Ofisi ya Vijana ya Afrika ni mshiriki wa udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu

Ofisi ya Vijana ya Afrika ni mshiriki wa udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu

Ofisi ya Vijana ya Afrika inazingatiwa sehemu ya taasisi halisi kubwa yenye uzoefu na michango mikubwa katika kuimarisha jukumu la vijana katika ngazi za kitaifa, kikanda na kimataifa, na mshiriki mwendelezaji wa Misri – pamoja na taasisi za serikali za kitaifa - katika kukuza mahusiano ya ushirikiano na urafiki kati ya Misri na nchi nyingine, haswa nchi za bara la Afrika. 

Mnamo 2011,Ofisi ya Vijana ya Afrika ilianzishwa kama mpango huru wa vijana ikifanya kazi pekee , na baada ya mapinduzi ya Juni 30, 2013, mwanzilishi wa mradi huo, Hassan Ghazaly, ametoa ombi kwa Wizara ya Vijana na Michezo ili taasisi za serikali ziweze kukumbatia na kuzingatia vijana wake ndani ya Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri katika wakati muhimu sana nao ni Februari 2014, kwa lengo la kuboresha mahusiano ya Afrika kupitia Vijana, kwa kuunda ushirikiano na kutekeleza mipango husika ya Bara na taasisi za kitaifa zinazohusika na vijana na Umoja wa Afrika, ili kuweka thabiti maadili ya kiafrika ambayo yalianzishwa na Baba Waanzilishi wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika mwaka 1960, nazo zilizopitishwa na Ajenda ya Afrika 2063.  Ofisi hiyo iliidhinishwa kuwa kituo kikuu mnamo Julai 2014 na Tume ya Umoja wa Afrika ya Rasilimali Watu, Sayansi na Teknolojia.

Ofisi hiyo inafanya kazi ya kuwawezesha vijana waafrika ndani na nje ya Misri katika ngazi zote kupitia ukuzaji wa dhana za kiafrika ambazo Umoja wa Afrika ulianzishwa ukizitegemea kupitia programu za kubadilishana ujuzi na kuunda uwezo, ili wawe kama nguvu ya ushawishi katika eneo la kimataifa, pia tufanye  karibu na Afrika tunayoitaka, kwa kuzingatia maoni ya Misri ya 2030, kuhusu ngazi ya kitaifa, Ajenda ya Afrika 2063 Barani, na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 katika ngazi ya kimataifa.