Vijana na uzoefu wa Ukuaji... Ni Changamoto hadi Fursa" ni miongoni mwa Mazungumzo ya Toleo la Nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Vijana na uzoefu wa Ukuaji... Ni Changamoto hadi Fursa" ni miongoni mwa Mazungumzo ya Toleo la Nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Ndani ya shughuli za "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne, linalofanyika likiwa na Ufadhili wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, na hubeba kauli mbiu "Vijana wa Kutofungamana kwa upande wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini", na ushiriki wa Viongozi Vijana 150 Duniani kote, mnamo kipindi cha Juni mosi hadi Juni 15.

Shughuli za siku ya 10 zilifunguliwa na kikao cha mazungumzo kilichoitwa "Uzoefu wa Vijana na Ukuaji: Kutoka Changamoto hadi Fursa" na: Ahmed Al-Sabbagh, Mwakilishi wa Mkoa wa Utawala, Amani na Usalama katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika Kikundi Kikuu cha Vijana cha Umoja wa Mataifa, na Dkt. Sameh Kamel, Mwenyekiti wa Kikundi Kikuu cha Umoja wa Mataifa cha Watoto na Vijana, kwa mahudhurio ya Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kikundi cha viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo, wataalamu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari.  

   

Kwa upande wake, Ahmed Sabbagh, Mwakilishi wa Mkoa wa Utawala, Amani na Usalama katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika Kikundi Kikuu cha Vijana cha Umoja wa Mataifa, alijadili jinsi ya kufikia Ajenda ya Maendeleo Endelevu kama usambazaji wa haki wa rasilimali bila kuathiri vizazi vijavyo, Al-Sabbagh pia aligusia juu ya mazungumzo ya muda, ambayo baadhi huyafafanua kama makubaliano bila kujisalimisha yaliyofikiwa na pande hizo mbili, akimaanisha mazungumzo yanayofanywa na nchi, pamoja na mazungumzo ya mtu binafsi, na kusisitiza kuwa matatizo mengi yanayotukabili katika bara la Afrika ni kwamba kila wakati tunaafikiana badala ya kuungana, haswa kwa kuwa kila sehemu Barani Afrika ina tabia maalum, na kwamba matatizo ya Afrika hayahitaji matumizi ya suluhisho moja, na kuwashauri vijana, akisema:  Kama unataka kubadilisha kitu chochote katika jamii, tunapaswa kujibadilisha kwanza."

Wakati wa hotuba yake, Dkt. Sameh Kamel, Mwenyekiti wa Kikundi Kikuu cha Umoja wa Mataifa cha Watoto na Vijana, alielezea jukumu la ulinzi wa kijamii kwa vijana na jukumu la Umoja wa Mataifa katika suala hili, akionyesha kuwa uamuzi katika Umoja wa Mataifa hapo zamani ulizingatia kile nchi wanachama wanaona hadi hali ilibadilika baada ya Mkutano wa Dunia uliofanyika Rio de Janeiro, ambapo ulizunguka mada kuu mbili, mabadiliko ya hali ya hewa na uendelevu, na mkutano huo ulitoka na mapendekezo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kwamba sio sauti zote zinaonesha Ukweli katika nchi, hivyo mfumo wa vikundi vikubwa ulianzishwa ukigawanya katika makundi 9, kuelezea vikundi vyote katika jamii.

Kwa upande wao, washiriki katika toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa waliuliza maswali kadhaa, baada ya wasemaji vijana kumaliza hotuba zao wakati wa kikao, na kisha washiriki walipiga picha za kumbukumbu katikati ya mwingiliano, ukarimu mkubwa na furaha na kila mtu na kikao hiki cha mazungumzo na habari muhimu waliyopata.

Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini huo alielezea kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unakuja kama mfano wa maoni ya serikali ya Misri na juhudi zake za kuongeza jukumu la vijana ndani na kimataifa, na kuwawezesha kuwa na zana za uongozi na kazi za kisiasa na kijamii, kama matoleo mbalimbali ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kuendelea ndani ya muktadha wa nia ya kuhamisha mbinu ya uzoefu wa Misri katika kujenga jamhuri mpya, na kujenga msingi wa uwezo wa vijana wenye kuahidi.

Ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni moja ya njia za utendaji kutekeleza mapendekezo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kusaidia uwezo wa vijana wa Afrika, kuwawezesha kujenga maono kamili na muhimu kuhusiana na masuala ya kimataifa na mipango ya Maendeleo Endelevu, na kusaidia fursa za kukuza jukumu la Misri Duniani kote.