Makumbusho ya Nubia

Kwenye kilima kirefu, karibu na Nilemeter; Ambayo ni moja wapo ya maeneo mazuri ya kiakiolojia huko Aswan, Jumba la kumbukumbu la Nubia liko kwenye eneo la mita za mraba elfu 50;Jengo la makumbusho limejengwa juu ya mita za mraba elfu 7 kutoka kwake, na mita za mraba elfu 43 kwa sehemu ya nje na maonesho wazi, tena nusu ya eneo ambalo jengo la makumbusho limejengwa lilitengwa kwa ajili ya kumbi za maonesho ya ndani ya makumbusho, na nusu nyingine kwa ajili ya maduka na urejeshaji, usimamizi wa utafiti, maeneo ya idara na huduma za umma.
Historia ya kuanzishwa kwa jumba hilo la makumbusho ilianza tangu mwanzo wa ugawaji wa ardhi katika eneo la hoteli, ambalo liko karibu na baadhi ya makaburi ya Fatimid, hadi kukamilika kwa jengo kama tunavyoona leo.
Inajulikana katika uwanja wa mambo ya kale kwamba jengo lolote kwenye ardhi ya archaeological au karibu na mambo ya kale lazima lipimwe kabla ya ujenzi, ili kuhakikisha kwamba ardhi haina mambo ya kale, au kuondoa mambo ya kale kutoka kwao, ikiwa yapo.
Uchimbaji ulianza katika uwanja wa jumba la makumbusho, ambalo lilikuwa ardhi yenye miamba kwa miezi 6 mfululizo kila siku, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi na kumalizika saa nane mchana, na wakati wa kazi ya uchimbaji, makaburi manne ya enzi ya Warumi yaligunduliwa, na makaburi hayo yalichongwa kwenye mwamba na bila maandishi, yakiwa na majeneza ya mawe ndani yake na vyombo vingine vya udongo vilivyoitwa (Infurat) kwa wingi.
Kampuni inayotekeleza mradi huo imeunda misingi ya makumbusho ya Nubia tangu 1985. Muundo wa usanifu wa makumbusho unajulikana na mtindo wa usanifu wa kinubi, ambao wabunifu waliongozwa na makaburi ya Farao, kwani makumbusho yanajumuisha sakafu kadhaa; sehemu ya chini ya ardhi: Ina ukumbi mkuu wa maonesho, maabara za urejeshaji, warsha, bohari ya vitu vya kale, kituo cha mapokezi, na ukumbi wa michezo wazi. Ghorofa ya chini: Ina lango kuu la kuingilia, ukumbi wa maonesho, ukumbi wa mihadhara, chumba cha faragha, vyumba vya usalama na usimamizi, na chumba cha meneja mkuu wa makumbusho. Ghorofa ya kwanza: Inajumuisha mkahawa, maktaba, makumbusho, vyumba vya kupiga picha, filamu ndogo ndogo, usimamizi wa makumbusho na huduma.
Jengo hilo lilibaki giza kabisa na bila umeme hadi kazi ilipoanza mnamo 1997, na takriban vitu 1,000 vya kale vililetwa kutoka kwa makumbusho matatu huko Kairo: Makumbusho ya Misri, Makumbusho ya Kiislamu, na Makumbusho ya kikoptiki. Sehemu kubwa zaidi ilikuwa kutoka kwa Makumbusho ya Misri na vilisafirishwa kwa njia ya magari 6 ya usafiri yaliyofunikwa na yenye milango ya chuma. Safari ya usafirishaji ilianza kutoka Makumbusho ya Misri alfajiri ya Julai 9 na ilidumu kwa muda wa saa 35 kupitia Bahari ya Shamu katika safari ngumu.
Baada ya kuwasili katika bohari la makumbusho, kazi ya kugawanya vitu vya kale katika vikundi vilianza moja kwa moja, kila kikundi kikiwakilisha idadi ya mahali palipopangwa kuonesha, na utekelezaji wa hali ya maonesho ulikamilishwa katika kipindi cha rekodi, na wakati huo huo sanamu za watoto wa Nubia, sheikh wao na sanamu za furaha za wanubi ziliwasili kutoka Uingereza baada ya kutengenezwa kwa njia sawa kabisa kwa watu wa Nubia, na kazi ya ujenzi ilimalizika mnamo 1996 na Makumbusho yalikuwa tayari kufunguliwa.
Jumba la Makumbusho la Nubia lilizinduliwa mnamo Novemba 23,1997 , na jioni ya siku hiyo hiyo, msanii Mohamed Mounir alitoa tamasha la kisanii kwenye jukwaa wazi katika onesho la nje la jumba la kumbukumbu, ambalo kupitia kwake aliwasilisha nyimbo zake maarufu za Nubia.
Makumbusho ya Nubia huko Aswan ni moja ya makumbusho muhimu zaidi ya Misri; kwani ni Makumbusho ya kipekee ya aina yake, nayo yana jukumu muhimu sio tu katika kiwango cha kutambulisha ulimwengu kwa urithi wa mkoa huo au katika kiwango cha kuhifadhi na kuonesha vitu vya kale kwa njia inayofaa, lakini pia katika ngazi ya kuunga mkono tafiti mbalimbali zinazofanywa na wasomi na watafiti kutoka Duniani kote kuhusu eneo hilo la Nubia, na hivyo kupitia Kituo cha Mafunzo na Vituo vya Nyaraka vilivyopo kwenye jumba la makumbusho, na kuchapisha taarifa zaidi kuhusu "Ardhi ya Dhahabu" huko Misri, siku zilizopita, za sasa na zijazo.
Na Makumbusho ya Nubia yanakuja kuendeleza katika pembe zake zote za historia na sanaa za Nubia kupitia sanamu, vichongaji, maandishi, maiti, zana, mbao za ukumbusho, mawe ya kaburi, michoro ya ukutani, n.k, kupitia maeneo 17 ya maonesho yaliyopangwa kwa mpangilio, ikiwa ni pamoja na:
eneo la Nubia, mazingira ya Wanubi, kuibuka kwa Bonde la Nile, na enzi ya kabla ya historia Ustaarabu wa Neolithic, Enzi ya Piramidi, enzi ya kati ya Wanubi, ufalme wa Wanubi wa Kush, ugani wa ustaarabu wa Misri huko Nubia, nasaba ya 25, Ufalme wa Meroe, enzi ya marehemu, Nubia ya Kikristo, Nubia ya Kiislamu, eneo la umwagiliaji, kampeni ya kimataifa ya kuokoa makaburi ya Nubia, na hatimaye sehemu ya urithi wa kienyeji .
Na Makumbusho hayo yanajumuisha vitu vya kale 5000 vinawakilisha vipindi vya maendeleo ya ustaarabu wa kimisri na urithi wa Nubia na onesho la nje la jumba hilo lina vitu vya kale vya kipekee 68 vya masanamu makubwa na michoro ya kikale yenye uzito mbalimbali na miongoni mwa makumbusho mazuri na nadra Mifupa ya binadamu, umri wake miaka laki 2, ilikutwa mwaka wa 1982 katika eneo la Edkobate mkoani Aswan na pia jengo la jumba hilo lilipata tuzo ya jengo bora zaidi mnamo mwaka 2001.
Vyanzo:
Tovuti ya Taasisi kuu ya Taarifa.
Gazeti la Al Ahram la Kimisri.