Ni wajibu wenu, enyi Vijana wa Syria kufahamiana na Vijana wa Misri
Imefasiriwa na / Ali Mahmoud
Ni fursa ninayofurahia sana; fursa ya kukutana na vijana wa Syria, ambao ninawaona kuwa mlinzi wa uongozi na sababu kuu ya kufikia malengo ya Kiarabu.
Vijana hawa wa Syria, wenye hisia nyingi, tena hisia kali, wanaoamini katika malengo makubwa ya nchi yake, ndio wanaobeba mzigo wa utetezi ili kufikia malengo hayo, ambayo yamejikita katika kujenga Taifa la Kiarabu lenye nguvu na mshikamano, linalofanya kazi bila ya maeneo bure, linalohisi hatari na kufanya kazi kujitetea, na halituliwi isipokuwa hatari ziondolewe kabisa humo, na haliwaruhusu kulikaribia.
Sote tunahisi kuwa tunahangaika kufikia malengo hayo, nami ninafurahi kuona kundi la vijana wa Syria ambao wako macho na walio na wasiwasi, na wanaohisi hatari inayowasukuma. Ninafurahi kuona vijana wa Syria wakitembelea Misri; kuwasiliana na vijana wa Misri na kufanya kazi kuimarisha mahusiano yao nao.
Kulikuwa na kipindi ambacho kila mmoja alijishughulikia haki yake binafsi, na kumwacha mwenzake akutane na kile anachokutana nacho, na kulikuwa na hatari tangu muda mrefu ambayo inafanya kazi kutenganisha mwungamano huo.
Ninaona kupitia kubadilishana ziara hizi kati ya vijana ni sababu kubwa zaidi katika kuunganisha mwungamano na kuunga mkono neno la Waarabu, na natumai kuwa ziara hizi ziongezeke katika siku zijazo. Na kama tunaona leo vijana 800 wa Misri katika Damascus, tunatarajia kuwa mwaka ujao idadi hii ifikiee vijana 1600, na iongezeke maradufu mnamo miaka ijayo.
Ni wajibu wenu, enyi vijana wa Syria, kufahamiana na vijana wa Misri, na kufanya kazi nao kutimiza jukumu lenu kuu; tunaishi katika ulimwengu uliojaa uroho na upendo wa udhibiti, na nyinyi - Vijana- mnatarajia kufanya kazi kufikia malengo makubwa ya taifa lenu.
Mwenyezi Mungu aijaalie Syria mafanikio, na aijaalie nguvu, kiburi na utukufu, ikishirikiana na nchi zake ndugu za kiarabu.
ــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــــ
Hotuba ya Rais Gamal Abdel Nasser katika Ujumbe wa Shule ya Sekondari huko Latakia, Syria
Kwa tarehe ya Februari 24, 1956.