Shirikisho la Wachezaji wa Olimpiki Afrika Lafanya Mikutano yake Misri

Shirikisho la Wachezaji wa Olimpiki Afrika Lafanya Mikutano yake Misri

Imetafsiriwa na: Hussein Mohammed 
Imehaririwa na:  Mervat Sakr 
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Shirikisho la wachezaji wa Olimpiki barani Afrika limefanya kikao kuhudhuria Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri, Dkt. Ashraf Sobhy na wanachama 25 kutoka bara la Afrika kutoka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ambayo inajumuisha nchi 150 duniani kote, inayofanyika kujadili mipango imeyotekelezwa katika nchi za Afrika ili kuwahudumia wanariadha wa Olimpiki na mipango iliyopendekezwa na baadhi ya nchi kwa wanariadha wa Olimpiki katika kipindi kijacho. 

Shughuli hizo zilihudhuriwa na Bw. Jawwal Bozo, Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji wa Olimpiki Duniani, Dkt. Hassan Mustafa, Mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mikono, Mustafa Beraf, Mwenyekiti wa Chama cha Kamati za Olimpiki za Afrika (ANOCA), Mhandisi Hisham Hatab, Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, Mhandisi Sherif El-Erian, Mwenyekiti wa Shirikisho la Pentathlon la Misri na Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, Dkt. Ehab Amin, Mwenyekiti wa Shirikisho la Gymnastics la Misri, Mamdouh El-Sheshtawy, Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, na kikundi cha wanariadha wa Olimpiki wa Misri na Afrika.

Katika hotuba yake, Waziri wa Vijana na Michezo Dkt. Ashraf Sobhy aliwakaribisha washiriki hao, akielezea furaha yake kwa uwepo wake katika mkutano huu mkubwa wa kuwatumikia wanariadha wa Olimpiki katika bara la Afrika, akiashiria nia yake ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zote za bara hili kuendeleza michezo ya Afrika kwa kuzingatia maelekezo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, kuimarisha ushirikiano na uratibu endelevu na nchi za bara la Afrika katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na michezo na vijana.

Waziri huyo alisema kuwa mkutano huo ulifanyika kwa mara ya kwanza katika bara la Afrika, hasa nchini Misri, ambapo kuna wawakilishi 50 wa nchi zinazoshiriki katika mashindano hayo, kutokana na Misri kuwa na utaratibu wa kipekee wa matukio, matukio na mashindano ya michezo, na kusisitiza jukumu la Misri katika michezo katika kipindi cha sasa, kinachoshuhudia shirika la Misri na mwenyeji wa mashindano mengi ya kimataifa ya michezo na mikutano.

Chama cha wachezaji wa Olimpiki wa Afrika kimemheshimu Waziri wa Vijana na Michezo, Mwenyekiti wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa mikono, Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, Mwenyekiti wa ANOCA, viongozi wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, na wachezaji wa Olimpiki wa Misri na Afrika, na Chama pia kilimshukuru na kumpongeza Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri kwa ubora na maendeleo makubwa yaliyoshuhudiwa na michezo ya Misri, aliyoshuhudia wakati wa uwepo wake nchini Misri hivi karibuni.