapisha kitabu kiitwacho "Zagloliat": ndani yake lilimwangazia Safia Zaghloul na jukumu kubwa alilokuwa nayo kati ya wanaume na wanawake baada ya uhamisho wa mume wake kutoka Misri, na jukumu lililofanywa na harakati za wanawake wakati wa uwepo wa Saad Pasha nchini humo.

Safia Mustafa Fahmy, alizaliwa mwaka wa 1878 katika familia ya kifalme, baba yake, Mustafa Pasha, Waziri Mkuu wa Misri mwanzoni mwa karne ya 19, aliolewa na Saad Zaghloul, ambaye wakati huo alikuwa Jaji wa Misri, kutoka kwa watu wa kawaida, kisha akaenda kwenye kazi ya kisiasa ya umma, alimhimiza, na alibeba bendera ya mapambano baada yake, na alikufa Januari 12, 1946, akiacha nyuma yake historia hiyo tajiri ya mapambano, uvumilivu na Jihadi kwa ajili ya Nchi.