Teknolojia yachangia kuenea kwa lugha ya Kiswahili

Imeandikwa na/ Noureldin Mahmoud
Lugha ya Kiswahili ni mojawapo ya lugha zinazozungumzwa zaidi barani Afrika, ikitumika na watu wapatao milioni 200 katika zaidi ya nchi 20 katika pwani ya mashariki ya bara, ikiwemo Kenya na Tanzania. Teknolojia imekuwa na jukumu muhimu katika kueneza lugha hii kwa kasi zaidi kuliko hapo awali, iwe ndani ya bara au kimataifa. Katika makala hii, tutachunguza jinsi teknolojia imechangia kueneza lugha ya Kiswahili na kuimarisha nafasi yake katika jukwaa la dunia.
Mitandao ya kijamii ina mchango mkubwa katika kueneza lugha ya Kiswahili. Majukwaa kama vile X (zamani Twitter), Facebook, na Instagram yamekuwa njia kuu ya mawasiliano kati ya wazungumzaji wa Kiswahili na jamii nyingine. Kupitia majukwaa haya, maudhui ya Kiswahili yanashirikiwa ikiwemo video, picha na maandishi ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uelewa wa lugha na kuongeza idadi ya wazungumzaji. Kwa mfano, kampeni ya #SwahiliChallenge kwenye jukwaa la X ilivutia watumiaji wengi, na ikisaidia kueneza msamiati na misemo mipya ya Kiswahili.
Programu za kielimu zimechangia usambazaji na ufundishaji wa lugha ya Kiswahili, zikiwemo Duolingo, inayofundisha Kiswahili kupitia masomo ya kufurahisha, rahisi, na yasiyo na utata. Clozemaster huwawezesha watumiaji kufanya mazoezi ya Kiswahili kwa kujaza nafasi tupu katika sentensi na kukagua maneno na misemo ya kawaida. Drops husaidia kujifunza msamiati mpya kwa haraka na kwa ufanisi kupitia picha na michezo mifupi. Pimsleur hulenga kuboresha ujuzi wa kuzungumza na kusikiliza. Programu hizi zimefanya kujifunza Kiswahili kupatikana kwa kila mtu.
Uzalishaji na ushirikishwaji wa maudhui ya sauti na video kwa lugha mbalimbali umekuwa jambo la kawaida kutokana na majukwaa kama vile YouTube na Spotify. Kuna idadi kubwa ya vituo na podcast zinazotolewa kwa lugha ya Kiswahili, ambazo huangazia mada mbalimbali zikiwemo elimu, burudani, habari, na utamaduni. husaidia kueneza lugha na kuimarisha uelewa wake kati ya hadhira pana. Kwa mfano, kituo cha Learn Swahili with David kwenye YouTube na Swahilipod101.com.
Tovuti na vikao huchangia katika usambazaji wa lugha ya Kiswahili kwa kutoa makala mbalimbali, zikiwemo habari, blogu binafsi, utafiti wa kisayansi na masomo ya kitaaluma, hii hutoa fursa za mwingiliano na ushirikishwaji kati ya wazungumzaji wa Kiswahili na wengine wanaopenda kujifunza na kuitumia lugha hiyo.
Pamoja na maendeleo ya teknolojia, Kiswahili kimekuwa lugha rahisi na ya kujifunza, na nafasi ya kueneza lugha hii na kupanua wigo wake wa wazungumzaji inatarajiwa kuongezeka katika siku zijazo.