Mhadhara wenye kichwa: Jukumu la Wanafunzi katika Awamu ya Mpito nchini Chad na Maandalizi ya Majadiliano ya Kitaifa Jumuishi

Imetafsiriwa na: Salma Ehab Zakaria
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr 

Harakati ya Nasser kwa Vijana, Tawi la Chad, kwa kushirikiana na Umoja Mkuu wa Wanafunzi wa Chad katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, waliandaa mkutano wa kifkra kuhusu "Jukumu la Wanafunzi katika Awamu ya Mpito nchini Chad na Maandalizi ya Majadiliano ya Kitaifa ya Kina", mnamo tarehe Ijumaa, 17/6/2022, katika Nyumba ya Umoja huko Kairo.

Wakati wa mkutano huo, Mhandisi Mohamed Haroun Adam, Mhitimu wa kundi la pili la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na Mwakilishi wa Nchi ya Chad katika Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Afrika, na Mhandisi Mohamed Salam Mustafa, Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kundi la tatu, alizungumza kwa Uwepo wa kundi la wanafunzi wa Chad na watafiti katika Jamhuri ya Misri.