Radio ya Vijana ya Afrika: Matokeo mengine ya Matunda kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi

Imetafsiriwa na: Nourhan Mohamed
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr
Redio ya Vijana ya Afrika ilianzishwa ndani ya muktadha wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi, uliofanyika Misri mnamo tarehe Juni 2019, wakati ambapo washiriki walitembelea Jiji la Uzalishaji wa Vyombo vya Habari na kujifunza kuhusu majukwaa tofauti ya vyombo vya habari na jukumu la vyombo vya habari kwa ujumla katika kufikia idadi kubwa ya watu.
Wakati wa mojawapo ya vikao vya mwingiliano, timu ya viongozi wa vijana kutoka Afrika nzima ilitambua haja ya kuendeleza njia ya mawasiliano ambayo inaunganisha vijana wa Kiafrika na kuwawezesha kushiriki habari na kuwasiliana kwa uhuru, na hivyo kujiwezesha.
Baada ya wahitimu wa Udhamini wa Nasser kutambua thamani ya vijana kama utajiri kwa Afrika, waliamua kuweka hiyo katika vitendo: walishirikiana kuunda mabadiliko mazuri na kufanya kazi ili kuendeleza zaidi jamii zetu, mataifa, bara la Afrika na ulimwengu kwa ujumla.
Waliunda jukwaa la Redio ya Vijana wa Afrika ili kushiriki fursa maalum kwa vijana wa Kiafrika, kama vile mikutano, masomo, mashindano, mipango ya mafunzo ya ushauri.
Radio ya Vijana Afrika pia inalenga kushiriki hadithi za viongozi vijana ambao hufanya tofauti katika jamii tofauti ili kuwatangaza ili hadithi zao za mafanikio zihamasishe vijana wengine na kuhamasisha vijana wa Kiafrika kushiriki katika kujenga nafasi ambapo wanaweza kushiriki uzoefu wao, habari na mawazo.
Kauli mbiu ya Redio ya Vijana ya Afrika ni "Mawasiliano, Elimu na Uwezeshaji", sambamba na mpango wa Umoja wa Afrika "Milioni Moja ifikapo mwaka 2021", akibainisha kuwa nguzo zake kuu ni: ushiriki, elimu, ajira na ujasiriamali.
Waanzilishi wa Redio ya Vijana ya Afrika ni wahitimu wa Udhamini wa Nasser kutoka Uganda, Rwanda, Kenya, Kamerun, Gambia na Zimbabwe.
Katika video hii, Bw. Tugum Shafik Rojmir (kutoka Uganda), Mhitimu wa Udhamini wa Nasser na Mwanzilishi mwenza wa redio, anaelezea maono, dhamira na malengo ya mpango huu. Inatoa wito kwa vijana wa Afrika kushiriki katika kuunda nafasi salama na kwa vijana ili waweze kushiriki kwa uhuru habari, maarifa na mawazo yao.