"Njia mbadala za kiuchumi za kusini mwa Dunia" miongoni mwa Mazungumzo ya Toleo la Nne la Udhamini wa Nasser kwa mahudhurio ya Balozi wa Singapore

"Njia mbadala za kiuchumi za kusini mwa Dunia" miongoni mwa Mazungumzo ya Toleo la Nne la Udhamini wa Nasser kwa mahudhurio ya Balozi wa Singapore

Shughuli za jioni ya siku ya tatu ya" Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" katika toleo lake la nne zilihitimishwa kwa kikao cha majadiliano chenye  kichwa “ Njia Mbadala za Kiuchumi za Kusini mwa Dunia" kwa ushiriki wa  Balozi Dominic Goh, Balozi wa Singapore nchini Misri, Dkt. Samuel Egba, Mtafiti katika Kituo cha Usuluhishi Barani  Afrika katika Chuo Kikuu cha Pretoria, Giuliana Seledonio Digani, Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya ya Ushirikiano wa Kimataifa.na kikao hicho  kilisimamiwa na Ravello Prigo.


Balozi Dominic Goh, Balozi wa Singapore nchini Misri,mwanzoni mwa hotuba yake katika kikao cha mwisho cha majadiliano kilichofanyika jioni ya leo Jumamosi miongoni mwa shughuli za Udhamini wa Nasser  kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne, alieleza furaha yake ya kuhudhuria katika Udhamini huo muhimu miongoni mwa kundi mashuhuri la Viongozi Vijana wanaoshiriki kutoka nchi mbalimbali za Dunia katika toleo la nne la  Udhamini huo, wakati wa hotuba yake katika kikao hicho cha mazungumzo, alionesha tajiriba kuu ya kiuchumi ya Singapore , pamoja na kujadili Njia mbadala za kiuchumi za Kusini mwa Dunia.


Dkt Samuel Egba, Mtafiti katika Kituo cha Usuluhishi Barani Afrika katika Chuo Kikuu cha Pretoria, alisisitiza  mwanzoni mwa hotuba yake katika kikao cha mwisho cha mazungumzo kilichofanyika jioni ya leo, Jumamosi, miongoni mwa shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa  katika toleo lake la nne, kuwa ilikuwa furaha na fahari kwake kuwa katika kikao hicho muhimu cha Udhamini huo mkubwa, akiashiria katika hotuba yake kuhusu njia mbadala za kiuchumi za Kusini mwa Dunia.


Kwa upande wake, Giuliana Celedonio Dijani Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya ya Ushirikiano wa Kimataifa, mwanzoni mwa hotuba yake katika kikao cha mwisho cha majadiliano kilichofanyika jioni ya leo, Jumamosi miongoni mwa shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, alielezea furaha yake ya kuhudhuria miongoni mwa Viongozi Vijana wanaoshiriki katika toleo la nne la Udhamini huo , na shukrani zake kwa Wizara ya Vijana na Michezo kwa kuandaa Udhamini huo muhimu, na katika hotuba yake iligusia umuhimu wa kutafuta njia mbadala za kiuchumi katika Kusini mwa Dunia.

Washiriki waliuliza maswali kadhaa na uingiliaji baada ya wazungumzaji kumaliza hotuba zao katika kikao kilichofanyika mwishoni mwa Jumamosi ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa,  kilichohusu Njia mbadala za kiuchumi za Kusini mwa Dunia, na Washiriki wa Udhamini huo walipiga picha za kumbukumbu wakati wa mwingiliano,  
uchangamfu mkubwa na furaha kutoka kwa kila mtu kwa kikao hicho cha kipekee na taarifa muhimu waliyopata.

Kwa upande wake, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , "Hassan Ghazali" alieleza kuwa Viongozi mashuhuri Vijana wakishiriki katika toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kutoka nchi za ( Tanzania, Tunisia, Afrika Kusini, China, Azerbaijan, Brazil, Palestina, Sierraleone, Russia, Morocco, Oman, Jordan, Chad, Pakistan, Cameroon, Lebanon, Armenia, Niger, Mexico, na Algeria) na wameshiriki jana Jumatano katika Marathon ya Baiskeli iliyoandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo katika mji Mkuu mpya wa utawala miongoni mwa sherehe za Siku ya Baiskeli Duniani, shughuli za jana zilijumuisha kikao cha utambulisho baina ya washiriki wa Udhamini kutoka nchi mbalimbali.

Mratibu Mkuu huyo wa Udhamini huo  aliongeza kuwa warsha zilifanyika wakati wa shughuli za jana, Jumamosi, Wajumbe wa Udhamini huo wenye uwezo maalum walishiriki katika hilo -kwa mara ya kwanza - ambapo majadiliano yalifanyika kuhusu jinsi ya kuwaunganisha watu wenye uwezo maalum katika taasisi za kazi, na warsha zilishughulikia changamoto ambazo watu wenye ulemavu wanakabiliana nazo katika taasisi mbalimbali za kazi ndani ya nchi mbalimbali, pamoja na kuzungumzia jukumu la serikali, jukumu la kiraia. jamii, na jukumu la taasisi za kazi zenyewe katika kuunganisho huo, Washiriki pia wakaonesha kundi la mapendekezo  yatayopitishwa na Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimataifa katika toleo lake la nne.

Ikumbukwe kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni mojawapo ya mifumo ya utendaji ya kutekeleza mapendekezo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri;kusaidia Vijana waafrika,na kuwawezesha kuunda maoni ya kina na muhimu yanayohusishwa na masuala ya kimataifa na mipango ya Maendeleo Endelevu, na kuunga mkono fursa za kukuza jukumu la Misri Duniani kote kwani inakuja miongoni mwa mfumo wa utekelezaji wa maoni ya Misri ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030, Ajenda ya Afrika 2063, na Ushirikiano wa Kusini-Kusini.