Kipindi cha kwanza: Misri na nyumba ya Afrika mnamo miaka 55 baina ya maendeleo na mabadiliko
1_ Nasser na Urais wa Umoja wa Afrika
kihistoria, Hii ni Urais wa nne wa Misri kwa Umoja wa Afrika _ Shirika la Umoja wa Afrika hapo awali_ Serikali ya Misri tangu zamani waliangalia kuwa na msimamo wenye ufanisi na wa pekee ambao una majukumu yanalinganisha na sifa za Misri na kuratiba na mahusiano yake ya asili katika bara letu la Afrika, ambapo yanaifanya muigizaji wa kikanda mwenye ushawishi katika usawa wa madaraka.
Urais wa kwanza wa Misri kwa Shirika la Umoja wa Afrika ulikuja katika mwaka wa 1964; yaani mwaka mmoja baadaye kutoka uanzishi wa Shirika. Na kutokana na juhudi endelevu za Misri kuelekea Afrika katika kipindi hiki, Rais Gamal Abd El Nasser alikuwa mtendaji, mpangaji na msimamizi mkuu wa Sera za nje za Misri kuelekea Afrika, Na vilivyomsaidia ni vyombo ya Utawala ambao ni ofisi ya mambo ya Afrika ya Urais wa Jamhuri ikiwemo Makada wa nchi kama "Helmy Shaarawy" na "Mohamed Fayek" pamoja na kamati kuu ya mambo ya Afrika, na baadhi ya vyombo vingine vya utekelezaji kama uongozi wa Afrika katika Wizara ya mambo ya nje ya Misri, vituo vya redio, vyombo maarufu kama kamati ya Ushirikiano ya Afro_ Asia ya Misri.
Mnamo kipindi hicho, Misri ilichukua jukumu kubwa katika masuala yote ya bara hilo, Na ilikuwa na jukumu katika kukabiliana na ukoloni wa jadi ambalo baadaye lilikuwa muhimu zaidi la ajenda ya Umoja, ambayo ilianzisha "kamati ya uratibu kwa ukombozi wa Afrika" na Misri ilianza tena jukumu lake la kuhimiza harakati za ukombozi kupitia muktadha mpya wa utendaji wa Afrika , Na bajeti ya Misri ilikuwa kubwa zaidi katika Shirika kwa kadri ya paundi 100,000 kwa mujibu wa kifungu Na 23 kutoka Hati ya uanzishi.
Kabla ya hapo, Misri ilikuwa ya kwanza ikihimiza harakati za ukombozi barani Afrika kabla ya kuanzisha Shirika; kwa sababu ya " Nasser" aliona katika wakati huo kuwa usalama wa taifa la Misri unahusishwa na usalama na uhuru wa nchi nyingine za bara; kwa hivyo ukombozi wa Misri kutoka ukoloni unahusishwa na nchi nyingine za bara; kutokana na hiyo aliwapokea viongozi kadhaa wa Afrika huko Kairo, ambapo aliwapa ulinzi na kufungua ofisi kwa wawakilishi wa harakati za ukombozi ikiwa huko Kenya, Nigeria, Uganda au Somalia kisha kutoa misaada ya kijeshi kwa harakati za ukombozi wa taifa; kwa mfano harakati za ukombozi wa taifa nchini Algeria, akibeba matukio ya ushiriki huo wa Ufaransa katika Uchokozi wa pande tatu kwa Misri, na asitoshe kwa hivyo tu bali alianzisha Jumuiya ya Afrika huko Kairo; kwa ajili ya kuratibu kati ya ofisi za harakati za ukombozi na shughuli zake katika muktadha wa siasa ya Misri, na ofisi zilifika ofisi na taasisi 22 mwanzoni mwa miaka sitini , na Jumuiya ilitoa mafunzo muhimu kama " maendeleo ya Afrika" na " Ujumbe wa Afrika" .
Na pia alitoa mafunzo kwa Makada wa harakati katika Taasisi za Misri , shule ya Saiqa na kitivo cha Vita, na haya yote yalichangia katika kutimiza kamati ya uratibu wa ukombozi wa Afrika wa Shirika la Umoja wa Afrika kwa lengo lake na bara nzima lilikomboa kutoka ukoloni, Kamati ilifilisi akaunti yake katika Benki baada ya kutimiza kazi zake zote.
Misri pia iliongoza katika kukabiliana masuala ya ubaguzi wa rangi; kwa hiyo ilikataa " Bantustans" na ilikuwa katika mawasiliano ya kudumu na raia wa Afrika na harakati za ukombozi, haswa Afrika kusini kupitia Makada wake huko Kairo kupitia vipindi vya redio kwa lugha ya Kiingereza, Kizulu, na kiswahili, na uungaji mkono wake kwa chama cha mkutano wa taifa ya Afrika ( ANC) na pia ilitoa msaada kwa
harakati za "ZANU" iliokuwa kukabiliana wazungu wachache huko Rohodesia_ Zimbabwe _ sasa.
Huu ulikuwa utangazaji kwa hali zilizoifanya Misri kuwa mkuu wa Umoja wa Afrika " Shirika la Umoja wa Afrika hapo awali" katika enzi ya Abd El Nasser , sera zilibadilika kwa mabadiliko ya Marais, lakini wote walikubaliana katika kutumia bara letu la Afrika, basi ni hali gani zilizoambatana katika kurudi kwa Misri kwa urais wa Umoja katika enzi ya El Sisi?