Mhitimu wa Udhamini wa Nasser ashinda  Uongozi wa Umoja wa Wanafunzi waafrika nchini Misri

Mhitimu wa Udhamini wa Nasser ashinda  Uongozi wa Umoja wa Wanafunzi waafrika nchini Misri

Abdul Majeed Alan Shikula wa Malawi, Mwanachama wa Harakati  ya Nasser kwa Vijana na Mhitimu wa Udhamini  wa   Nasser kwa Uongozi , alishinda Uongozi wa Umoja Mkuu wa Wanafunzi waafrika katika Jamhuri ya Kiarabu ya  Misri, akawa Kiongozi wa kwanza kwa Umoja huo kutoka Afrika  Kusini. 

Shekola, Mwanafunzi wa Kitivo cha Kilimo, Chuo Kikuu cha Kairo, amechaguliwa kushiriki katika Udhamini wa  Nasser kwa Uongozi, uliozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo (Ofisi ya Vijana ya Afrika kwa Ushirikiano na idara kuu  ya  Bunge na Elimu ya Uraia). mnamo Juni 2019, ukiwa na viongozi 100 wa vijana katika Barani Afrika,  ulioathiri  - kutokana na maneno yake - katika kazi yake kama  Mwanaharakati na Mwenye Ushawishi wa kijamii pamoja na kukuza  imani yake kubwa kwa msingi wa "Pan-Africanism".

kwa upande wa maoni yake ya Umoja wa Wanafunzi waafrika, “Shikula” anaona  kuwa yeyote atakayeshika cheo  hicho anapaswa  afanye juu chini  kwa ajili ya maslahi kuu ya Afrika, na kuangalia kuwawezesha wanafunzi waafrika sambamba na Ajenda ya Afrika ya 2063,  hiyo ndiyo lengo lake analolitafutia  wakati wa uongozi wake   kwa Umoja huo . 

Kwa kuzingatia mafanikio yasiyo ya kifani ya bara la Afrika yaliyofikiwa na Udhamini huo , Wizara ya Vijana na Michezo inajiandaa kuzindua toleo la pili la Udhamini wa  Nasser kwa Uongozi pamoja na Ufadhili wa Rais Abd El Fatah El-Sisi ambapo  ilivyopangwa kwa mara ya kwanza, kujumuisha na kushiriki kwa kundi la viongozi wa vijana wanaowakilisha mabara ya Asia na Amerika ya  Kusini pamoja na Bara la Afrika.