Harakati ya Nasser kwa Vijana ni mojawapo ya matokeo ya kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na sasa ni mshirika

Harakati ya Nasser kwa Vijana ni mojawapo ya matokeo ya kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na sasa ni mshirika

Imefasiriwa na / Alaa Zaki

Harakati ya Nasser kwa Vijana ni mojawapo ya matokeo ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kundi la Julai, 2019" pamoja na uangalizi wa Waziri Mkuu Dkt. Mostafa Madbouly, na ilichukua jina la Rais wa zamani wa Misri Gamal Abdel Nasser kama jina lake, ambapo ni miongoni mwa mifano ya kipekee ya uongozi katika nchi zetu zinazoendelea, kwa hivyo aliitwa "Baba wa Afrika" ", ambayo ni mfano wa Afro-Asian na mfano wa kisiasa na kihistoria wa dhana ya uongozi wa mabadiliko.

Kwa upande wake, kiongozi aliyetaka kuunga mkono harakati za ukombozi katika nchi zinazoendelea hadi kupata uhuru wake. Hiyo kwa upande wa kihistoria, ama kwa upande unahusu mustakabali, Harakati ya Nasser kwa Vijana  inakuja kama nyenzo ya uendelevu wa udhamini huo, iliyozinduliwa kutoka kwa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, ili kuchangamsha malengo ya "Mkataba wa Vijana Waafrika" ndani ya jamii kupitia wahitimu wa udhamini wa Nasser na kueleza matarajio ya “Ajenda ya Afrika 2063” katika ngazi ya chini na kusonga mbele katika kuyafikia, pamoja na kuunganisha kanuni za “Shirika la Mshikamano la Watu wa Afrika na Asia” na kanuni za nchi zisizofungamana kwa upande wowote, kwa hivyo Harakati ya Naseer kwa Vijana inazingatiwa kama jukwaa linalonyumbulika kwa vijana ili kukuza ujuzi wao, ili baadaye kuwa mwigizaji wa kimataifa kwa hilo Jukumu lenye ushawishi, kama ilivyoainishwa katika Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030.

Wahitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi walikuwa na nia ya kuunda mtandao wa mahusiano nchini Misri ili kuimarisha njia za ushirikiano kati ya taasisi za Misri na wenzao katika nchi mbalimbali za Afrika. Kwa mfano tu tunataja ushirikiano uliofanyika kati ya Jumuiya ya wahandisi Wamisri ( inayojumuisha wahandisi zaidi ya 700,000) na Jumuiya ya Wahandisi Wazambia "Shirika la Uhandisi la Zambia" ( inayojumuisha wahandisi zaidi ya 45,000), walitia saini Mkataba wa Maelewano mnamo Septemba 17, mwaka wa 2019, wakati wa shughuli za ufunguzi wa Wiki ya Sita ya Uhandisi Afrika huko Livingstone, Zambia.  Mkataba wa Maelewano unatoa fursa ya kubadilishana uzoefu jambo linaloruhusu wahandisi Wazambia kushiriki katika programu za kujenga uwezo nchini Misri, pamoja na kuanzisha vifaa vya mafunzo nchini Zambia.

Tangu kuzinduliwa kwake, Harakati ya Nasser imefanikiwa kuunda msingi wa viongozi vijana wenye ushawishi mkubwa katika ngazi ya ndani katika bara zima, ili kuweka ufumbuzi endelevu kwa matatizo ya Afrika kwa mafunzo, ujuzi muhimu na maoni ya kimkakati, na imefanya kazi kuunda mtandao wa vijana wa wahitimu wa Udhamini wa Nasser katika ngazi ya bara la Afrika ili kutumikia malengo ya Umoja wa Afrika, katika jaribio la kutoa fursa kwa vijana kukutana na watoaji wa maamuzi na wataalamu, kubadilishana uzoefu na kutangaza mifano yenye mafanikio, pamoja na kuchukua kama kuzingatia tofauti za mitaa.