Jumuiya ya Afrika... Nyumba ya Afrika 

Jumuiya ya Afrika... Nyumba ya Afrika 
Jumuiya ya Afrika... Nyumba ya Afrika 
Jumuiya ya Afrika... Nyumba ya Afrika 
Jumuiya ya Afrika... Nyumba ya Afrika 
Jumuiya ya Afrika... Nyumba ya Afrika 
Jumuiya ya Afrika... Nyumba ya Afrika 
Jumuiya ya Afrika... Nyumba ya Afrika 
Jumuiya ya Afrika... Nyumba ya Afrika 
Jumuiya ya Afrika... Nyumba ya Afrika 
Jumuiya ya Afrika... Nyumba ya Afrika 
Jumuiya ya Afrika... Nyumba ya Afrika 

Wanadiplomasia na wanafunzi wa Afrika nchini Misri wanaiita "Nyumba Ya Afrika". Jumuiya ya Afrika ilianzishwa mnamo 1956 na baadhi ya wasomi wa Misri, maprofesa wa vyuo vikuu na wanadiplomasia wa Misri na ilitangazwa kama mkusanyiko wa kiutamaduni na jukwaa la kimawazo kwa wale wanaohusika masuala ya kiafrika nchini Misri.  

Imeasisiwa katika nyumba ya mwanadiplomasia marehemu (Mohamed Abdel Aziz Ishaq), na ilikuwa mwelekeo wa wanafalsafa na wanamapinduzi waaminifu wakati wa mapinduzi matukufu ya Julai (1952) kwa kuzingatia sera ya Gamal Abdel Nasser na mwelekeo wake kuelekea bara la Afrika na kuipa kipaumbele maalum kama mojawapo ya nguzo muhimu za maslahi ya kisiasa katika mapinduzi ya Misri.  

Mwishoni mwa miaka ya hamsini, ilijumuisha ofisi 29 za vyama vya ukombozi wa Afrika kutoka nchi za mashariki, magharibi na kusini mwa bara hilo.Misri ilitoa kwake kila aina ya nyenzo ya kifedha, vyombo vya habari na uungaji mkono wa kisiasa katika majukwaa yote ya kimataifa na kutoa wito wa kukombolewa kutoka kwa ukoloni kwa watu wote wa bara la Afrika, baada ya kuunga mkono harakati za ukombozi na uhuru wa nchi za Kiafrika, Jumuiya hiyo ikishughulikia suala la kubatilisha tawala na sera za ubaguzi wa rangi katika nchi kadhaa. 

Nguzo muhimu  za Jumuiya ni katika sekta za mafunzo, Maendeleo ya Binadamu, Kujiboresha, Utamaduni, Mazingira, Watoto na Wanawake. Mkuu wa Jumuiya sasabhivi ni: Balozi Muhammad Nasr El-Din. 

Kwa mafanikio ya juhudi zake, ikishughulikia kuimarisha mahusiano na balozi na wanadiplomasia wa Afrika walioidhinishwa huko Kairo, pamoja na wanafunzi waafrika wote wa wanaosoma katika vyuo vikuu na taasisi za Misri, pamoja na kufadhili shughuli za Umoja Mkuu wa Wanafunzi wa Afrika nchini Misri. 

Hiyo ndiyo iliyopelekea kupitishwa kwa Jumuiya ya Afrika kama mwanachama mwangalizi wa Shirika la Haki za Binadamu la Afrika, uanachama wake katika Kamati ya Ushauri ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya Umoja wa Mataifa, na kuzingatiwa kama chombo cha wataalamu katika Jumuiya ya Nchi za kiarabu kwa kuwa mwanachama wa Shirikisho la Mkoa wa NGOs na mwanachama wa Shirikisho la Mkoa wa Jumuiya za Mazingira.