Siku ya Michezo ndani ya Uwanja wa Kimataifa wa Kairo kwa washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi
Imetafsiriwa na: Habiba El-Sayed
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Wizara ya Vijana na Michezo iliandaa siku ya michezo katika Uwanja wa Kairo kwa wajumbe wa vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, kama sehemu ya shughuli za siku ya kumi na nne ya Udhamini, ambapo siku hiyo ilijumuisha mazoezi ya shughuli nyingi za michezo na burudani, kuanzia mazoezi ya mazoezi ya mwili hadi mpira wa miguu na michezo na shughuli mbalimbali, hii ilikuja na ushiriki wa Hassan Ghazaly, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa.
Kwa upande wake, Ghazaly alisema kuwa mazoezi ya michezo ni haki ya binadamu na haki ya raia, hivyo tahadhari ilichukuliwa kuandaa siku hii ya michezo ndani ya shughuli za kundi la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, akibainisha kuwa Udhamini huo unalenga kufundisha, kuhitimu na kuongeza jukumu la vijana, na inakuja ndani ya mfumo wa maslahi katika kuwasilisha uzoefu wa maendeleo ya Misri katika kujenga taasisi na utu wa kitaifa kama mfano wa kuigwa, na ndani ya mfumo wa ushirikiano wenye matunda kati ya taasisi za kitaifa na jitihada za Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ili kuongeza jukumu la vijana duniani kote kwa kutoa aina zote za msaada, ukarabati na mafunzo.
Ni vyema kutajwa kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unalenga kuhamisha uzoefu wa zamani wa Misri katika kujenga taasisi za kitaifa, pamoja na kufanya kazi ili kuunda kizazi cha viongozi wa vijana kutoka nchi zisizofungamana na Upande wowote zenye maono kulingana na ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza ufahamu wa jukumu la Harakati ya kutofungamana na upande wowote.