Ushirikiano wa pande mbili kati ya Kenya na Zimbabwe katika maeneo saba
 
                                Imetafsiriwa na: Walaa Marey
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza Jumatano 9/3 kutia saini makubaliano mapya saba kati ya nchi hiyo na Zimbabwe kufuatia mazungumzo na Rais Emmerson Mnangagwa.
Viongozi hao wawili walikutana katika Ikulu ya Nairobi siku moja baada ya Mnangagwa kuwasili kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.
Mkutano huo umekuja siku moja baada ya Kamati ya Kudumu ya Pamoja ya Kenya na Zimbabwe kukutana ili kuweka msingi wa mazungumzo ya ushirikiano wa sekta mtambuka yenye lengo la kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo mbili.
Ikumbukwe kuwa mikataba iliyosainiwa ilihusu nyanja za mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia, utalii na ulinzi wa wanyamapori, uchunguzi wa ajali za ndege za kiraia na ajali mbaya, kukuza uwezeshaji wa wanawake na maendeleo ya jamii, masuala ya vijana, vyama vya ushirika, michezo na burudani.
Mbali na makubaliano hayo, Rais Kenyatta pia alitoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo vikali vilivyowekwa dhidi ya Zimbabwe na jumuiya ya kimataifa, ambavyo alisema vimesababisha matatizo ya nchi na akaongeza: "Tulisisitiza dhamira yetu thabiti ya kuendelea kuiunga mkono Zimbabwe dhidi ya vikwazo visivyo halali ambavyo vimewekwa dhidi ya nchi hiyo ambavyo vinaendelea kusababisha matatizo, masuala na matatizo yasiyo ya lazima kwa watu wa Zimbabwe na hili ndilo tunaloona kuwa sio la haki.
Kwa upande wake, Mnangagwa alisema "Mkutano huu ni maendeleo mazuri yanayoonesha kuwa uhusiano wetu unasonga mbele katika mwelekeo sahihi. Kupitia Utekelezaji wa hati zetu za makubaliano, uchumi wetu utabadilishwa ili kukidhi viwango vya juu vya maisha kwa watu wetu."
 
                         
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
             
            
                                        
                                     
            
            