Kumbukumbu ya kuzaliwa kwa daraja la uandishi wa habari wa fasihi .. Mohamed Hassanein Heikal

Kumbukumbu ya kuzaliwa kwa daraja la uandishi wa habari wa fasihi .. Mohamed Hassanein Heikal

Mwandishi mkongwe na mchambuzi wa kisiasa, ambaye alivyoelezwa kama mwanahistoria wa Historia ya Kisasa ya Misri, alielezwa na gazeti maarufu la Marekani “New York Times” likimsifu kama mkuu wa Wachambuzi wa Kisiasa waarabu, lakini yeye alijiona mwenyewe kama mwandishi wa habari katika nafasi ya kwanza, au kama alivyosema kuhusu nafsi yake, “Mtu aliruka katika upeo na aliendelea majaribio ya zamani na zama yake na aliona wazi Mipango na miradi imejitokeza, malimwengu yanaundwa, matukio yaliyoshuhudiwa katika vita na siasa, enzi za Dola na Ukombozi, mapinduzi na mabadiliko, maendeleo na kurudi nyuma yanapiganwa vikali kwa ukubwa wa nchi, kanda na ulimwengu”.

Heikal alikuwa msiri wa Hayati Rais Gamal Abdel Nasser, na vitabu vyake ni miongoni mwa marejeo muhimu sana ambayo yanarejelewa katika masuala ya kikanda na kimataifa kwa sababu ya nguvu zao kama nyaraka zinazoungwa mkono na taarifa na ushahidi wa watoa maamuzi, wafalme na wanadiplomasia, yeye aliandika vitabu 40 ambaye alieleza matukio ya kihistoria ambapo aliishi wakati wake, miongoni mwake; “Abdel Nasser: Hati za Kairo”, “Barabara Kuelekea Ramadhani” na kitabu “Sphink na Comyser” na kitabu cha “Hadithi ya Suez” Mwaka wa 1977, “Vuli ya hasira” Mwaka wa 1984, na kitabu chake “vita vya miaka 30” kimetolewa mnamo mwaka wa 1986, kitabu cha “mazungumzo katika dhoruba” Mwaka wa 1987, pamoja na kitabu cha “vita vya ghuba .. fantasia za nguvu na ushindi” mnamo Mwaka wa 1992, na mnamo Mwaka wa 1998 kimetolewa kitabu cha “viti vya ufalme na majeshi” ambapo mwandishi mashuhuri Mohammed Hassanein Heikal aliandika Mgongano wa Waarabu-Israeli tangu Mwaka wa 1948 hadi Mwaka wa 1998.

Pia alianzisha vituo kadhaa maalum, ikiwa ni pamoja na kituo cha kuorodha historia ya kisasa ya Misri, kituo cha tafiti za uandishi wa habari, Kituo cha Al – Ahram cha tafiti za kisiasa na kimkakati, pamoja na usimamizi wake wa gazeti la Al-Ahram hadi lilipogeuka kuwa taasisi, Heikal pia alikuwa mwanachama wa Kamati kuu ya Muungano wa Kisoshalisti wa kiarabu (1968 - 1974), na Waziri wa Vyombo vya Habari mnamo 1970.

Heikal alizaliwa mnamo Septemba 23, 1923, kijijini mwa “Pasos” katika mkoa wa Al-Qalubeiah, na alikamilisha masomo yake mjini Kairo, kisha akaanza maisha yake ya kazi katika “Egyptian Gazeti ” mnamo 1942, kama mhariri chini ya idara ya mafunzo katika sehemu ya ajali, kisha alihamia sehemu ya kiujerumani, na katika  1944 alijiunga na gazeti la Rosa El Youssef, kama mwandishi wa habari wa kijeshi hadi 1947 alihamia gazeti la  Akhbar Al Youm, na katika 1952, alifanya kazi kama Mhariri mkuu wa gazeti la Akher Saa, na katika  1957 alichukua uenyekiti wa uhariri wa Gazeti Al-Ahram na amebakia katika cheo chake hadi Mwaka wa 1974.

Profesa “Mohammed Hassanein Heikal” ameweka vizazi vya taaluma ya uandishi wa habari-sasa na baadaye- kwa kuzingatia wajibu ambao una athari kubwa kwa nchi zao na Jamii zao za kiarabu katika nyakati za mabadiliko ambazo huathiri watu wote, alianzisha “Taasisi ya Mohammed Hassanein Heikal kwa Ajili ya Uandishi wa habari wa Kiarabu” mnamo  2007, kwa lengo la kuchangia kwa ufanisi katika kuimarisha na kuendeleza uzoefu wa wataalamu wa uandishi wa habari katika majukwaa mbalimbali, na kuwajulisha kwa maendeleo ya hivi karibuni katika vyombo vya habari vya kimataifa, pamoja na kuzingatia haswa  vizazi vijana wa waandishi wa habari, na hivi karibuni taasisi ilizindua  tuzo mbili za “Mohammed Hassanein Heikal” kwa ajili ya kazi ya uandishi wa habari katika nyanja zote, na tuzo ni (medali ya Kumbukumbu na kiasi cha pesa cha Paundi 250,000), mshindi hutangazwa na kukabidhiwa tuzo katika sherehe ya kila Mwaka Katika siku ya ishirini na tatu ya Septemba katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

Tuzo hizo zinategemea maoni ya Profesa “Heikal” kwamba taarifa ya uandishi wa habari ni mwingiliano na hatua ya kuanzia, na uchambuzi wa kina ni jukwaa ambalo jamii zinaangalia kile kinachokuja kwa uangalifu na kuelewa, kuhamasisha vipaji vya habari vya vijana na kwa tuzo kuwa msaada kwa mshindi katika kuendeleza zana na ujuzi wake, na kukamilisha kile ambacho taaluma ya kale inahitaji kuweka juu na kile kipya katika ulimwengu unaobadilika.

Heikal amefariki Dunia  mnamo mwezi wa Februari Mwaka wa 2016 akiwa na umri wa miaka tisini na tatu, amekaa miaka sabini akiwa ni mwandishi, mwanahabari na mchambuzi wa siasa, akiliandika jina lake kwa herufi za dhahabu ambazo bado zinaelimisha akili za wasomaji wake, akiwafahamisha matukio ya zamani, kurasa za historia, na kuwahamasisha siku zijazo zenye matarajio.