Baraza la Mambo ya Nje la Misri

Baraza la Mambo ya Nje la Misri

 Imefasiriwa na / Ali Mahmoud

Misri daima imekuwa na sera ya kigeni ambayo kwayo inaingiliana na mazingira yake ya kikanda na Dunia, mnamo miongo saba iliyopita, duru za harakati zimepanuka mbele ya sera ya nje ya Misri, na majukumu yake katika masuala ya kikanda na kimataifa yameongezeka.
 
Mazingira ya kikanda na kimataifa yalishuhudia mabadiliko makubwa katika asili ya mifumo ya kikanda na kimataifa na mahusiano ya nguvu, mabadiliko ya mfumo wa uchumi wa kimataifa, vipimo vilivyochukuliwa na mapinduzi ya habari na mawasiliano, pamoja na jukumu la sababu ya kitamaduni katika mahusiano ya kimataifa.
 
Hayo yote yalikuwa na matokeo kwenye sera ya nje ya Misri, na yaliiongezea mizigo mipya, iwe katika kiwango cha utambuzi na uchambuzi au katika kiwango cha mazoezi, ili moja ya malengo ya sera hii iwe kuunda mazingira mazuri ya kikanda na ya kimataifa, ili kufikia na kutoa mahitaji ya ujenzi mpya wa ndani, na kuongeza kasi ya mafanikio ya kiuchumi na kijamii.
 
Kwa hivyo, ilikuwa ni lazima kuanzisha jukwaa la Misri linalowakilisha ufahamu wa jumuiya ya kiraia ya Misri kuhusu mabadiliko haya, na kuchangia uzoefu wake katika kujadili masuala yake, na kuimarisha ufahamu wa maoni ya umma juu yake. Kwa hivyo, kundi la wale wanaopenda sera ya kigeni waliungana kwenye malengo haya, na wazo la kuanzisha baraza hilo lilikuja mnamo mwaka wa 1999.
 
Ujumbe wa Baraza
 
Dira ya Baraza la Masuala ya nje la Misri ni kuwa jukwaa huru na lisilo na upendeleo la kuelewa vyema sera ya nje ya Misri. Katika muktadha huo, ujumbe wa baraza hilo unafumbatwa katika kufanya kazi ili kufikia uelewa wa maudhui na wa kina wa masuala yote ya kigeni katika ngazi mbili za kikanda na kimataifa, kwa ajili ya kuhudumia maslahi ya kimkakati, kiuchumi na kisiasa ya kitaifa ya Misri. Katika suala hili, baraza linategemea mawazo na utaalamu wa wajumbe wake, kutoka kwa wenye taaluma, uzoefu tofauti, na mawasiliano na masuala ya umma, na kwa wale wanaowaalika kushiriki katika majadiliano ya masuala maalum kutoka kwa watu wa umma na wataalam maalumu kutoka kwa wamisri na wageni, ili kuimarisha majadiliano na kuuleta kwa manufaa na lengo yanayohitajika.
 
Malengo ya Baraza
 
Kulingana na dira ya Baraza na dhamira yake, Baraza la Mambo ya Nje la Misri linalenga:

1- Kuongeza na kuimarisha mjadala wa umma nchini Misri kuhusu masuala ya nje na matatizo yanayohusiana nayo, haswa yale mapya, na kutoa mwanga juu ya uhusiano wa masuala hayo na maslahi ya juu ya Misri  na usalama wake wa taifa kuathiri na kuathiriwa.

Lengo hilo limeonekana wazi katika shughuli mbalimbali za Baraza, na katika makongamano, semina, meza za duara na mikutano mikuu inayofanywa kwa wanachama wake, na katika makundi maalumu yanayojali masuala yanayojadiliwa, yanashughulikia, kwa mfano: migogoro ya Mashariki ya Kati, hali ya ugaidi, au mustakabali wa mchakato wa Amani katika Mashariki ya Kati, na mahusiano ya Misri na mataifa ya nje, kama vile uhusiano na Marekani, Ulaya, Urusi, Uchina, Afrika na Marekani ya Kusini. Mikutano hii, kwa kawaida, hutokeza seti ya karatasi za kazi na taarifa ambazo zinabeba mtazamo wa baraza juu ya kile kilichojadiliwa, karatasi hizi pia hushughulikia masuala mbalimbali kama maendeleo katika kanda, kama vile mgogoro wa Syria, na hali za Libya na Yemen. Mbali na masuala mengine yenye umuhimu maalumu kwa usalama wa taifa wa Misri, kama vile:

kupambana na ugaidi, suala la maji, uchumi wa nishati, na mengine. Baraza, kwa kawaida, huwakaribisha watu wanaohusika na masuala ya kuangaziwa na kuchambuliwa, au kubadilishana mitazamo juu yao.
 
2- Kuanzisha jukwaa huru la kukuza sera za kigeni na kidiplomasia.

Baraza linahangaika kutoa jukwaa huru na lisiloegemea upande wowote linaloruhusu mielekeo yote ya kisiasa na kiakili nchini Misri kutoa maoni na mawazo yao kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa, kuchangia kuunga mkono sera ya nje na diplomasia ya Misri, na kuweka msingi wa makubaliano ya kitaifa kuhusu mistari yake mikuu.
 
3 – Kuanzisha madaraja ya mawasiliano na mahusiano ya pamoja na vituo vingi vya utafiti na mawazo ya kisiasa na ya kimkakati katika nchi mbalimbali za Dunia.
 
Baraza hupanga mikutano na vituo hivyo kwa ajili ya kufanya mazungumzo navyo kuhusu masuala yanayowahusu wote, na kuunda mawazo kuhusu matatizo yaliyoibuliwa. Mikutano hii, kwa kawaida, hufanyika kwa zamu kati ya Misri na nchi ambamo kituo cha utafiti ni mshirika wa msingi wa baraza hilo. Mikutano na hafla hizi hufanyika kila mwaka, mara kwa mara. Idadi ya washirika wa baraza kutoka halmashauri na vituo vinavyofanana imefikia halmashauri na vituo vipatavyo (32); Ikiwa ni pamoja na baadhi ya vituo vya Misri; Kama vile Kituo cha Kikanda cha Mafunzo ya Kimkakati huko Kairo, Kituo cha Al-Ahram cha Mafunzo ya Kisiasa na Kimkakati, Baraza la Misri la Masuala ya Kiuchumi, na Shirika la Ushirikiano la Misri kwa ajili ya Maendeleo. Na vituo vingine vya kigeni kama vile Taasisi ya Watu wa China ya mahusiano ya Kimataifa, Taasisi ya Moscow ya Mahusiano ya Kimataifa, Baraza la Urusi la Mambo ya Nje, Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa cha Morocco, Taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa ya India, Jukwaa la Mawazo la Waarabu. Oman, Taasisi ya Mambo ya Nje ya Hungaria, Baraza la Sudan la Mambo ya Nje, na Taasisi ya Mahusiano ya Nje na Masomo ya Kimkakati ya Ethiopia. 

4-  Kuzingatia kuunganisha kati ya sera za nje na mahitaji ya kusaidia uchumi wa Misri.

Baraza linajaribu kuunganisha sera za nje na mahitaji ya kusaidia uchumi wa Misri; haswa kuhusu kuvutia uwekezaji wa kigeni nchini Misri, na kufungua masoko kwa bidhaa na huduma za Misri. Hili lilifanywa kupitia mikutano na wajumbe waliotembelea Misri na maafisa wanaohusika na masuala ya uchumi.
 
5 – Kufikia eneo pana zaidi la maoni ya umma.
 
Baraza linataka kupanua ufikiaji wake kwa maoni ya umma kupitia tafiti na makala zilizochapishwa katika magazeti ya Misri na idadi kubwa ya wajumbe wa Baraza, ikiwa ni pamoja na waandishi, wanafikra, na wanadiplomasia wa zamani; Wale wanaopewa nafasi katika magazeti ya kila siku, majarida na mahojiano ya televisheni mara kwa mara, pamoja na kunufaika na ushiriki wao katika semina zinazofanywa na mashirika mbalimbali ya jumuiya ya kiraia, na semina za kila mwaka zinazofanyika katika Maonesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Kairo.
 
Vikundi vya Kazi:
 
Kikundi cha Kazi cha Sudan (Sudan Kusini) na Ethiopia.
 
Kikundi cha Kazi cha Kupambana na Ugaidi.
 
Kikundi cha Kazi cha Wataalam wa Sheria ya Kimataifa.
 
Kamati za Kudumu
 
Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Kiarabu.
 
Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Marekani Kaskazini.
 
Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Marekani ya Kati, Karibea na Marekani ya Kusini.
 
Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Ulaya.
 
Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Afrika.
 
Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Asia.

Kamati ya Kudumu ya Rasilimali za Maji na Mabadiliko ya Hali ya Hewa.
 
Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
 
Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Jamii.
 
Kamati ya Kudumu ya Utamaduni na Nguvu laini.
 
Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Uchumi (ikijumuisha masuala ya Biashara, Usafiri, Nishani na Mazingira).
 
Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Uhamiaji na Wamisri nje ya Nchi.
 
Baraza hutegemea uwasilishaji wa shughuli zake kwa kutoa jarida la mara kwa mara ambalo linajumuisha utangulizi wa shughuli za Baraza na uwasilishaji wa matokeo ya kazi yake na shughuli zake, mikutano na majadiliano katika kipindi ambacho jarida la mara kwa mara lilitolewa mwishoni mwake. Pia zinatolewa taarifa za makongamano yanayoandaliwa nje ya nchi na zingine kuhusu semina zinazoandaliwa nchini Misri, pamoja na Machapisho ya Baraza hilo kuhusu masuala mbalimbali. Maandalizi yanaendelea kutoa jarida kwa Kiarabu na lugha za kigeni ambazo zinaonesha zaidi msukumo wa Misri katika mambo ya nje na inatoa fursa kwa waandishi wasio wamisri kuwasilisha maono yao na mtazamo wao pamoja na waandishi wa Misri kuhusu matatizo ya kimataifa na kikanda.

 
Vyanzo:
 
Tovuti ya Baraza la Mambo ya Nje la Misri.