Misri yaiunga mkono Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuhusu waathirika wa ajali ya treni ya Koloise

Misri yaiunga mkono Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuhusu waathirika wa ajali ya treni ya Koloise

Imetafsiriwa na: Tarek Said 
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Misri imetoa rambirambi zake za dhati kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia ajali ya treni iliyotokea katika eneo la kusini mashariki la Koloizi, ambalo lilisababisha vifo vya watu kadhaa na majeruhi.

Serikali na watu wa Misri wanatoa pole zao za dhati kwa serikali na watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na familia za wahanga, wakitakia kupona haraka kwa wale wote waliojeruhiwa na kusisitiza msaada wao kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kipindi hiki kigumu.