Kiswahili na Ulimwengu wa Nje

Kiswahili na Ulimwengu wa Nje

Imeandikwa na/ Basmala Ayman Mohamed 

       Kuna zaidi ya lugha 6900 ulimwenguni, lugha yoyote inahusiana na kundi la watu au nchi fulani. Ambapo lugha ni mojawapo ya mhimili unatusaidia kuwasiliana, na vilevile ni mojawapo ya mambo yaliyo muhimu zaidi duniani. Lugha ya Kiswahili miongoni mwa lugha hizi. Kama kawaida lugha zote zina historia fulani na maendeleo. Pia kuna vitu vinaathiri lugha hizi. Na lugha ya Kiswahili kama lugha yoyote, ina historia, maendeleo na imeathiriwa na vitu vingine. 

      Lugha ya Kiswahili imeanzishwa kwenye Afrika Mashariki. Waarabu walianza kuandika Kiswahili kwa herufi ya Kiarabu tangu karne ya 1 Hijria, imesalia kuandikwa kwa lugha ya Kiarabu kwa karne kadhaa hadi miishoni mwa karne ya 18, ukoloni wa Ulaya umebadilisha kuandika kwake kwa herufi ya Kilatini ambayo ilikuwa lugha za Ulaya zote zimeandikiwa sasa. Kufikia waarabu hadi pwani za Afrika Mashariki kulisaidia kwa ukubwa katika kuandika lugha hii kwa herufi ya Kiarabu. Ingawa kutumia herufi za Kilatini katika kuandika lugha ya Kiswahili, lakini lugha ya Kiswahili imeathiriwa kwa lugha ya kiarabu kwa ukubwa na katika lugha ya Kiswahili kuna baadhi ya maneno ya maazimio kutoka lugha ya Kiarabu; kiwango cha maneno ya Kiswahili ya maazimio kutoka lugha ya Kiarabu kimefikia kwa zaidi ya 27% miongoni mwa misamisti yote ya lugha ya Kiswahili, pia kuna baadhi ya maneno ya maazimio kutoka lugha ya Kiingereza, Kijerumani na Kireno, na hiyo kutokana na biashara iliyokuwa kuaimarishwa kwenye pwani za Afrika Mashariki tangu karne kadhaa zilizopita.

    Kuna nchi nyingi zinaongea Kiswahili kama vile: Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na baadhi ya nchi nyingine katika Afrika Mashariki. Lugha ya Kiswahili inatumiwa kama lugha rasmi huko nchini Tanzania. Pia ni lugha ya elimu katika sehemu ambazo kabla ya sehemu ya chuo kikuu. Pia ni lugha rasmi ya pili baada ya  Kiingereza huko nchini Kenya, ni lugha ya kibiashara na ya kitaifa huko nchini Uganda na lugha ya kimawasiliano katika nchi nyingine za Afrika Mashariki. Zaidi ya watu milioni 200 wanaoongea kwa lugha hii. Na lugha hii ni mojawapo ya  lugha 10  zinazoenea zaidi ulimwenguni. Umuhimu wa kimataifa wa lugha ya Kiswahili umeongezeka katika enzi ya kisasa; inafundishwa kwenye vyuo vikuu vya kimataifa kama: katika Chuo Kikuu cha London  York huko nchini Uingereza, Sorbonne huko nchini Ufaransa, Cologne nchini Ujerumani, Washington na West Virginia huko Marekani, pia huko nchini Misri kuna majaribio mema ya watafiti ili kueneza lugha hii kama jaribio la “lugha yangu ni kiafrika” linazingatia kufundisha lugha ya Kiswahili na lugha za Kihausa na Mandinko. Pia lugha ya Kiswahili inatumiwa katika Matangazo ya redio katika redio nyingi za kimataifa kama: BBC ya Uingereza (BBC), Redio ya Ujerumani (DW), vituo vya redio vilivyoelekezwa Moscow, Kairo, na Beijing, Sauti ya Amerika (VOA) na nyingine.   

   Biashara inasaidia kuimarisha mawasiliano baina ya watu kupitia ubadilishanaji wa kibiashara, hiyo inasaidia katika ubadilishanaji wa lugha, lahaja na misamisti baina ya nchi tofauti. Mahusiano ya kibiashara inasaidia kuzinakili maarifa na teknolojia mpya. Kwa hiyo lugha inafanya jukumu wazi la kuzinakili maarifa baina ya watu kwa hiyo maarifa yanaongezeka duniani na itakuwa kuna uwazi baina ya nchi nyingine. Pia inawezekana biashara inasaidia katika kuendeleza misamisti, kiasi kuwa wafanyabishara wanatumia misamisti mingine, kwa hiyo kuna misamisti mipya imeingizwa katika Kiswahili na itaimarishwa sana.

     Biashara inasaidia kuienea Kiswahili, kiasi kuwa inawahimiza wafanyabiashara kwa mawasiliano ya kitamaduni na kilugha baina ya nchi na jamii katika Afrika Mashariki. Hiyo inaimarisha kutumia  Kiswahili kama lugha ya pamoja baina ya watu, wafanyabiashara na jamii tofauti, pia biashara inasaidia kuienea lugha hii ulimwenguni kote, kwa hiyo biashara inaashiria umuhimu wa kujifunza lugha hii na kuijali. Pamoja ya hayo Waswahili walikuwa na umaarufu kwa ufanisi wao wa kuabiria bahari na biashara ya baharini na kupitia biashara yao hii, lugha ya Kiswahili imeenezwa kwa kiasi kikubwa ulimwenguni kotem 

        Pia biashara ya kimataifa ni miongoni mwa mambo yanayosaidia kwa ukubwa ili kuendeleza lugha ya Kiswahili na kuienea, kiasi kuwa lugha ya Kiswahili inatumiwa katika mahusiano ya kibiashara na mawasiliano ya siku katika maeneo yanayojaa kwa biashara ya kimataifa na hiyo inaongeza kuienea na kuitumia. Pia kutumia kwa lugha ya Kiswahili katika vyombo tofauti vya habari kama redio na televisheni au vyombo vya kielektroni vya habari kama mfano Facebook kunasaidia kuienea kwa maana ya kuna wengi wanaovisikia au kuvisoma kupitia vyombo hivi vya habari. Kwa hiyo biashara ina jukumu muhimu ili kuimarisha lugha ya Kiswahili na kuienea na hiyo inasaidia kuitumia kwa ukubwa ulimwenguni kote. 

    Mwishoni mwa lugha ya Kiswahili ni mojawapo ya lugha muhimu ulimwenguni kote, Pia ni mojawapo ya lugha ambazo ulimwengu unajaribu kuziimarisha na kuzieneza. Pia ilibainishwa kuwa kuna nchi na watu wengi wanaojua kuwa Kiswahili na kuna wanaoijifunza pia. Tunalazimisha kuijali ili itakuwa maarufu na itaimarishwa kwa ukubwa. Itabainishwa pia kwamba kujifunza lugha ya Kiswahili ni mojawapo ya mambo yaliyo muhimu zaidi ili kubadilishana utamaduni na kuwasiliana na wanaoiongea.