Maadhimisho ya Miaka 45 ya Uhuru wa Jamhuri ya Msumbiji

Imefasiriwa na/ Radwa Ahmed
Imeharirwa na/ Mervat Sakr
Msumbiji iliteswa na Ukoloni wa Kireno ulioendelea kwa muda wa karne nne na nusu, Ureno ilipochukua udhibiti wa nchi mwanzoni mwa karne ya 16, na kuanzisha uwepo mkubwa kwenye eneo lililodhibiti eneo hilo kwa ufanisi. Mwaka 1962 makundi kadhaa ya kupinga ukoloni yaliungana kuunda kundi la Ukombozi wa Msumbiji (Frelimo). Mnamo Septemba 1964, walianza kampeni ya vita vya msituni dhidi ya Wareno. Mgogoro huu uliendelea kwa karibu miaka kumi, hadi Frelimo ilipotawala Maputo, mji mkuu wa Msumbiji, Aprili 1974, na Msumbiji ikajitangazia uhuru wake Juni 25, 1975.
Misri ilikuwa na mchango mkubwa katika Uhuru wa Msumbiji, wakati Misri ilipokuwa mwenyeji wakati wa enzi za hayati Rais Gamal Abdel Nasser, Harakati kadhaa za Ukombozi wa Msumbiji baadaye zilizoungana Tanzania kuunda Harakati za Ukombozi wa Msumbiji zilizojulikana kama Ferlimo, na kuwa mwenyeji wa makada wa Harakati hizo baada ya kuundwa kwake na kuwapa msaada muhimu wa kisiasa na kiufundi ili kuwaandaa kwa mapambano ya Uhuru, na kwenye kipindi cha Vita vya Ukombozi, Misri ilitoa Harakati hizo kwa silaha na mafunzo.
Misri ilikuwa mojawapo ya nchi za kwanza kutambua Jamhuri ya Msumbiji baada ya Uhuru wake mwaka 1975, na kufungua ubalozi wake mjini Maputo, mji mkuu, Septemba mwaka huo huo kama ubalozi wa sita kufunguliwa nchini na ubalozi wa kwanza wa Kiarabu.
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy