Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wafunga maombi na kuchapisha takwimu za waombaji

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wafunga maombi na kuchapisha takwimu za waombaji

Wizara ya Vijana na Michezo ilitangaza kufungwa kwa fomu ya maombi ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne na kuchapisha takwimu wazi za waombaji wa Udhamini huo mwaka huu, ambapo taarifa yake ilisema kuwa jumla ya waombaji wa Udhamini huo walifikia viongozi vijana wapatao 1,185 kutoka nchi 90 Duniani kote, na hivyo iko na kauli mbiu ya "Vijana wa Kutofungamana kwa upande wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini" tena pamoja na Ufadhili wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri. 

Kulingana na taarifa ya Wizara hiyo, bara la Afrika liliwakilisha 84.7% ya waombaji wote wa Udhamini huo, na bara la Asia liliwakilisha 11.2%, wakati bara la Ulaya lilitoa karibu na 2.4%, pamoja na 0.9% ya bara la Amerika Kusini, na bara la Amerika Kaskazini liliwakilisha karibu na 0.4% ya waombaji wote, wakati bara la Australia linawakilisha karibu 0.4% tu ya jumla ya idadi ya waombaji wa Udhamini huo.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa kiasi cha waombaji wa Udhamini kiko na jinsia zote mbili, hivi waombaji wa udhamini wa wanaume ilifikia 63%, ambapo wanawake ikifikia 37% ya idadi ya waombaji wote, ikiwa ni pamoja na 2.7 % ya watu wenye Ulemavu kutoka mataifa mbalimbali.

Katika muktadha unaohusiana, Udhamini wa Nasser ulikuwa umetangaza kuwa kundi lengwa lina umri kati ya miaka 20 hadi 35 kutoka nyanja na digrii tofauti za viongozi vijana wanaofanya kazi katika jamii zao, na ipasavyo, asilimia ya waombaji wa Udhamini kutoka kwa wenye shahada ya Uzamivu ilikuwa karibu 5.7%, pamoja na 6.4% asilimia ya waombaji kutoka kwa wenye Uzamili wa kiufundi, wakati shahada ya Uzamili wa kitaaluma ilifikia 20.5% ya waombaji wote, pamoja na karibu 4.9% ambao bado wako katika masomo ya Uzamili na karibu 7.9% yao wana Diploma pamoja na 41.8% ya waombaji wa Udhamini kutoka kwa wenye shahada ya kwanza, wakati kiasi cha waombaji kutoka hatua ya awali ya kuhitimu ilikuwa takribani 12.8% ya waombaji wote wa Udhamini huo.

Ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne hivi karibuni umepokea Udhamini wa Uandishi wa habari kutoka kwa Mamlaka ya Kitaifa ya Uandishi wa habari, pamoja na Ufadhili wa kisiasa kwa mara ya tatu mfululizo kutoka kwa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, na umepangwa kufanyikwa  mnamo Juni ijayo ya 2023.