Dokta Adel El-Adawy

Dokta Adel El-Adawy

Dkt. Adel El-Adawy,  Profesa Msaidizi wa Mahusiano ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Marekani huko Kairo, naye ni mhitimu wa Mpango wa Rais wa kuwawezesha Vijana  kwa Uongozi katika toleo lake la kwanza.

Dkt. Adel El-Adawy anapata shahada ya Uzamivu kutoka Idara ya Mafunzo ya Vita, Chuo cha King's London,na pia alipata shahada ya Uzamili katika sayansi za siasa kutoka Chuo Kikuu cha Marekani huko mjimkuu, Washington.

Hapo awali, Dkt. Adel El-Adawy alishikia wadhifa wa Mkurugenzi Mtendaji kwa Kongamano la Kimataifa la Uchumi la Misri, Pia alikuwa Mwanafunzi wa Kitivo cha Chama cha NATO huko Roma, aliposoma ushirikiano wa kiutendaji na kisiasa kati ya Misri na NATO katika uwanja wa Mediterania.

Pia, Al-Adawy alishikilia kazi nyingi za juu katika taasisi maarufu ya fikra kama Taasisi ya Washington ya Sera ya Mashariki ya Karibu,na Mradi wa Usalama wa Marekani, na Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa, na Taasisi ya Mashariki ya Kati, na Kituo cha Tafiti cha Kimataifa huko Kairo.

Tafiti na machapisho ya Dkt. Adel El-Adawy yalilenga haswa mahusiano ya kiraia na kijeshi katika Ulimwengu wa kiarabu, na Usalama wa kitaifa, na masuala ya Geopolitics katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, na sera ya kigeni ya Misri kwa karne ya ishirini na moja.