Maadhimisho ya Kukamilika kwa Kampeni ya Kitaifa ya Kuokoa Mambo ya Kale ya Nubia ya Misri kwenye Eneo la Ushindi wa Ajabu na Usio wa Kawaida
Imetafasiriwa na/ Mariz Ehab
Imeharirwa na/ Mervat Sakr
Hekalu Kuu la Abu Simbel, lililoanzia enzi za Mfalme Ramses II 1279 - 1212 KK, liliwekwa wakfu kwa ibada ya miungu mikubwa ya serikali wakati huo, yaani "Ra Hor-akhti", "Ptah" na "Amun", wakati hekalu dogo liliwekwa wakfu kwa mungu wa "Hathor" na Malkia Nefertari, mke mkuu wa mfalme, na Sehemu ya mbele ya Hekalu Kuu ina sanamu nne kubwa za Ramses II, ambazo kila moja ni Urefu wa mita 20, Iliundwa ili jua liangaze juu ya Uso wa sanamu ya Ramses iliyo katika Patakatifu pa Patakatifu ndani ya hekalu wakati wa jua. Jua lazima liwe sawa na Uso wa Mfalme Ramesses II kwa siku mbili kwa mwaka moja ambayo huanguka mnamo Oktoba 22, na nyingine mnamo Februari 22, na inasemekana kwamba wanaadhimisha kuzaliwa kwake na kumbukumbu ya kuingia kwake kwenye kiti cha enzi cha Misri.
Uchunguzi umeonesha kuwa mahekalu ya Abu Simbel yako hatarini kuzama kutokana na mkusanyiko wa maji katika Ziwa Nasser baada ya ujenzi wa Bwawa Kuu, hivyo serikali ya Misri iliona haja ya kuhamisha mahekalu ili kuyalinda yasizame na kisha kukimbilia UNESCO mwaka 1959, nayo iliyofanya kazi ya kuhamasisha msaada wa jumuiya ya kimataifa kuelekea suala la kuokoa mahekalu ya Nubia.

Kazi ya mradi huu mkubwa wa kimataifa ilikamilishwa kati ya 1964 na 1968, kwa msaada wa UNESCO kama operesheni kubwa zaidi ya Uhandisi na akiolojia ili kuokoa mahekalu ya Abu Simbel, iliyojumuisha wafanyakazi na wahandisi wa 2000, mashirika ya kimataifa, kwa gharama ya karibu dola milioni 40, na aina mbalimbali za cranes kubwa na cranes zilizotokana na misumeno ya mkono na ng'ombe zilitumika katika mchakato huu wa kiufundi na Uhandisi, kama mpango ulihitaji hekalu kubwa lihamishwe na sanamu zake kubwa, baada ya kuikata kuwa mawe makubwa yenye Izito wa tani 1-2 kila mmoja, na baada ya kupiga picha na kuinua Uhandisi ulianza kukata mawe ya hekalu katika vipande vyenye uzito kati ya tani 10-15 kwa kila kipande, wakati idadi ya vipande ilifikia vipande 5000, katika maandalizi ya kuisogeza kwa Umbali wa mita 65 mbali na mto, na hadi mita 200 upande, kuwekwa tena kwenye kilima bandia, baada ya kuchukua hatua zote za kiufundi kutoka kupata taa, kupima Usalama kutoka kwa tetemeko na majanga, na kupima joto na Unyevu, iliyofanya ionekane katika muonekano sahihi sana na wa kitaalamu kama hapo awali.
Ikumbukwe kwamba jina "Abu Simbel" lilipewa tovuti hii na msafiri wa Uswisi "Johann Ludwig Burckhardt", anayejulikana kama "Ibrahim Burckhardt", aliyegundua tovuti hiyo mnamo 1813 wakati alipochukuliwa kwake na mtoto aitwaye "Abu Simbel".
Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy