Abdel Nasser na harakati za ukombozi.. Uasi wa Mau Mau ni suala la kiafrika

Abdel Nasser na harakati za ukombozi.. Uasi wa Mau Mau ni suala la kiafrika
Abdel Nasser na harakati za ukombozi.. Uasi wa Mau Mau ni suala la kiafrika
Abdel Nasser na harakati za ukombozi.. Uasi wa Mau Mau ni suala la kiafrika
Abdel Nasser na harakati za ukombozi.. Uasi wa Mau Mau ni suala la kiafrika
Abdel Nasser na harakati za ukombozi.. Uasi wa Mau Mau ni suala la kiafrika
Abdel Nasser na harakati za ukombozi.. Uasi wa Mau Mau ni suala la kiafrika
Abdel Nasser na harakati za ukombozi.. Uasi wa Mau Mau ni suala la kiafrika
Abdel Nasser na harakati za ukombozi.. Uasi wa Mau Mau ni suala la kiafrika
Abdel Nasser na harakati za ukombozi.. Uasi wa Mau Mau ni suala la kiafrika

Ureno inazingatiwa nchi ya kwanza ya kikoloni ambayo jumbe zake za uvumbuzi zilifika pwani za Afrika magharibi, na kufungua ukurasa wa ukoloni wa kisasa Barani Afrika.

Mnamo 1488, mreno, Bartholomew Diaz, aligundua njia ya Rasi ya ElRagaa ElSaleh humo Afrika Kusini. Na baada ya muongo mmoja, mreno "Vasco da Gama" alisafiri kwa meli kuzunguka Rasi ya ElRagaa ElSaleh mnamo 1498, na alifika pwani ya Kenya. katika karne nlya 16 wareno waliweza kushika eneo la pwani, wakauvamia mji wa Mombasa mara tano na kupanua udhibiti wao huko pwani ya Afrika Mashariki, kisha wakaelekeza macho yao kuelekea Oman, ambao waliichukulia kama hasimu wao wa kibiashara Barani Asia, mfalme wa Ureno alipeleka kampeni ya jeshi la majini ikiongozwa na Alfonso De Albuquerque mnamo 1507, hadi kisiwa cha Yemen cha Socotra baharini, na mnamo mwaka wa 1508, Ureno ilifanya mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya meli za Waoman, na walivamia ngome ya Kalhat, Qurayyat, Muscat, Khorfakkan na Sohar.

Kisha Albuquerque alivamia Malngo wa kimkakati wa Hormuz, ambao hutenganisha Maji ya Ghuba ya kiarabu, Ghuba ya Oman, Bahari ya Arab na Bahari ya Hindi, na alianzisha ngome ya kwanza ya kireno katika Ghuba, na udhibiti wa wareno uliendelea kwenye pwani za waoman na pwani za Afrika Mashariki kwa zaidi ya miaka mia moja, Ambapo Waturuki walijaribu kuwafukuza wareno kutoka eneo hilo.

Mnamo mwaka wa 1558, waoman waliomba msaada wa Sinan Pasha, Mtawala wa Uturuki nchini Yemen, katika enzi ya Sultani Murad wa tatu, ambapo Sinan Pasha alituma kampeni ya jeshi la majini inayoongozwa na Bey Amir Ali Bek na akauzingira mji wa Muscat na kuingia ndani, kisha  akaandamana na kushambulia vituo vya wareno katika Afrika Mashariki, haswa mji wa Mombasa. Hata hivyo, kampeni yake ilishindwa kutokana na usaliti wa mojawapo ya makabila ya Afrika (yanayojulikana kama Bazemba), na kufikia msaada kwa wareno kupitia Mlango wa Hormuz, Ali Bey alikamatwa na kupelekwa Lisbon. Baada ya waturuki Walikaribia kukomboa pwani ya Afrika kutoka wareno.

Wareno walifikiria katika umuhimu wa kuimarisha uwepo wao wa kijeshi katika eneo hilo, na kuanzisha ngome ya kijeshi kwao mahali hapo, hivyo wakaanzisha ngome yao inayoitwa (ngome ya Yesu), iliyojengwa kwa sura ya msalaba, na lengo lilikuwa kudhibiti biashara na usafiri katika Bahari ya Hindi, na hilo ambalo lilijulikana baadaye kama ngome ya Mombasa katika mwaka wa 1593.

Hadi mwaka wa 1649 ulipofika, ili Waoman waanze hatua zao kuelekea ukombozi pamoja na uongozi wa Imamu wa Oman Nasser bin Murshid Al-yarabi, mwanzilishi wa Jimbo la Al-yaariba, aliyeweza kuunda jeshi na safu ya maji, akitumia fursa ya kushughulikia kwa Ureno katika vita vyake vya majini na Uholanzi, Uingereza na Ufaransa. Jeshi la Waoman waliweza kuvunja milango na kuingia mjini, na wakazingira ngome ya wareno, na hatimaye wakawashinda wareno na kuwafukuza kutoka Muscat, na miji mingine ya Waoman baada ya vita mfululizo ambapo alipata mafanikio makubwa ya kijeshi, hadi alipoweza kuikomboa Oman mnamo mwaka wa 1650.

Sultani wa Oman hakutosheka kuwafukuza wareno kutoka nchini tu, bali aliwafuatilia na kutuma meli zilizoshambulia kambi za wareno katika pwani za India na Afrika, tangu mwaka wa ukombozi hadi mwisho wa karne ya 17 Usultani wa Oman ulianza kuanzisha safi yake kubwa ya kijeshi majini, kutegemea safu ya kireno kwamba wao waliidhibiti na kuiboresha, wawe na uvutano mkubwa Juu ya Bahari ya Hindi, na waweze kumaliza kabisa uwepo wa wareno katika eneo, haswa kutoka Pwani ya Afrika, ambayo kwa kiasi kidogo ni karibu na pwani ya Oman.

Baada ya kuipoteza Oman, wareno walijaribu kudhibiti baadhi ya pwani za Afrika Mashariki kwa kutumia chuma na moto ili kuzuia jaribio lolote la ukombozi katika maeneo haya, lakini walikuwa na miadi na jeshi la maji la vijana la Oman, ambalo lilielekeza udhibiti wa Pwani ya Afrika.

Mnamo mwaka wa 1660, jeshi la wanamaji la Waoman ilianzisha kampeni dhidi ya wareno katika miji ya Afrika ya Faza na Bata, nchini Guinea ya Ikweta hivi sasa, na wakadhibiti pwani yote ya Afrika isipokuwa ngome ya Kristo, Mombasa na Zanzibar. Na mnamo mwaka wa 1694, watu wa Mombasa na Zanzibar waliomba msaada wa Sultani wa Oman kuwasaidia kutoka kwa wareno, ambao walifanya mauaji dhidi ya wenyeji wa eneo hilo, kwa kukandamiza harakati ya uasi iliyofanywa na gavana wa Mombasa Sultan Hassan. Imamu Wa Omanil Sultan Bin Saif al-yarabi alijibu wito na akaelekea pamoja na jeshi lake na jeshi lake la wanamaji kwenye pwani za Afrika Mashariki, na akafanikiwa katika mwaka wa 1696, kuharibu ngome za wareno zilizokuwa kwenye kisiwa cha Bemba, mojawapo ya visiwa vya Zanzibar, kisha akaenda kwenye ngome ya Mombasa, akaizunguka, kuidhibiti na kuikomboa kutoka kwa wareno na kumteua gavana wa Omani naye ni Sheikh Nasser bin Abdullah Al-Mazrouei.

Hata hivyo, Waoman walipoikomboa Mombasa na Zanzibar, kulikuwa na migogoro ya ndani kati ya viongozi katika Mombasa, na kundi la maafisa wakapinga Sheikh Nasser, na mtu mmoja aitwaye Ciss Rombe aliteuliwa kama gavana, jambo ambalo liliwezesha wareno kuirejesha tena udhibiti.

Mara tu Sultani wa Oman alipojua hili, alipeleka jeshi lake la wanamaji tena na akaizingira ngome ya Mombasa kwa zaidi ya miaka miwili, tangu mwaka wa 1696 hadi mwaka wa 1698, na aliweza kuwashinda wareno, ambao walikuwa walichoka na kuzingirwa na magonjwa, naye aliwafukuza kutoka Mombasa baada ya kujisalimisha kwao, na kuufanya mji wa Zanzibar kuwa mji mkuu wa Oman.

Utawala wa Waarabu wa Oman ulidumu kwa miongo mingi, hadi Kifo cha Sultani Said Bin Sultan katika mwaka wa 1856, ufalme uligawanywa kwa Usultani wa Oman na Usultani wa Zanzibar baada ya mzozo kati ya wanawe Majid na Thuwaini, ambao wote waliomba cheo cha Sultani, na kumteua Majid bin Said kama gavana wa Zanzibar, na alifanya Kazi kama Sultani tangu mwaka alipokufa baba yake hadi mwaka wa 1870 ambapo ni kufariki kwake, kisha kaka yake Burghash bin Said alichukua utawala hadi mwaka wa 1888.

Wakati wa utawala wa Burghash, Zanzibar ilisitawi, ambapo madaraja, barabara, majengo ya kisasa na hospitali zilijengwa, Na Mombasa ilikuwa mji maarufu chini ya utawala wa Zanzibar na ilihitaji kuongozwa na mtu anayefaa kwa hivyo, Sultani Salim bin Khalfan, Mwenyeji wake wa Oman, aliteuliwa gavana wa Mombasa mnamo mwaka wa 1884.

Salem alishikilia nafasi ya gavana katika Mombasa hadi mwaka wa 1912, ambapo alikuwa mwenyekiti wa mikutano ya hadhara ambapo hadhira huweza kutoa maoni yao na kufikiriwa naye, na kutua migogoro kati ya watu wa Mombasa, na alikuwa akisafiri mara moja kwa mwaka kwenda Zanzibar kumwambia Sultani kwa hali ya mambo na kupokea mshahara wake, na mshahara wake ulikuwa ukitegemea iwapo Sultani alifurahishwa na utendaji wake au la, na kwa ujumla, uwezo wake wa kukabiliana na hali ngumu ulikuwa moja ya sifa zilizochangia urefu wa kipindi cha utawala wake.

Kabla ya Salem kuwa gavana, alizaa mtoto wa kiume na mwanamke wa Ethiopia, alimwita Ali, na baadaye Ali akafuata hatua za baba yake ambapo baba na mtoto wote walishirikiana na Waingereza wakati wa maasi ya Mazrouei katika mwaka wa 1896, na baadyae Ali alipelekwa Chuo kikuu cha Oxford kusoma kiingereza huko.

pia gavana wa kiingereza wa Kenya “Sir Charlon Elliot” aliita idadi ya familia tajiri za kiingereza za aristocratic kuishi katika Kenya, na kuwapa majaribu ya kumiliki kile kinachojulikana kama "ardhi za juu", ambayo  zenye rutuba zaidi katika nchi, na ilikaliwa na makabila ya "Kikuyu na Wamasai" yanayojulikana kwa uwezo wao mkuu wa kupambana, na Mohamed Fayek, mkuu wa idara ya Mambo ya Afrika ya urais wa Jamhuri na Rais Gamal Abdel Nasser, anataja katika kitabu chake “Abdel Nasser na mapinduzi ya Afrika”, kwamba lengo kuu la mtawala wa kiingereza ya kwa kuwaita familia za kiingereza lilikuwa kulinda reli aliyoamua kujenga kati ya mji wa “Mombasa” kwenye pwani ya Kenya, na mji mkuu wa Uganda "Kampala" kupita mji mkuu wa Kenya "Nairobi", kisha gavana wa uingereza aliamuru kwa kufukuza makabila ya kiafrika kutoka maeneo haya, na alitangaza kuwa Kenya ikawa "Mzungu".

Fayek anaonesha picha ya kutisha ya hali ambayo uvamizi wa Uingereza ulitekeleza sera mbaya zaidi za kikoloni dhidi ya watu wa bara la Afrika, akisema: "Waafrika waliofukuzwa kutoka katika ardhi hii ya "juu" walikuwa wanakwenda kuishi katika maeneo waliyopewa kama maghala ya kibinadamu, na wale ambao hawakupata sehemu katika maeneo haya yenye msongamano mkubwa wakawa watumwa katika ardhi inayomilikiwa na wazungu, na karibu robo ya milioni kati yao ambao wanaruhusiwa kukua wanachoishi na tu badala ya kuimarisha yao na familia zao kufanya kazi katika ardhi ya wamiliki weupe, na mkataba wa kazi kwa hawa ulikuwa unaandikwa kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi miaka mitano, na ikiwa ardhi imeuzwa, mkataba wa kazi hupita kwa mmiliki mpya, na wale ambao kutoroka kutoka kwao wanaweza kukamatwa na kufungwa jela, na kwa sababu ya uwezo mkubwa wa utawala wa waajiri juu ya wafanyakazi wao alitakiwa na sheria kuwa kila mwafrika ashikilie kibali cha kazi". 

Kati ya mwisho wa vita na kuondoka kwa Ali kwenda Uingereza, Sultani wa Oman wakati huo alikabidhi Ngome ya Mombasa - Ngome ya Yesu - kwa Waingereza, huu ulikuwa mwanzo wa utawala wa pili kwenye pwani ya Afrika Mashariki, ambapo magavana wote wanaofuata usultani walianza kupata mishahara kutoka kwa Waingereza ambao sasa hivi wana maoni katika majukumu ya uongozi, na wakati wa kurudi kwa Ali, Waingereza walimpandisha cheo cha naibu gavana, kama msaidizi wa baba yake, na katika mwaka wa 1912, Mfalme George wa tano alimpa Salim bin Khalfan medali ya Mtakatifu Michael na Mtakatifu George kwa ajili ya huduma zake zilizotolewa kwa Uingereza katika kile kinachohusiana na shughuli za kijeshi wakati wa maasi ya Mazrouei, na wakati Salim alipojiondoa kutoka cheo ya gavana, Ali Bin Salem akachukua mahali pake, na akawa anajulikana mwishoni kama Bwana Ali bin Salem, na Mombasa ilipoboreshwa mnamo 1907, Ali Bin Salem alikuwa na Uangalifu haswa kujenga barabara ambazo alizingatia chombo kikuu cha kuboresha jiji, ambapo alishiriki katika kamati ya barabara mnamo mwaka wa 1909, na alipendekeza kujenga barabara kuu kubwa inayopanua moja kwa moja kupitia kisiwa kutoka njia ya Freetown mpkaka kisiwa cha Likoni, na kwa sababu alitaka kuita barabara hii kwa jina la baba yake, yeye alichukua daraka la kununua ardhi kwa kujenga barabara hii kwa na kulipa ridhaa kwa wenyeji na miti ambayo ni lazima kukatwa kwa kujenga barabara, na katika mwaka wa 1910 alibadilishana ekari mia moja za ardhi na serikali ya kikoloni kwa kubadilishana na kipande cha ardhi katika kilindini na ramani ya eneo hilo, na licha ya ujenzi wa polepole na ugumu wa Barabara ya Salem, ifikapo mwaka wa 1914, barabara ilikamilika na kupewa jina la baba yake Salem Bin Khalfan.

Barabara ya Salem ilijulikana zaidi kwa soko la MacKinnon lenye shughuli nyingi, ambalo lilifunguliwa mnamo mwaka huo huo na lilipata jina la gavana wa kikoloni wakati huo, Bwan Henry MacKinnon, na wakati soko limebakia kituo muhimu cha biashara hadi sasa, baada ya uhuru, barabara ya Salem ilichukua jina jipya.

Ifikapo mwaka wa 1952, uasi wa Mau Mau uliongozwa na "Jomo Kenyatta" kupinga ukatili huu, ambao uliendelea mpaka kuwa vita vilivyodumu kwa miaka minane hadi mwisho wa utawala wa kikoloni nchini Kenya, kati ya jeshi la ardhi na uhuru la Kenya (KLFA) na mamlaka za Uingereza nchini Kenya.

Mnamo Oktoba ya mwaka huo huo, Kiongozi Kenyatta alikamatwa pamoja na watu wengine 20, na kuletwa mahakamani, ambayo ilidumu siku 90, baadyae  alihukumiwa kifungo cha miaka saba pamoja na kazi ngumu, na Waingereza walizindua kampeni ya kigaidi sawa na Afrika Kusini, na walitumia mizinga na ndege kugonga mambo ya "Mau Mau" katika milima ambapo walikuwa kujikinga.  Katika tarehe Januari 27, mwaka wa 1955 jumla ya hasara ilitangazwa, na kulingana na takwimu za kiingereza hasara zilifikia vifo 7800 kutoka kwa watu wa Mau Mau, na utekelezaji wa adhabu ya kifo katika 791, na hasara hizi hazijumuishi hasara za ndege na mizuka, pia kulikuwa na waafrika 7000 katika kambi za mateso na magereza, na kufukuzwa kwa watu 600,000 wa "Kikuyu" kutoka katika ardi yao, na kuharibu vibanda 150,000 kutoka vibanda vyao.

Misri ilikuwa ikishughulikia suala hili, na uasi huu uliungwa mkono na Rais wa Misri Gamal Abdel Nasser kupitia kampeni kubwa ya kidiplomasia ya vyombo vya habari dhidi ya Utawala wa Uingereza nchini Kenya, Na kwa amri yake, Misri ilianzisha kituo cha redio – “Sauti Ya Afrika” – kwa Kiswahili kusaidia Wakenya asili katika kupambana kwa ajili ya ukombozi kupitia kutangaza matukio nchini Kenya na kusaidia kikamilifu Wakenya wanaotaka uhuru, redio ya sauti ya Afrika ilifanya kutoka Maasi ya Mau Mau suala la kiafrika, na kituo hicho kilishawishi kuachiwa kwa Kiongozi wa Kenya Jomo Kenyatta aliyefungwa katika Kabingoria.

Hii haikuwa tu kile kilichofanywa na Rais Nasser na Serikali ya Misri kwa Wakenya, kwani ambapo Kairo ilikuwa mji mkuu wa kwanza kuwakaribisha wapiganaji wa ukombozi wa Kenya kama Vile, Tom Mbuya, James Gichuru, Oginga Odinga, Joseph Murumbi na wanachama wengine wa Vyama vya Kisiasa vya (Kano) na (Kadu).

Fayek anaonesha asili ya misaada iliyotolewa.. inatajwa kwamba msimamo wa Misri ulikuwa matumizi ya kauli ya Nasser katika falsafa ya mapinduzi: “sisi sitaweza kwa njia yoyote, hata kama tulitaka kusimama mbali na mgogoro wa umwagaji damu kwamba ni kwenda huko Afrika kati ya wazungu milioni 5 na Waafrika milioni 200” idadi ya watu wa Afrika wakati huo.

Fayek anasema: “Misri imepitisha suala la wazalendo nchini Kenya, hivyo ilizindua umakini kampeni ya vyombo vya habari na kidiplomasia dhidi ya vitendo hivyo vya kinyama, na iliagiza idhaa iliyotolewa kwa Kiswahili kwa jina la “Sauti ya Afrika” kwa watu wa Kenya, na watu wa eneo linalozungumzia lugha hii kushambuliwa ukoloni wa Uingereza ukali sana na kumchukulia kuwajibika kwa vitendo vyote vya ukatili na kuangamiza, na imebaini mpango wa Uingereza  kufanya Kenya nchi ya mtu mweupe, na  redio hii ilianza kama redio siri katika mara ya kwanza, na makao yake yalikuwa katika kambi moja huko Manshiyat Al-Bakri, na inafuata Urais wa Jamhuri moja kwa moja, kisha ilihamia kwa idhaa zilizotolewa kwenye redio ya Misri, lakini chini ya usimamizi wa mambo ya Afrika katika Urais wa Jamhuri”.

Fayek aliongeza: “tulikuwa tunapata habari sahihi tangu mwanzo kuhusu ukandamizaji na ubaguzi uliofanywa na waingereza nchini Kenya, na kupatikana kwa akili ya Misri, jambo ambalo lilifanya matangazo ya moja kwa moja ya redio”sauti ya Afrika” ya habari hizi kuwa na ushawishi mkubwa, ilikuwa redio ya kwanza kwa Kiswahili iliyotolewa kutoka Afrika, na inashughulikia suala la Waafrika, kuzungumza kwa niaba yao, na kushambulia ukoloni na ubaguzi wa rangi, na inaalika kwa mapinduzi makubwa kwa jina la Afrika na watu wake”.

Fayek anafichua: “redio hii iliweza kuwasilisha nyimbo nyingi za shauku kwa Kiswahili, baada ya kuwekwa katika melodia nzuri zilizoimbwa na baadhi ya wanafunzi wa Kenya jijini Kairo, na Misri ilifanya suala la “Mau Mau” na kuachia huru kwa “Jomo Kenyatta” suala la Afrika yote, na  pengine hili lilikuwa suala la kwanza la kiafrika kuchukua tabia hii barani kote, na ilikuwa kwa sababu ya msaada wa Misri”.

Na kama kuelezea Shukrani, wakati Kenya ilipata uhuru katika mwaka wa 1963, na ikawa Jamhuri mnamo1964, jina la barabara ya Salem lilibadilishwa kuwa barabara ya Abd elNasser.

Marejeleo

Kitabu cha "Abd ElNasser na Mapinduzi ya Afrika", Profesa Mohamed Fayek.

Kitabu "Historia ya Kiislamu - Enzi ya Ottoman", Mahmoud Shakir.

Kitabu cha "Harakati ya kisayansi huko Zanzibar na Pwani ya Afrika Mashariki", Dkt. Suleiman bin Saeed Al-Kiyumi.

Makala ikiwa  na kichwa "Mgogoro wa karne nyingi ukimalizika kwa kushindwa kwa Ureno kutoka kwa Usultani wa Oman... Historia ya uwepo wa Oman barani Afrika", tovuti ya Al-Masdar.

Ukurasa "Sio ukurasa wa Mfalme Farouk, wa kwanza na wa mwisho, Mwenyezi Mungu akipenda" kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

https://www.britannica.com/place/Cape-of-Good-Hope