Mjumbe wa Kamati ya Kitaaluma ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimataifa ashinda Uanachama wa Muungano wa Kimataifa wa Wanahabari wa Uchunguzi

Mjumbe wa Kamati ya Kitaaluma ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimataifa ashinda Uanachama wa Muungano wa Kimataifa wa Wanahabari wa Uchunguzi

Imefasiriwa na / Alaa Zaki

Muungano wa Kimataifa wa Wanahabari wa Uchunguzi (ICIJ) ulitangaza kuchaguliwa kwa mwandishi wa habari na mkufunzi wa kimataifa, "Mohamed Zaidan" miongoni mwa waandishi wa habari waandamizi 20 kutoka nchi 18 ulimwenguni waliochaguliwa kujiunga na mtandao wa wanachama wa Muungano huo, ambapo Muungano huo unajumuisha wanachama 290 wanaowakilisha takriban nchi 150.

Mwanahabari mchanga, "Mohammed Zaidan", anajulikana kwa taaluma yake ya vyombo vya habari iliyojaa mafanikio mahiri katika uwanja wa uandishi wa habari wa uchunguzi na mafunzo ya vyombo vya habari, yaliyozidi miaka 14 ya kazi bidii, miongoni mwake, kazi yake kama mwandishi wa habari katika majukwaa na magazeti mengi ya kitaifa na ya kimataifa, na kama mshauri wa Kituo cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari. Pia alishinda tuzo nyingi za kimataifa.

Tena mnamo 2012, alishiriki kama mwanachama mwanzilishi wa idara ya uandishi wa habari wa uchunguzi katika Gazeti la Al-Watan, na ana michango mingi kwa faili nyingi za uchunguzi, miongoni mwake, kazi yake mnamo 2021 kwenye mradi wa Hati za Pandora, ambao ni mradi mkubwa zaidi wa Uandishi wa Habari  katika historia.

Katika muktadha unaohusiana, ikumbukwe kuwa mwandishi wa habari Mohamed Zaidan alishiriki katika mafunzo ya washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika "Jukumu la Uandishi wa Habari na Vyombo vya Habari katika Maeneo yenye Migogoro" ndani ya shughuli za toleo la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Juni iliyopita, mwaka wa 2022, pamoja na kauli mbiu ya "Vijana Wasiofungamana kwa upande wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini", kwa ushiriki wa viongozi vijana 150 kutoka nchi 65 Duniani kote.

Kwa upande wake, "Hassan Ghazali", Mwanzilishi na Mratibu mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, alisema kuwa Udhamini wa Nasser ulijali kuweka faili la vyombo vya habari katika fomu zake zote kwenye meza ya majadiliano miongoni mwa shughuli za Udhamini katika matoleo ya zamani, ambapo masuala mengi yalijadiliwa, ikiwa ni pamoja na "Jukumu la Vyombo vya Habari", kwa mahudhurio ya Dkt. Miral Sabry, makamu mkuu wa zamani wa Kitivo cha Uchumi na Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Mustakabali, Ahmed Esmat, mwenyekiti wa ukongamano wa Alexandria kwa Vyombo vya Habari, Mahmoud Mamlouk mwandishi wa habari na mhariri mkuu wa tovuti ya Kairo 24, na Omar Mostafa, mkurugenzi wa maendeleo ya kidijitali katika taasisi ya Al-Fanar. Mbali na kikao kilichoitwa "Maadili na Kanuni za Vyombo vya Habari na Athari zake za Kimataifa", kwa mahudhurio ya Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Ahmed Jalal, mwandishi wa habari na mwandishi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Akhbar Al-Youm, Ali Hassan, Mwenyekiti na Mhariri Mkuu wa Shirika la Habari la Mashariki ya Kati, Iyad Abu Al-Hajjaj, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi hiyo Dar Al-Tahrir, na ilisimamiwa na mwandishi wa habari anayeheshimika Nashat Al-Daihi. Akisisitiza kuwa vikao hivyo, mijadala ya jopo na warsha zilitokana na imani yetu kubwa katika umuhimu wa Vyombo vya Habari kama njia ya kuhamasisha uungaji mkono katika mikakati na mipango ya maendeleo, kama sauti ya wazi kwa watu, na kama nguvu laini inayoweza kuathiri amani, utulivu na usalama, chanya na hasi, kitaifa na kimataifa.

Ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ulipata uangalifu wa Uandishi wa Habari kutoka Mamlaka ya Kitaifa ya Uandishi wa Habari miongoni mwa  maandalizi ya toleo la nne, litakalofanyika Juni ijayo pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fatah El-Sisi.