Mapokezi ya watu wa Sudan kwa Rais Abd El- Nasser huko Khartoum ni uthibitisho wa Umoja wa Bonde la Mto Nile
Mnamo Agosti 29, 1967, viongozi wa kiarabu wakiwa wajiandae kwa mkutano wa kilele wa nne wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, uliofanyika nchini Sudan,pia unaojulikana kama Mkutano wa Hakuna mara tatu (Hakuna Amani, Hakuna Kutambuliwa, Hakuna Majadiliano na Israeli), mara tu baada ya ndege ya Rais Gamal Abdel Nasser kutua katika uwanja wa ndege wa Khartoum, aliwakuta Mamilioni ya watu wa Sudan wakimkaribisha kwa njia isiyokuwa ya kawaida Wakiimba kwa jina la Abdel Nasser, maisha ya mshikamano wa kiarabu, na Umoja wa Waarabu, na umati uliendelea nyuma ya Abdel Nasser hadi wakampeleka kwa hoteli ambamo anamokaa, na mapokezi hayo makubwa yalikuwa Kama kielelezo cha dhati cha Umoja wa kina unaowaunganisha watu wa Bonde la Mto Nile.
Maamuzi ya mkutano wa kilele wa kiarabu yalikuja kama uthibitisho wa Umoja wa safu za Waarabu, na Kukomesha matatizo yote,na kufuata Hati ya Mshikamano wa kiarabu, pia kuongeza juhudi za kuondoa athari za uvamizi, na kuhakikisha uondoaji kabisa wa vikosi vya Israeli kutoka eneo hilo, kwa kuzingatia kwamba ardhi zinazochukuliwa vibaya ni za kiarabu, mzigo wa kuzirejesha unaangukia nchi zote za kiarabu, na hiyo ni kwa mujibu wa kanuni za msingi za mkutano huo, ambazo ni: Hakuna Amani na Israeli ,au kutambuliwa kwake kama nchi, au mshikamano nayo.
Wakati wa moja ya vikao vya mkutano huo, Rais Abdel Nasser alitoa maelezo ya kina kuhusu msimamo wa kiarabu, ambapo alisema: "Hatuna chochote isipokuwa upinzani na hatuna njia nyingine kwa sababu hiyo ndiyo ni njia ya maisha."
Pia Rais Abdel Nasser alielezea mapokezi ya watu wa Sudan kwake kama yanazidisha matumaini ndani ya nafsi yake na mustakabali anaouota kwa taifa hilo la Kiarabu, na alisifu msimamo wa kishujaa wa ndugu wa Sudan, ambao ulikuja kama jibu zito sana kwa majaribio ya nje ya nguvu za uadui kwa kulazimisha kujisalimisha na kueneza kukata tamaa ndani ya roho.