Mwanafasihi wa Guatemala Miguel Ángel Asturias

Mwanafasihi wa Guatemala Miguel Ángel Asturias

Imetafsiriwa na/ Ahmed Magdy
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled  


Mwanafasihi yule Mweledi Miguel Ángel Asturias amezaliwa Guatemala tarehe 19 mwaka 1899 , ambapo alikuwa na umahiri wa kuwa mshairi, mwandishi wa riwaya, mwandishi wa tamthilia, mwandishi wa habari na mwanadiplomasia, ambapo anazingatiwa kuwa mmoja wa wanafasihi wenye ufanisi mkubwa zaidi huko Amerika ya kilatini, alishikilia fikra ya kuzifanyia upya mbinu za kuandika na uhalisia wa mazingaombwe uliojitokeza kwa kiwango kikubwa ukiunda harakati ya (Alboom) , katika fasihi ya uhispania ya kimarekani mnamo miaka ya 60 ya karne ya 20. 

Pia alisoma uanasheria katika chuo kikuu cha San Carlos huko Guatemala, ambapo alishiriki katika mapambano yaliyokuwa dhidi ya udekteta wa “  Estrada Cabrera”  hadi kumuondoa mnamo mwaka 1920, na baada ya miaka miwili alianzisha na alitawala chuo kikuu cha kiraia, na sambamba na hilo alianza kuyachapisha maandishi yake ya mwanzo , halafu akasafiri ulaya jambo ambalo lilimsogeza kwa harakati za kifasihi na itikadi za kifikra, zilizokisaidia kwa kiwango kikubwa kipaji chake cha kifasihi, na huko alisoma lugha za Maya na Elimu ya binadamu na maendeleo yake ya awali, katika chuo kikuu cha Sorbonne pamoja na mmarekani Jorge Reno 

Mnamo mwaka 1933 alirudi Guatemala, ambapo alikuwa anafundisha chuoni, halafu akaanzisha jarida la “Diario Del Aire “ linalozingatiwa kama jarida la kwanza la vyombo vya habari , na haya yalikuwa maisha ya Asturias yaliyojaa utamaduni na utaalamu, na mnamo kipindi cha mapinduzi cha kati ya 1944 na 1954 Asturias alishika vyeo tofauti vya kidiplomasia, na mnamo mwaka 1966 aliipata tuzo ya Lenin ya amani, na pia tuzo ya Nobel ya fasihi mwaka 1967 

Kazi ya fasihi ya kwanza aliyofanya kwa ufanisi ilikuwa “ visaasili vya Guatemala “ ambapo ni mkusanyiko wa hadithi za kubuniwa na za mazingaombwe zilizojitokeza huko Paris pamoja na utangulizi wa Paul Ferry , na baadhi ya riwaya kama vile: “ Mheshimiwa R (1946) , “ Bwana wa Atomu” (1949) , “ likizo kwenye Guatemala”(1955) , “ Kioo cha Lida Sal “  (1967), “ jua tatu miongoni mwa nne “ 1971 pamoja na kazi nyingi za kifasihi za aina zake  tofauti.

Kuhusu riwaya yake maarufu zaidi “ Mheshimiwa Rais “ ambapo umaarufu wake ulitokana na kuyashughulikia maisha kwenye Guatemala wakati wa kipindi cha udekteta wa “Estrada Cabrera “, ambapo alitia fora katika kumithilisha udekteta kwa mtindo mzuri wa kueleza matukio unaoakisi kipindi alichoishi huko ulaya , na mwandishi alisema kuhusu riwaya hiyo: “ nilihisi kwa hofu, kukosekana kwa utulivu na kiwewe kilichoakisiwa na kazi hiyo” 

Ndani ya riwaya yake ya “ Bwana wa Atomu” unaweza kuona uhalisia wa mazingaombwe unaojitokeza katika kazi zake zote za kifasihi, na pia anawakilisha ushahidi wa maendeleo ya wanadamu kutoka jamii ya awali hadi imekuwa ulimwengu wa sasa wa kiupebari.

Kuhusu fikra zake za kisiasa Aatorias alikuwa mpiganaji mkali wa kisiasa, ambapo alipohamishwa huko “Buenos Aires” , alifanya safari nyingi katika Marekani ya kilatini na katika nchi ya Hindi , China na Urusi, ambapo alikuwa anawahamasisha watu bila ya kupata taabu , na msajili wa matukio ya zama pamoja na kuipinga siasa ya muungano, na alipomunga mkono “ Kastro “ alifukuzwa kutoka Argentina mwaka 1962 , halafu akarudi Ufaransa uliompokea kwa furaha kubwa, na alitembelea Moscow uliomtunuku tuzo ya Lenin ya amani mwaka 1966 , kabla ya kupata tuzo ya Nobel ya fasihi mwaka 1967, na alipochaguliwa na serekali ya Mends Montenegro ili kuwa balozi huko Paris alianzisha onesho la urithi wa lugha za Maya kwenye ikulu ya nchi , kwa msaada wa André Marlo waziri wa utamaduni wa Ufaransa wakati huo na alipewa heshima ya chuo kikuu cha Sorbonne mnamo mwaka 1968.

Mwishoni mwa maisha yake Asturias alishiriki kwenye mkutano wa amani wa Helsinki, na katika mazungumzo ya chuo kikuu cha Dakar kuhusu weusi na Marekani ya kilatini, na alitaka sana kupatikana kwa maelewano ya kimataifa kuhusu uhalali wa tamaduni zinazowabagua watu . 
_ na Asturias alifariki alipokuwa huko Madrid , novemba tarehe 9 mwaka 1974, alipokuwa anatoa jitahada nyingi na kuipa maktaba ya taifa ya Paris maandishi yake, iliyofanya sherehe kubwa ya kumwaga .


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy