Baraza la Kiutamaduni la Kiingereza lamtukuza "Ghazaly", Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana kwa juhudi zake za kukuza Diplomasia ya Vijana

Baraza la Kiutamaduni la Kiingereza lamtukuza "Ghazaly", Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana kwa juhudi zake za kukuza Diplomasia ya Vijana

 Taasisi ya Empower Hub imemtunuku Mtafiti wa Anthropolojia, Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Harakati ya Nasser kwa Vijana, ikiwa ni sehemu ya hafla ya kufunga mpango wa "Gender and Climate Guide Book ", uliofadhiliwa na Baraza la Kiutamaduni la Kiingereza, Ijumaa, Machi 10, sanjari na Siku ya Wanawake Duniani, kwa mahudhurio ya Dkt.Amr Ramadan, Meneja wa mpango huo, na Mkurugenzi wa Programu za Elimu isiyo Rasmi katika Baraza la Kiutamaduni la Kiingereza Bi.Yusr Jadu mbele ya viongozi wa vijana wenye ushawishi mkubwa katika masuala ya uwezeshaji wa kiuchumi, hali ya hewa, ujasiriamali na mazingira.

 Kwa upande wake, Hassan Ghazaly alithibitisha kupitishwa kwake na imani katika msingi wa  usawa wa nafasi kijinsia katika programu na miradi yote anayoyaandaa kwa kuzingatia Dira ya Misri ya kitaifa 2023, Ajenda ya Afrika ya 2063, na Ajenda ya kimataifa ya Maendeleo Endelevu, akiashiria  umuhimu wa michango ya wanawake ndani ya Harakati Nasser kwa Vijana.


 Ghazaly pia aliwasifu baadhi ya viongozi wa vijana wa kike  ambao wamehitimu Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na kwa sasa ni wanachama mashuhuri wa Harakati hiyo ya Nasser kutoka Utaifa mbalimbali wa Kiarabu, Kiafrika, Asia na Kilatini, ambapo ndani ya mazingira magumu haya waliweza kushika nyadhifa za Uongozi na kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii zao.

Ikumbukwe kuwa Mpango wa Gender and Climate Guide Book  ulianza mnamo Oktoba 2022 kwa ufadhili wa Baraza la Kiutamaduni la Kiingereza, ukijumuisha mafunzo yaliyogawanywa katika makundi matatu, kila kundi lilijumuisha wanafunzi 75 ambao waligawanywa katika vikundi takriban 10, na ilipangwa kuwa kila mmoja wao atatekeleza mradi wa kuhitimu kwa kuzindua warsha 20 za kazi halisi katika maeneo na jamii tofauti, na zilitawanyika hivyo kwa ajili ya kuhakikisha mabadiliko makubwa zaidi, kisha kuandaa ripoti ya mwisho kwa kila mradi katika maandalizi ya kuwasilisha matokeo yake katika sherehe ya kufunga ya mradi huo mnamo Machi 2023, ambayo hatimaye ilisababisha ushindi wa timu tatu ambazo zilikuwa na ushawishi mkubwa zaidi, kama Powderpuff Girls ilishinda Nafasi ya kwanza ilitolewa na zawadi ya paundi 10,000 kama msaada wa kukamilisha warsha za mradi huo, wakati Timu ya "EcoColors" ilishika nafasi ya pili, na timu ya "Equalizers" ilishika nafasi ya tatu.