Washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa watembelea Piramidi za Giza na Saqqara

Washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa watembelea Piramidi za Giza na Saqqara

Washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne walitembelea eneo la Piramidi za Giza na Saqqara, Kwa mahudhurio ya Balozi Obaid Boama Akwa, Balozi wa Ghana huko Kairo,aliyekuwa na nia ya kushiriki na ujumbe wa vijana wa Ghana kushiriki katika Udhamini huo wa kuwatembelea, kuona maeneo ya akiolojia katika mkoa huo na Piramidi tatu, kisha washiriki walimaliza ziara yao kwa kutembelea eneo la Sphinx.

Washiriki hao walionesha furaha yao kubwa na kile walichokiona juu ya hazina za akiolojia za ustaarabu wa kale wa Misri na ukubwa wa ujenzi wa Piramidi, wakieleza shukrani zao kubwa kwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, kwa mabadiliko ya kiitamaduni yaliyoshuhudiwa na Misri katika ukuaji wa miji na ujenzi, ambapo asili ya zamani inaungana na sifa ya sasa, wakisifu ukuu wa Misri, makaburi yake, historia na urithi wa kale.

Washiriki pia walituma ujumbe wa Twitter kupitia kurasa zao za kibinafsi kwenye mitandao ya kijamii, wakimshukuru Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, kwa nia yake ya mara kwa mara ya kudhamini na kuandaa matukio ya vijana wa kimataifa, na kufanya kila juhudi na ndugu katika nchi tofauti ili kufanikisha ufufuaji wa vijana katika nyanja mbalimbali, na kushare picha waliozipiga kutoka eneo la Piramidi za Giza, pamoja na kuelezea furaha yao kubwa kuona moja ya maajabu ya saba ya Ulimwenguni.

Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, alielezea kuwa Udhamini huo unakuja kama mfano wa maono ya serikali ya Misri na juhudi zake za kuongeza jukumu la vijana ndani na kimataifa, na kuwawezesha kuwa na zana za uongozi na kazi za kisiasa na kijamii, kama matoleo mbalimbali ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa yanayoendelea ndani ya muktadha wa nia ya kuhamisha mbinu ya uzoefu wa Misri katika kujenga jamhuri mpya, na kujenga msingi wa uwezo wa vijana wenye kuahidi, ambapo aina zote za msaada, ukarabati na mafunzo hutolewa kwa vijana wanaoshiriki katika Udhamini huo, mbali na kuandaa ziara za shamba na vikao vya majadiliano na mazungumzo katika nyanja mbalimbali ili kupanua upeo na maoni ya vijana, na kuwawezesha kuunda maono kamili na muhimu yanayohusiana na masuala ya kimataifa na mipango endelevu ya Maendeleo.

Ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni moja ya njia za utendaji kutekeleza mapendekezo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kusaidia uwezo wa vijana wa Afrika, kuwawezesha kujenga maoni kamili na muhimu kuhusiana na masuala ya kimataifa na mipango ya maendeleo endelevu, na kusaidia fursa za kukuza jukumu la Misri duniani kote, kama inakuja ndani ya mfumo wa kutekeleza maoni ya Misri kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, Ajenda ya Afrika 2063, na Ushirikiano wa Kusini-Kusini.