Wahitimu wa " Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kiafrika" wakitoa wimbo kwenye hafla ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa kiongozi marehemu Gamal Abdel Nasser

Wizara ya Vijana na Michezo, kwa Uongozi wa Dokta Ashraf Sobhy, ilizindua wimbo fulani unaohusu Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika, uliotekelezwa kwa Wizara hiyo kupitia "Idara kuu kwa Bunge na Elimu ya kiraia na Ofisi ya Vijana ya Afrika chini ya Uangalifu wa Waziri Mkuu Dokta Mostafa Madbouly, kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika, mnamo kipindi cha tarehe 8 hadi 22 Juni 2019 .
kuzindua kwa wimbo huo kunakuja sawasawa na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa kiongozi Gamal Abdel Nasser, ambapo uliimbwa na Kundi la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika ,chini ya usimamizi wa kiufundi kutoka Taasisi ya Africao kwa Sanaa.
inatajwa kwamba Udhamini wa Nasser kwa uongozi wa kiafrika ulilenga viongozi wakuu wa vijana 100 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika , watoa uamuzi wa sekta ya serikali, viongozi watendaji katika sekta binafsi, vijana wa Jamii ya kiraia, wakuu wa baraza la vijana la kitaifa, wanachama wa vyuo vikuu, watafiti katika vituo vya tafiti za kimikakati na mawazo, na washirika wa Vyama , wataalamu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari.
pia Udhamini wa Nasser unazingatiwa wa kwanza wa (kiafrika-kiafrika) unaowakilisha moja ya vyombo vya utekelezaji wa mpango wa Milioni 1 ifikapo 2021 kwa ajili ya kuwawezesha vijana waafrika milioni moja ifikapo 2021, iliotolewa kwa Kameshina ya Sayansi, Teknolojia na Rasilimali watu kwa Umoja wa Afrika hivi karibuni huko mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Wakati ambapo Udhamini huo unalenga kuhamisha Jaribio kale la kimisri katika kujenga taasisi za kitaifa, na kuunda kizazi kipya cha viongozi wakuu wa mabadiliko wa Kiafrika , wenye maoni yanayosawazisha na mwelekeo wa urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika, wenye imani ya kuhudumia malengo ya umoja wa Afrika kupitia Ukamilifu , pamoja na kuanzisha mkusanyiko wa viongozi wachanga wa Kiafrika wenye athari kubwa Barani, kwa mafunzo, ustadi unaohitajika , na mitazamo ya kimikakati.