Odinga mgombea urais wa Kenya

Odinga mgombea urais wa Kenya

Imetafsiriwa na: Islam Adel
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amechaguliwa rasmi kuwa mgombea wa uchaguzi ujao na zaidi ya vyama 22 vya kisiasa.

Vyama vya kisiasa vinavyounda muungano wa Azimu La Umoja, ambavyo vilisababisha 'handshake' ya 2018 kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga, vilifanya uamuzi wa kumuunga mkono Odinga katika uchaguzi wa Agosti 6, 2022 wakati wa mkutano wa wajumbe wa kitaifa.

Rais Kenyatta ametangaza rasmi kuunga mkono azma ya Odinga kuwania urais baada ya mazungumzo ya muda mrefu ya kisiasa na Stephen Kalonzo Musyoka, aliyekuwa Makamu wa Rais Mwai Kibaki.

Baada ya kuteuliwa Nairobi kuwa mgombea wa vyama vya siasa aliyetajwa, Odinga alisema: "Lugha haina usemi. Nashukuru kwa kazi hii. Umenikabidhi bendera ya vuguvugu la kitaifa la kidemokrasia."

Katika barua yake ya kukubali, aliongeza, "Nitafanya kazi na msaada wako unaoendelea. Hakuna mtu aliyefikiria kwamba vyama vilivyopigana katika pande tofauti za 2013 vitakuwa na umoja. Hali hii imebadilisha historia ya siasa zetu."

Katika hotuba yake kabla ya Raila Odinga kualikwa jukwaani, Rais Uhuru Kenyatta, kwa upande wake, alimpongeza Musyoka kwa kukubali kumuunga mkono Odinga."Tumeamua kwamba kuundwa kwa serikali itakuwa mpango jumuishi," Rais Kenyatta alisema.

Kenyatta aliwakaribisha wagombea kadhaa wameofichua matarajio yao ya kisiasa ya kuongoza nchi.

Odinga alisema ataongoza juhudi za kupambana na umaskini, kuendeleza makazi, kuhakikisha haki za wanawake, kupambana na kukata tamaa na kuendeleza ajenda ya vijana.

Harakati ya Odinga cha Orange, Chama cha Jubilee cha Rais Kenyatta, Chama cha Mop na vyama vingine vilitia saini Mkataba wa Umoja, wakirejelea uungaji mkono wao kwa mgombea Odinga.

Katika uchaguzi wa urais, Odinga atakabiliana na Naibu Rais William Ruto ambaye ni mwaniaji wa chama cha Muungano wa Kidemokrasia.

Odinga pia aliahidi kuhakikisha msaada wa kilimo, teknolojia ya kilimo, upatikanaji wa bima ya afya, na kuongeza msaada wa kifedha kwa mamlaka za majimbo 47 nchini.

Pia aliahidi kupambana na ufisadi, kuhakikisha huduma za elimu kwa watoto wote nchini Kenya na kuwaajiri vijana katika taasisi muhimu za umma wakati wa urais wake.

Odinga alisema ataendelea kutetea kanuni ya mwelekeo wa Afrika na kukabiliana na mgogoro wa madeni ya umma.

Kenya itaendelea kuchukua majukumu muhimu katika siasa za bara na kimataifa kwa kuendelea na mpango wa barabara uliowekwa na serikali ya Rais Kenyatta.Odinga bado hajafichua mgombea mwenza wake wa urais.