Abdel Nasser na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF)

Abdel Nasser na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF)

Imefasiriwa na / Aya Nabil

Uimarishaji wa uhusiano wa kimisri na kiafrika ulikuwa lengo la Rais Gamal Abdel Nasser, na imani yake katika jukumu la michezo katika ukaribu wa watu,hii ilimfanya afikirie kuanzisha Shirika ambalo lingeshughulikia masuala ya Soka ndani ya bara, kwa hivyo aliwakabidhi  wale wanaohusika na Soka nchini Misri kuzingatia   Afrika ili kuimarisha mahusiano.

Mnamo Juni 1956, na pembezoni mwa  Mikutano ya FIFA Congress iliyofanyika  katika mji mkuu wa Ureno, Lisbon; Mhandisi Abdulaziz Salem, Mkuu wa Shirikisho la  Soka la Misri, Mohamed Latif na Youssef Mohamed, Bw. Abdel Rahim Shaddad kutoka Sudan, Badawi Mohamed, Dkt. Abdel Halim Mohamed, na mwafrika Kusini William Phil walikutana kuandaa mpango wa kuanzisha Shirikisho la Soka la Afrika. (Baraza kuu la Soka Barani ani Afrika).

Mkutano huo ulitanguliwa na mikutano ya FIFA Congress mwaka 1954, huko Bern, Uswisi,  na ilipigwa kura kutambua Afrika kama Shirikisho la bara, na kulipatia bara hilo haki ya kumteua mwakilishi wake wa kwanza katika Kamati ya Utendaji, Abdel Aziz Abdullah Salem kutoka Misri.

Mnamo Februari 8, 1957, wawakilishi wa Misri, Sudan, na Afrika Kusini walikutana, na wawakilishi wa Shirikisho la Ethiopia walijiunga nao, kwenye Hoteli ya Grand katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, na mswada wa sheria ulitayarishwa, na kuandaa toleo la kwanza la Kombe la Mataifa ya Afrika lilijadiliwa.

Baada ya kuidhinisha kwa mswada wa sheria , Mmisri Abdel Aziz Abdullah Salem alichaguliwa kuwa Mkuu kwa kauli moja, hivyo kuwa Mkuu wa kwanza katika historia ya Shirikisho hilo.

Siku ya kumi ya mwezi huo wa Februari, na baada ya mkutano wa kwanza wa Baraza Kuu la Shirikisho, mji mkuu wa Sudan ulishuhudia kuzaliwa kwa Kombe la Mataifa ya Afrika, ambalo Misri ilishinda toleo lake la kwanza, na huo ukawa mwanzo wa tukio lililojaa furaha na uchangamfu na matukio mengi yasiyosahaulika hadi leo, na hatua katika njia ya kufafanua sura na sifa za Soka la Afrika.

Makao makuu ya CAF kwa sasa yako katika mji mkuu wa Misri, Kairo.

Vyanzo

Tovuti rasmi ya CAF.