Ushirikiano wa Kusini-Kusini

Ushirikiano wa Kusini-Kusini

Imetafsiriwa na: Hussein Mohammed 
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Ushirikiano kati ya nchi za Kusini na watu wake unakuja kufikia malengo ya maendeleo endelevu, na kuondokana na uharibifu wa virusi vya Corona vilivyosababisha kushuka kwa uchumi, na ushirikiano kati ya nchi za Kusini pia unachangia kupunguza umaskini, na jukumu la Umoja wa Mataifa katika kusaidia nchi zinazoendelea kupitia ushirikiano kati yao.

Majadiliano ya Kusini na Kusini yatafanyika ili kuhakikisha mustakabali bora katika sekta ya kusini mwa dunia kwa kuzingatia janga la Corona, na kuonesha ufuatiliaji wa kikao cha 20 kwa ushirikiano na nchi za Kusini, kilichofanyika kutoka 1 hadi 4 Juni 2021 huko New York.

Mifano muhimu ya ushirikiano wa Kusini-Kusini ni pamoja na uzoefu wa Mexico katika kutofautisha mahindi ili kuboresha hali ya afya ya Kenya, kuimarisha uwezo wa nchi zinazoendelea kutatua matatizo yao, kuimarisha uwezo wa kiteknolojia katika nchi zinazoendelea na kuunda uwezo mpya, na mifano mingine ya ajabu inayoonesha umuhimu wa ushirikiano wa Kusini-Kusini.