Jukwaa la Nasser la Kimataifa latangaza Uzinduzi wa Fomu ya Ushiriki kwa Kundi la Tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Jukwaa la Nasser la Kimataifa latangaza Uzinduzi wa Fomu ya Ushiriki kwa Kundi la Tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari asubuhi hii, Jukwaa la Nasser la Kimataifa limetangaza Uzinduzi wa Fomu ya Usajili kwa Kundi la Tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, ambalo litafanyika katika kipindi kijacho chini ya Ufadhili wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, na ushiriki wa vijana wa 150 wanaume na wanawake kutoka kwa viongozi wa vijana wenye utaalamu mbalimbali wa utendaji, na vijana wenye nguvu na wenye ushawishi duniani kote.


Mwanaanthropolojia Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Jukwaa la Nasser la Kimataifa, alieleza kwamba Kundi la Tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa linawalenga viongozi wa 150 kutoka nchi mbalimbali za ulimwengu, Miongoni mwao ni Watoa maamuzi kwenye sekta ya umma, Wahitimu wa Mpango wa Kujitolea wa Umoja wa Afrika, Wahitimu wa Mpango wa Kujitolea wa Umoja wa Mataifa, Wahitimu wa Chuo cha Kitaifa kwa Uongozi, Viongozi watendaji katika sekta binafsi, Wawakilishi wa Kamati za Kitaifa za Tamasha la Vijana Duniani, pamoja na Wawakilishi wa Matawi ya Kitaifa ya Mtandao wa Vijana wa Harakati ya Kutofungamana na Upande Wowote, Wanaharakati wa Asasi za Kiraia, Wakuu wa Mabaraza ya Vijana wa Kitaifa, Wajumbe wa Mabaraza ya Mitaa, Viongozi wa vijana wa vyama vya kisiasa, Wahadhiri wa vyuo vikuu, Watafiti kwenye Vituo vya Utafiti wa Kimkakati na Mizinga ya Kufikiri, wanachama wa vyama vya kitaaluma, Wataalamu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari, na Wajasiriamali wa kijamii.

Mwanzilishi wa Jukwaa la Nasser la Kimataifa aliongeza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tano unalenga kuchagua kikundi cha viongozi wa vijana duniani kote kulingana na vigezo sahihi na vya haki, kuonesha kujitolea kwa misingi ya uwazi na usawa wa fursa. Vigezo hivi vinazingatia Maono ya Misri 2030, Malengo ya Maendeleo Endelevu, na ajenda za kikanda na kimataifa. Alisisitiza kuwa mfumo kamili wa kuchagua washiriki unahakikisha utekelezaji wa haki ya kijamii na uvumbuzi wa uongozi. Aidha, alieleza kuwa miongoni mwa masharti ya Ushiriki kwenye Udhamini huo ni kwamba waombaji wanapaswa kuwa kati ya umri wa miaka 18 na 40, na vijana kutoka nchi za Ulimwenguni Kusini kama vile Afrika, Asia, Amerika ya Kilatini na na nyinginezo.

Ni vyema kutajwa kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni mojawapo ya juhudi za Misri zinazochangia kuunga mkono maendeleo ya kimataifa kupitia kuimarisha sifa ya makada wanaostahili kwa ajili ya huduma kwa kutoa aina zote za msaada, kufuzu na mafunzo kama mojawapo ya utaratibu wa maandalizi ya kuwawezesha katika nafasi za uongozi na utendaji, na kufaidika na uwezo na mawazo yao. Udhamini huo pia unawalenga viongozi wa vijana wenye taaluma mbalimbali na ufanisi wa utendaji ndani ya jamii zao, na unataka kuhamisha uzoefu wa maendeleo ya Misri katika kuimarisha taasisi na kujenga utu wa kitaifa.

Fomu ya Maombi: https://nasserforum.com/apply