Msikiti wa Al-Sahaba mjini Sharm El-Sheikh.. alama ya kipekee katika sanaa ya Usanifu wa kisasa wa kiislamu
Katika eneo la mita za mraba karibu elfu tatu katikati ya eneo la Soko la kale la Sharm el-Sheikh, “Mji wa Amani” ya mkoa wa Sinai Kusini, Msikiti wa Al-Sahaba uko katika usanii wa kipekee wa ujenzi unaochanganya ukale, utukufu na historia, ukipandwa na pwani ya Bahari ya Shamu na nyuma yake mlima, kama ni moja ya hadithi ya kale ya " Alf Lelah W Lelah", unazingatiwa kama "Alama ya kipekee" katika usanifu wa kisasa wa Kiislamu, ambapo idadi kubwa ya watalii kutoka kwa mataifa mbalimbali wanakuja kuuliza maswali yaliyopo akili zao kuhusu Uislamu, basi Msikiti huo una jukumu muhimu katika kurekebisha mawazo potofu katika dini ya kiislamu, na kubadilisha picha iliyopo kwenye baadhi ya raia kuhusu Uislamu, na kumtuliza kila mtu anayetembelea Misri.
Ujenzi wa msikiti huchanganyika mitindo mbalimbali ya usanifu, ambayo kwa mara ya kwanza kuonekana yenye utata, lakini ndani ya hilo ni falsafa ya kisanii ambapo wale ambao kupitishwa fomu waliiamini na, kutoka Enzi ya Ottoman, zilitokea kuba za msikiti zenye rangi ya shaba zilizokaribia na msikiti wa Muhammad Ali katika ngome yenye jina lake jijini Kairo. Alama ya enzi ya Wamamluki yaonekana katika “mudara” ambao huonekana ukipiga juu ya mnara wa Msikiti wa Al-Sahaba, pamoja na utumizi wa rangi ya dhahabu milangoni, haikuwa bila ya mguso wa mwanzo wa karne iliyopita, uliodhihirika katika kutaja moja ya vijia ndani ya msikiti huo kama "Kichochoro cha Masahaba", katika kuiga-kama inavyoonekana- kwa eneo"Kichochoro cha Midaq" lililo karibu na mtaa wa Al-Hussein kwenye la Kairo ya Fatimia.
Msikiti wa Al-Sahaba uko kwenye eneo la mita elfu tatu na tatu, na unajumuisha minara miwili urefu wa kila mnara miongoni mwao ni mita 76, na idadi kubwa ya kuba, na wakati wa giza linapoingia tu, na kandokando ya msikiti kuna idadi kubwa ya "Taa" kwa mwangaza iliyotengenezwa kwa ufinyanzi, nuru yake inapelekwa kwa majina mengi ya Masahaba wa Mtume Muhammad (S.A.W), ambapo kona za msikiti zimepambwa kwa majina yao ya kwanza, yakiongozwa na Abu Bakr Al-Sidik, Umar ibn Al-Khattab, Uthman Ibn Affan, Ali ibn Abi Talib, Ammar Ibn Yasir, na Wengine Allah awaridhie
Msikiti huo unajumuisha waumini zaidi ya elfu tatu. Na urefu wa nave yake kuu unafikia mita 36 kwenye ukubwa wa mita 1800, na unajumuisha waumini 800 na ndani yake kuna ukumbi wenye miavuli miwili kwa kusali, vyoo vya maji 36, hii ni pamoja na majengo ya huduma na vitengo vya biashara vinavyofanya kama sadaka ya msikiti, gharama za ujenzi wake kati ya Paundi milioni 35 na Paundi milioni 40, na ilitofautiana kati ya michango ya kifedha ya moja kwa moja, na kazi ya bure kama alivyofanya mbunifu wa mpango, Msanifu-ujenzi Fouad Tawfik, mbali na michango ya serikali, pamoja na kuhakikisha kwamba Mamlaka ya Uhandisi ya vikosi vya kijeshi, kwa kutimiza kazi za mwisho hadi kupelekwa kwake na ufunguzi wake kabla ya miezi 8, na ingawa jiwe la msingi wa msikiti liliwekwa kwa msikiti mnamo tarehe kumi Mwezi wa Januari, Mwaka 2011, lakini ulifunguliwa mnamo tarehe ishirini na nne, Mwezi wa Machi Mwaka 2017, na ukawa msikiti wa Pili kwa Ukubwa Mjini Sharm El-Sheikh na moja ya vivutio vyake vya kiutalii.
Msikiti pia unajumuisha kituo cha kimataifa cha utamaduni wa kiislamu maktaba ya utamaduni ya kidini kwa lugha mbalimbali, inayojumuisha vitabu vingi na machapisho kwa lugha mbalimbali zinazofafanua utambulisho wa Dini ya Kiislamu, maelekezo, sifa na maadili ya Mtume Muhammad (S.A.W) na neema ya Uislamu. watalii wanaotembelea maktaba, na wanaruhusiwa kuvinjari na kuchukua machapisho zilizotengwa na taasisi ya Utafiti wa kiislamu inayohusiana na Al-Azhar Al-Sharif pamoja na diski-songamano kwa lugha nyingi kuhusu tafsiri ya Qurani Tukufu.
Pia ilikabidhiwa timu kwa msikiti na kituo, inajumuisha maimamu sita, nusu yao wanahusika na Da’wah kwa kiingereza, na kama yao walikuwa weledi wa Kifaransa, na wote walichaguliwa katika mashindano maalumu kujaza nafasi hiyo miongoni mwa waombaji 150 kutoka kila mahali nchini Misri.
Msikiti huo unashughulikia kwa ujumbe wake wa Da’wah na wa elimu kupitia hotuba ya Ijumaa, masomo mbalimbali ya kila wiki, semina, sherehe za kidini, ofisi za kuhifadhi Qurani Tukufu pamoja na vinara vya msemaji na vipindi vya Qurani Tukufu.
Mtalii anapoingia tu msikiti naye anaheshimu mafundisho ya dini ya kiislamu, ambapo wanawake wanafunika nywele zao, mtu yeyote kutoka kwa ujumbe unaotembelea hagusi Qurani Tukufu ila akiwa safi kabisa, nayo ni mafundisho ambayo mwongozo wa Utalii anawaambia wakati wa kuingia.