Kampeni ya Vijana 75 wa Kiarabu kutambulisha Udhamini wa Nasser kwa Uongozi kwa maandalizi ya toleo la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Idadi ya wahitimu wa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walifanya kampeni ya
utangulizi, kwa ushiriki wa zaidi ya vijana wa kiume na wa kike 75 kutoka nchi mbalimbali za Kiarabu kupitia Fomu ya Zoom na ushiriki wa wasemaji kutoka
Misri Tunisia, Chad na Sudan.
Alzubaer Alburaki kutoka Libya msimamizi wa kikao na mjumbe wa timu ya vyombo vya habari vya kimataifa na Udhamini huo
alifungua mazungumzo kwa kuwakaribisha waliohudhuria na kutoa utangulizi wa aina ya Udhamini na kuwatambulisha wazungumzaji, tena alianza maneno yake akieleza zaidi kuhusu Udhamini na Historia yake akisema: Udhamini wa Nasser unazingatiwa mmoja wapo Udhamini muhimu zaidi unaoandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais wa Misri
Abdel Fattah El-Sisi.
Kutoka Misri Mahmoud Labib alisema kuwa Udhamini huo ni kiongozi wa kweli mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko
katika nchi yake na jamii kwa kujichanganya na watoa maamuzi hapa Misri katika nyanja mbalimbali
kufanya mazungumzo nao na kuwasilisha uzoefu wao wenyewe ambao ulichangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha
Uongozi wa washiriki na haukuishia kwenye vikao vya kitaaluma tu.
Sawakien Babker kutoka Sudan alimshukuru Dkt.Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri ambaye aliunga mkono Udhamini huo na ambaye alikuwepo kila wakati na karibu na washiriki
Pia alizungumzia uzoefu wake binafsi katika ufadhili huo na jinsi alivyofanikisha malengo yake Kushiriki na kutoa ushauri kwa waombaji wapya
Katika toleo lake la tatu, na Udhamini huo unalenga kuangazia jukumu la vijana wasiofungamana kwa upande wowote katika kukuza ushirikiano wa Kusini kwa kuzingatia ulimwengu unaobadilika haraka na jinsi ya kukuza ushirikiano huu kupitia vijana kama utaratibu mzuri na endelevu kwa kuzingatia jukumu la wanawake, kwa hivyo, kauli mbiu ya Udhamini wa mwaka huu ni Ushirikiano wa Kusini-Kusini na Vijana Wasiofungamana kwa upande wowote.
Iliamuliwa kuwa Udhamini huo kwa Uongozi wa Kimataifa utafanyika tarehe 28 Mei ijayo, na itadumu kwa siku 15.