Siku ya Kimataifa ya Wanubi

Siku ya Kimataifa ya Wanubi
Siku ya Kimataifa ya Wanubi
Siku ya Kimataifa ya Wanubi
Siku ya Kimataifa ya Wanubi
Siku ya Kimataifa ya Wanubi
Siku ya Kimataifa ya Wanubi
Siku ya Kimataifa ya Wanubi

Imetafsiriwa na/ Enas Abdelbassit
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled 


Wanubi waadhimisha kwenye tarehe 7, mwezi wa Julai, kila mwaka kama “Siku ya Kimataifa ya Wanubi” katika sehemu mbalimbali za dunia, Wazo la sherehe hiyo lilianza mnamo mwaka wa 2004 na vikundi kadhaa vya wanubi kwa ajili ya  kusherehekea eneo hilo kwa historia yake na urithi wake, Siku ya 7 ya mwezi wa Julai ilichaguliwa kwa ajili ya sherehe hiyo kwa sababu ya mahusiano yake na mila na desturi nyingi  za wanubi, kama vile kutembelea makaburi baada ya kifo huendelea kwa siku ya 7, kuwa mwanamke baada ya kuzaa hupita juu ya uvumba mara saba, na kwamba mtoto aliyezaliwa huingia maji ya Nile siku ya 7.

Wanubi ni miongoni mwa watu wa kale waliostaarabika duniani, waliishi karibu na Mto wa Nile kwa maelfu ya miaka katika eneo la kusini mwa Misri na kaskazini mwa Sudan, nchi za Nubia iligawanyika katika Falme tatu (Kush, Marwa na Nabata), na nchi za Bonde la Nile zilijumuishwa: Ethiopia, Tanzania, Sudan na Kong, Nubia za kale ziligawanywa katika maeneo matatu ya kijiografia, eneo la kaskazini ambalo lilikaliwa na wanubi “hazina” na kuzungumzia lugha ya Matuke, eneo la kati ambalo lilikaliwa na Waarabu na lina vijiji 6 na kuzungumzia lugha ya Kiarabu pamoja na kujifunza Nubia, na eneo la kusini ambalo lilikaliwa na watu wa Nubia Fadija.

Sherehe ya siku ya kimataifa ya wanubi ni mojawapo ya aina tofauti tofauti za kitamaduni ndani ya jamii ya kimisri, Mradi wa “bozoor” unazingatia dhana ya utofauti wa kitamaduni, kutafutia roho ya ushirikiano wa pande zote, na kuongeza thamani ya majadiliano,  inayokuza thamani ya Amani na kukataa vurugu.
Harakati ya vijana ya Nasser inategemea mikataba mingi ya kimataifa katika kuimarisha dhana ya utofauti wa kitamaduni, ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilipitisha “Azimio la UNESCO la Ulimwenguni juu ya utofauti wa kitamaduni” mnamo mwaka wa 2002, na kuweka utofauti wa kitamaduni kama mojawapo ya mambo ya urithi wa pamoja wa kibinadamu. Kifungu cha 1 cha Azimio hilo kinaeleza kuwa utofauti wa kitamaduni ni urithi wa pamoja wa wanadamu, na kwamba utamaduni huchukua aina mbalimbali katika nafasi na wakati. Tofauti hii inaonekana katika asili na utambulisho mbalimbali wa makundi na jamii zinazofanyiza wanadamu. Utamaduni mbalimbali, kama chanzo cha kubadilishana, upya na ubunifu, ni muhimu kwa jamii ya kibinadamu kama vile Bio-tofauti ni muhimu kwa viumbe hai. Kwa maana hii, utofauti wa kitamaduni ni urithi wa pamoja wa binadamu, na unapaswa kutambuliwa na kutekelezwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.

“Mkataba wa Kulinda na Kukuza Utofauti wa Njia za Kujieleza kwa Utamaduni”, uliopitishwa na UNESCO mnamo Oktoba 20, 2005, uliidhinisha malengo kadhaa, ambayo muhimu zaidi ni; kulinda na kukuza utofauti wa njia za kujieleza kwa kitamaduni, kuunda hali ambazo zinahakikisha kwamba tamaduni zinasitawi na zinaingiliana kwa uhuru na kwa njia ya kutajirisha, kukuza mazungumzo kati ya tamaduni ili kuhakikisha kuwa kubadilishana kwa kitamaduni kunafanywa kwa kiwango kikubwa na usawa zaidi ulimwenguni kusaidia heshima kati ya tamaduni na kueneza utamaduni wa amani, kukuza mawasiliano ya kitamaduni kwa lengo la kukuza mwingiliano kati ya tamaduni kwa roho ya kujitahidi kujenga madaraja kati ya watu, kukuza heshima kwa utofauti wa njia za kujieleza kwa kitamaduni na uelewa wa thamani yake kwa kiwango cha kitaifa.
Dira ya Misri 2030 inatafuta, kupitia mhimili wa utamaduni uliojumuishwa katika mwelekeo wake wa kijamii, kuunda mfumo wa maadili chanya ya kitamaduni katika jamii ya Wamisri, kuheshimu utofauti na tofauti, kujenga jamii yenye haki na umoja yenye sifa ya usawa katika kiuchumi, kijamii na kisiasa. Haki na fursa na kiwango cha juu zaidi cha ujumuishaji wa kijamii, inategemea sambamba na kusaidia makundi ya jamii.
Lengo la 10 la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa linahusu “kupunguza ukosefu wa usawa ndani na kati ya nchi”, ambalo linasema “kuwawezesha na kukuza ujumuishaji wa kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa wote, bila kujali umri, jinsia, ulemavu, rangi, kabila, asili, dini, hali ya uchumi au vinginevyo, ifikapo mwaka 2030”.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy