Angola: Uzinduzi wa Kiwanda cha Utengenezaji na Uunganishaji wa Pikipiki

Angola: Uzinduzi wa Kiwanda cha Utengenezaji na Uunganishaji wa Pikipiki

Imetafsiriwa na: Malak Diaa
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Waziri wa Viwanda na Biashara wa Angola, Victor Fernandes, alizindua kiwanda maalumu cha utengenezaji wa pikipiki siku ya Jumamosi, Machi 11, katika Kituo cha Maendeleo cha Viana huko Luanda. Mpango huu unatekelezwa kwa ushirikiano na kundi la biashara la NIODIOR, linalowekeza dola milioni 15 katika mradi huu.

Kiwanda hiki pia kinakusanya pikipiki za magurudumu matatu, bajaji (zikiwa na magurudumu mawili ya nyuma yenye uwezo wa kubeba tani moja), pampu za pikipiki, pamoja na magari ya wagonjwa na bajaji maalumu kwa ajili ya usafi wa mazingira.