Idumu Misri, Idumu Afrika.. mwaka wa kazi ya dhati

Idumu Misri, Idumu Afrika.. mwaka wa kazi ya dhati

Na/ Kitengo cha Tafiti za Ofisi ya Vijana ya Afrika - Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri

Utangulizi:

Kutokana na kujihusisha kwa Misri ndani ya Bara na mazingira yake ya Afrika, pia imani yake kwamba utulivu wa bara la Afrika uko na kipaumbele kikubwa kimoja cha  vipaumbele vya sera ya kigeni ya Misri, Urais wa Misri wa Umoja wa Afrika ulikuja ili kueleza vijambo vilivyounda sera ya kigeni ya Misri kuelekea bara hilo, na ili kuongeza nafasi kubwa ya Kairo kati ya ndugu waafrika na jambo lililoongezeka sana wakati wa Rais El Sisi kuchukua hatima za mambo, Mwaka mzima umepita tangu Rais Abdel Fattah El-Sisi kushika wadhifa wa urais wa Umoja wa Afrika katika mkutano wa kilele wa Afrika mjini Addis Ababa mwezi Februari 2019, na kupitia urais wake kwa Umoja wa Afrika, Misri ilishughulikia kazi hii kama imani inayothamini kutoka kwa viongozi wa nchi za kiafrika nchini Misri na uongozi wake, na wakati huo huo, kama jukumu linalopaswa kutimiza kwa bara na watu wake, na hii ni mara ya nne katika historia, Misri inayoshikilia bendera ya Bara la Afrika, na ya kwanza kwake, yenye jina jipya la shirika kubwa zaidi barani Afrika, "Umoja wa Afrika", ambapo Misri imechukua kiti cha uongozi mara tatu hapo awali, zote ikiwa ni baada ya Umoja wa Afrika kuutaja Shirika la Umoja wa Afrika.

Katika muktadha huu, na mnamo kipindi kizima cha mwaka huu, uongozi wa Misri ulisonga mbele zaidi ya ngazi moja kwa ajili ya maslahi ya watu wa Afrika, kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano kati ya Misri na nchi za Afrika, na kati ya watu wa Afrika na wao kwa wao.

Misri ilitwaa urais wa Umoja wa Afrika Februari 10, 2019, kwa mara ya nne katika historia yake, na kwa mara ya kwanza chini ya jina jipya la "Umoja wa Afrika.", ambapo Misri ilishikilia kiti cha urais mara tatu hapo awali, Misri ni moja ya nchi waanzilishi wa Shirika la Umoja wa Afrika, Rais Abdel Fattah El-Sisi katika hotuba yake, katika mkutano wa kilele wa Afrika, uliofanyika katika mji mkuu wa Ethiopia, Adis Ababa, alithibitisha kwamba Misri itafanya kazi kwa bidii ili kuendeleza njia kuelekea marekebisho ya kimuundo na kifedha ya muungano na kukamilika kwa mafanikio yameyopatikana ili kuunganisha umiliki wa nchi wanachama wa shirika lao la bara na katika harakati za kuendeleza zana na uwezo wa Muungano na tume zake ili kukidhi matarajio ya watu wa Afrika.

Rais Abdel Fattah El-Sisi pia ameshiriki katika makongamano na mikutano mingi ya kimataifa, tangu ashike urais wa Umoja wa Afrika, aliyoongoza idadi kadhaa kwa ushirikiano na viongozi wa Dunia katika mabara 4: Ulaya, Asia, Afrika na Amerika Kaskazini, katika mikutano yote hiyo ya kilele, alikuwa mtetezi hodari na muwazi wa haki za watu wa Afrika kupata amani, utulivu, maendeleo na ustawi, ambapo alisema kuwa, mnamo mwaka wa 2019, kazi itafanywa ili kuimarisha mifumo ya maendeleo endelevu ili kutoa fursa zaidi za kazi kwa vijana wa Kiafrika, akidokeza kuwa bara la Afrika linaahidi kuwa na fursa nyingi, na kwamba mapato ya maendeleo lazima yafikie sehemu zote za bara hilo kwa haki.

Kwa hiyo, baada ya Mkutano wa kilele wa Afrika, Rais Abdel Fattah El-Sisi alikuwa kwenye jukwaa la Mkutano wa Usalama wa Munich nchini Ujerumani kwa ajili ya amani barani Afrika, basi katika Mkutano wa Umoja wa Ulaya na Afrika huko Austria, na kisha katika Kongamano la China na Afrika mjini Beijing,na kisha katika Mkutano wa Japan na Afrika (TICAD) huko Tokyo, na mkutano wa kilele wa mataifa yaliyoendelea kiviwanda G7 katika Paris, na mkutano wa kilele wa G20 huko Osaka, Japan, na kisha katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, na kisha mkutano wa Ushirikiano wa G20 na Afrika nchini Ujerumani, na kisha mkutano wa kilele wa Waafrika na Urusi huko Sochi, na kisha Mkutano wa Uwekezaji wa Uingereza na Afrika huko London (Januari 2020), Kwa hiyo, katika majukwaa yote hayo na mengine ya kimataifa, Rais Abdel Fattah El-Sisi alikuwa mwelezaji bora wa masuala ya bara la Afrika na mtetezi wa haki na maslahi yake.

Kwa hivyo, jukumu la Misri linaweza kuangaziwa kupitia urais wa Misri wa Umoja wa Afrika kupitia pande tatu:

Upande wa Kwanza: Kuimarisha Amani na Usalama Barani Afrika

Upande wa pili: Katika ngazi ya Kiafrika

Upande wa tatu: mahusiano kati ya Misri na watu wa Afrika

Upande wa Kwanza: Kuimarisha Amani na Usalama Barani Afrika:

Rais alifanya juhudi wakati wa mikutano ya nchi mbili na ya kikundi cha Afrika, ikiwa ni pamoja na jukumu la Misri katika maelewano kati ya Kenya na Somalia, Pamoja na kuunga mkono kwa Rais Sisi kwa mpango wa kunyamazisha bunduki Barani Afrika (2020), na mbali na jukumu la kujenga la Misri kuhusu maendeleo ya Sudan,Vilevile juhudi za Misri za kusuluhisha mgogoro wa sasa wa Libya. Jukumu la Misri katika kukuza amani na usalama barani Afrika linaweza kuangaziwa kupitia yafuatayo:

Mkutano wa Usalama wa Munich mnamo Februari 15, 2019:

Rais El Sisi alitoa hotuba wakati wa kikao kikuu cha mkutano huo, na kumshirikisha Kansela wa Ujerumani, Kuwa mkuu wa nchi wa kwanza ambaye sio Mzungu kushiriki katika kikao kikuu tangu mkutano huo uanzishwe mnamo 1963, Rais aliwasilisha maono ya Misri ya kuimarisha kazi za Afrika katika hatua inayofuata. Na kwa kuzingatia urais wa Misri wa Umoja wa Afrika, Hii inafanywa kwa kukuza ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda katika ngazi ya bara, na kuwezesha harakati za biashara ya ndani ya kikanda, na ndani ya muktadha wa Ajenda ya Afrika ya 2063 ya Maendeleo Jumuishi na Endelevu, Pamoja na kukuza juhudi za ujenzi na maendeleo ya baada ya migogoro.

Mkutano wa Wabunge la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini:

Misri ilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wabunge katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini kuanzia Februari 20 hadi 23, Rais Abdel Fattah El-Sisi alithibitisha umuhimu wa jukumu la Bunge la Afrika katika kufanya kazi ili kuinua ufanisi wa huduma za mashtaka katika bara na kujenga uwezo wa wajumbe wake,akiashiria uungaji mkono wa Misri kwa jukumu la Bunge chini ya urais wa sasa wa Misri wa Umoja wa Afrika, na kwa kuzingatia kwamba kukuza hatua za pamoja za Afrika ni moja ya vipaumbele vya urais wa Misri wa Muungano.

Katika muktadha huu, Rais alipitia maoni ya Misri ya kupambana na ugaidi, inayotegemea kukabiliana na jambo hili katika nyanja zake zote, ikiwa ni pamoja na masuala ya usalama, kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiakili na kidini,na pamoja na kushughulikia taratibu za ufadhili, msaada wa kisiasa na vyombo vya habari kwa makundi ya kigaidi, akisisitiza umuhimu wa kuzidisha juhudi za Jumuiya ya kimataifa ili kuzuia unyonyaji wa ugaidi maendeleo ya habari na ya kiteknolojia.

mkutano wa kilele wa Troika na "Kamati ya Libya" Aprili 23, 2019:

Mkutano huo ulijadili maendeleo ya hivi punde kwenye uwanja wa Libya na njia za kudhibiti mzozo na kufufua mchakato wa kisiasa nchini Libya na kutokomeza ugaidi, na kwa ushiriki wa Marais wa Rwanda na Afrika Kusini, wanachama wa Utawala wa Troika wa shirika, na Rais wa Kongo katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Kamati ya Libya katika shirika, Pamoja na ushiriki wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika.

Mkutano wa kilele wa mashauriano kwa Washirika wa Kikanda wa Sudan, Aprili 23:

Nchi zinazoshiriki tena uthibitisho wa kanuni na malengo ya Umoja wa Afrika katika kukuza amani, usalama na utulivu katika bara hilo, Pia wamesisitiza dhamira yao ya umoja, mamlaka, uadilifu na mshikamano wa Sudan na utimilifu wa eneo lake, na kuelezea kuunga mkono kikamilifu jukumu la Umoja wa Afrika, IGAD na nchi jirani katika kuunga mkono juhudi za Sudan kushinda kisiasa, usalama na kiuchumi. changamoto zinazoikabili, Pia ilihimiza nchi zinazoshiriki Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa kuendeleza mazungumzo na mamlaka ya Sudan na vyama vya Sudan, na kuitaka serikali ya Sudan iende sambamba na ushirikiano wake wenye kujenga na Umoja wa Afrika na tume yake, Kama ilihimiza nchi zilizoshiriki katika mkutano huo zimeitaka jumuiya ya kimataifa kuendeleza uungaji mkono wake na kutoa msaada wa haraka wa kiuchumi kwa Sudan kutokana na kuzorota kwa hali ya uchumi, na kusisitiza umuhimu wa msamaha wa haraka wa madeni ya Sudan.

Mkutano wa Ukanda na Barabara Beijing mnamo Aprili 24, 2019 nchini Uchina:

Akizungumza kwa niaba ya Afrika, rais ametoa wito wa kuwepo ushirikiano zaidi katika masuala ya miundombinu na maendeleo ya kiuchumi.

Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo wa Maendeleo ya Afrika (TICAD):

Japan iliandaa mkutano wa ngazi ya juu ili kuunga mkono Afrika na matarajio yake ya maendeleo.Mkutano wa saba wa Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD) ulifanyika Yokohama, Japan, kuanzia tarehe 28-30 Agosti 2019, pamoja na urais wa  Japan na Misri, mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, na kwa ushiriki wa Wakuu wa Nchi za Afrika, na idadi ya mashirika na taasisi za kimataifa, zikiongozwa na Umoja wa Mataifa na Benki ya Dunia.

Katika muktadha huu, lengo linalotarajiwa la kufanya mkutano huu ni kukuza mazungumzo ya kisiasa kati ya Afrika na washirika wake wa maendeleo.

Mkutano wa kumi na nne wa Kundi la Ishirini:

Rais El Sisi alishiriki katika shughuli za mkutano wa 14 wa G-20 huko Osaka, Japan, ambao ulifanyika Juni 28-29, Baada ya mwaliko wa kwenda Misri na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe kushiriki katika mkutano huo wa kilele, Kwa kuzingatia nafasi ya Misri barani Afrika,na  urais wake wa Umoja wa Afrika, Rais Sisi pia alishiriki katika mkutano mdogo wa uratibu wa Afrika, Kando ya mkutano wa kilele wa G20, uliojumuisha Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Rais wa Senegal Macky Sall, Ilikubaliwa wakati wa mkutano mdogo wa kilele kufanya kazi ya kuangazia vipaumbele vya maendeleo vya nchi za Afrika mbele ya washirika wakati wa mikutano ya G-20, ikilenga katika muktadha huu malengo yaliyojumuishwa katika Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063.

Upande wa pili: Katika ngazi ya Kiafrika:

Uzinduzi wa Eneo Kubwa la Makubaliano ya Biashara Huria ya Afrika ni msukumo mkubwa zaidi wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi za bara hilo, Mkutano wa 12 wa Pekee wa Afrika ulifanyika ikiongozwa na Rais Abdel Fattah El-Sisi, katika mji mkuu wa Niger, Niamey, Julai 7 na 8, 2019, na Mkutano huo ulishuhudia uzinduzi wa eneo la Makubaliano ya Biashara Huria ya Bara la Afrika, Baada ya kukamilisha akidi ya uidhinishaji wa nchi za Afrika, na kuanza kutumika kwa makubaliano.

Kongamano la Kwanza la Afrika ili kupambana na rushwa:

Mnamo Juni 12, 2019, Misri iliandaa Kongamano la kwanza la Kupambana na Rushwa Barani Afrika chini ya urais wake wa Umoja wa Afrika,na hii inatokana na mpango uliozinduliwa na Rais El Sisi Januari 2018, wakati wa ushiriki wake katika Mkutano wa kila mwaka wa Viongozi wa Afrika wa Viongozi wa Afrika.

katika Kongamano hilo  nchi 55 za Afrika na maafisa 200 wa ngazi za juu wa Afrika walishiriki, Kongamano hilo lilijadili mafaili muhimu, haswa mapitio ya juhudi za kitaifa za kupambana na rushwa kwa baadhi ya nchi za Afrika katika utekelezaji wa ahadi za bara na kimataifa, Kongamano la kupambana na rushwa katika maendeleo ya bara la Afrika, na mbinu za kupambana na rushwa katika ngazi ya bara na kukuza uwezo wa rasilimali watu katika nyanja mbalimbali za kupambana na rushwa katika bara la Afrika, na kusaidia uratibu baina ya serikali za Afrika katika kupambana na rushwa, na nafasi ya utashi wa kisiasa katika kufanikisha juhudi za kupambana na ufisadi katika bara la Afrika.

Kusherehesha kwa Siku ya Afrika:

Rais El-Sisi alitoa hotuba Mei 25 kusherehesha kwa Siku ya Afrika katika nafasi yake ya Rais wa Umoja wa Afrika, Wakati huo alisisitiza umuhimu wa kuwawezesha vijana wa bara hili kwenda sambamba na maendeleo ya nyakati na kutekeleza wajibu wao katika kuongoza mustakabali wa Afrika, Pamoja na kuendelea kuimarisha nafasi ya wanawake wa Kiafrika kama moyo mkuu wa jamii zao na mwanga wa mabadiliko yao ya kiuchumi na utulivu, na mbali na kuimarisha uhusiano wa kitamaduni na ustaarabu kati ya watu wake, na kuunganisha utambulisho wa Mwafrika na kuzingatia kanuni za mshikamano wa Kiafrika,na katika hotuba yake, Rais alidokeza kwamba hakuna namna yoyote kwetu isipokuwa kufanya juhudi na kuzingatia umoja wetu ili kutimiza ndoto ya waasisi na matarajio makubwa ya watu wa Afrika ya kuunda bara lenye utulivu na ustawi kuhakikisha maisha bora kwa watoto wake wote, Inatangaza mwanga wa ustaarabu na utamaduni wa uvumilivu na upendo kwa ulimwengu wote.

Upande wa tatu: mahusiano kati ya Misri na watu wa Afrika:

Misri imefanya juhudi kubwa katika mwelekeo huu, Misri iliandaa Kongamano la Uwekezaji Barani Afrika, Jukwaa la Uchumi la Waarabu na Afrika, na Aswan ikawa mji mkuu wa vijana wa Kiafrika, na  utoaji wa maagizo kwa mashirika yote ya serikali ya Misri ili kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika katika nyanja zote, iliyotekeleza mipango mingi ya ushirikiano katika nyanja zote za uchumi, biashara, kilimo, umwagiliaji, diplomasia, mazingira, vijana, michezo, viwanda, kada za ujenzi na binadamu. uwezo, miongoni mwa wengine.

Shirikisho la Misri la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mpira wa miguu:

Misri ilikuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, pamoja na  uongozi wake wa Umoja wa Afrika, iliyopangwa kuandaliwa na Cameroon katikati mwa bara hilo, Hata hivyo, maandalizi ya Cameroon kwa ajili ya tukio kubwa zaidi la michezo hayajakamilika katika Afrika, Shirikisho la Soka barani Afrika lilishinikiza CAF kuondoa shirika lake na kufidiwa kwa kuandaa toleo lijalo la 2021, Huko kanuni zilizopangwa hapo awali nchini Côte d'Ivoire na Guinea zikiendelea hadi 2023 na 2025.

Katika muktadha huu, Misri ilikuwa mwenyeji wa Michuano ya Mataifa ya Afrika mara nne zilizopita, kuanzia 1959, Kupitia matoleo ya 1974 na 1986, na kumalizia na ubingwa wa 2006, Shirika la Misri la michuano hiyo halijawahi kukutana na urais wa Umoja wa Afrika, lakini hii ni mara ya kwanza katika historia kwa Misri kuunganisha kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika na urais wa Umoja wa Afrika, Misri ichukue nafasi kubwa katika ngazi ya kisiasa na Pia hutiwa rangi na rangi ya michezo.

Kuandaa Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Vijana U-23, Misri ilikuwa juu ya jukumu hilo na kuangaza ulimwengu tena na mpangilio mzuri wa mashindano hayo, lililoweka taji la Mafarao na jina lake, Ambapo timu ya Olimpiki ya Misri ilipata mafanikio ya kihistoria mwaka 2019, baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika U-23 kwa mara ya kwanza katika historia yake,  Alifuzu kwa Michezo ya Olimpiki (Tokyo 2020) kwa mara ya 12 katika historia yake, na ya kwanza tangu toleo la 2012 huko London.

Kongamano la Aswan la Amani na Maendeleo Endelevu:

Rais Abdel Fattah El-Sisi alizindua katika Mkutano wa Sochi katika Shirikisho la Urusi kufanya toleo la kwanza la Jukwaa la Amani na Maendeleo Endelevu la Aswan, Hii ni ndani ya mfumo wa urais wa Misri wa Umoja wa Afrika 2019 na kufungua upeo mpya wa kufikia amani na maendeleo endelevu katika bara la Afrika.

Kongamano hilo lilifanyika Desemba 11, likiwa na lengo la kutaka uwekezaji wa rasilimali mbalimbali za Bara la Afrika na kuzigeuza kuwa thamani ya ziada sambamba na uendelezaji wa miundombinu yake, na ambayo ina maana utangulizi wa kufikia maendeleo endelevu, Pia, lengo la kuunganisha amani na kufikia maendeleo endelevu ni kuhimiza na kuhamasisha taasisi za fedha za kimataifa kusaidia na kufadhili miradi ya maendeleo barani Afrika na kuvutia uwekezaji kwake, hii ni kwa manufaa ya jumla ya bara kupitia upatikanaji wa bidhaa zake kwa Ulaya na kinyume chake kupitia lango la Misri.

Kongamano la Vijana wa Kiarabu na Kiafrika:

Kongamano la Vijana wa Kiarabu na Kiafrika, lililoandaliwa na Aswan kuanzia tarehe 16 hadi 18 Machi 2019, lilizinduliwa chini ya usimamizi wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, kwa ushiriki wa zaidi ya vijana 1,500 wa Kiafrika na Kiarabu kujadili masuala na changamoto za bara la kahawia na eneo la Kiarabu, Wakati wa kongamano hilo, Rais alisisitiza kwamba wazo la Jukwaa la Vijana Ulimwenguni lilikuja kuwasiliana na vikundi vyote vya vijana ili tuweze kusikia na kuzungumza kila mmoja, na akisisitiza umuhimu wa kuendelea kwa makongamano hayo na kwamba yanafanyika mara kwa mara ili lengo tarajiwa liweze kujulikana.

Kongamano hilo lilijumuisha shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kikao cha majadiliano "Mustakabali wa Utafiti wa Kisayansi na Huduma za Afya", na kikao cha meza ya pande zote kiitwacho "Bonde la Mto Nile ni ukanda wa ushirikiano wa Waafrika na Waarabu",na mkutano huo pia ulijumuisha warsha kuhusu "Maendeleo ya eneo la Sahel ya Afrika", Pamoja na kufanya warsha mbili za ujasiriamali, mojawapo ikiwa na mada “Jinsi ya kuwa Mjasiriamali mwenye Mafanikio”, na nyingine inaitwa "ujasiriamali wa kijamii kwa mtazamo wa Kiafrika".

Katika uwanja wa miundombinu, usafirishaji na mawasiliano:

Miradi ya kuunganisha Misri na nchi za bara la Afrika ilikuja juu ya miradi ya miundombinu (mradi wa Cairo-Cape Town), Mbali na hayo, mradi wa kuunganisha umeme kati ya Misri na nchi za mabara ya Afrika na Ulaya,Kwa kuzipatia nchi za mabara haya mawili umeme kupitia minara ya chuma inayovuka mpaka, na mradi wa kuunganisha maji (Alexandria - Victoria) ni mradi wa kuunganisha maji kati ya Ziwa Victoria lililoko Afrika na maji ya Mediterania nchini Misri, na mradi huu unachangia katika ufufuo wa kikanda kwa nchi zote za Bonde la Mto Nile.

Katika muktadha huu, Misri ilichangia kuanzishwa kwa hazina ya kuwekeza katika miundomsingi ya habari kwa lengo la kusaidia maendeleo ya teknolojia na mabadiliko ya kidijitali katika bara hilo,Ili kujenga uchumi wa kisasa kulingana na mifumo ya kisasa ya kiteknolojia, na Mamlaka Kuu ya Uwekezaji na Maeneo Huru pia ilitia saini, na Tume ya Uwekezaji ya Ethiopia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia mkataba wa maelewano katika uwanja wa kuimarisha uhusiano wa uwekezaji wa nchi mbili.

Katika ngazi ya afya

Misri ilitwaa urais wa Kamati Maalumu ya Kiufundi ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya ya Umoja wa Afrika, Sambamba na mipango iliyozinduliwa na Rais Abdel Fattah El-Sisi katika uwanja y

wa afya, inayolenga kupambana na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza, na hasa mpango wa "Seha Milioni 100", uliojumuisha kuwachunguza wakaazi wasio Wamisri, na Misri pia inakusudia kuanzisha kituo cha kikanda ili kusaidia mipango ya afya ya umma kuwa na makao yake huko Kairo ili kuamsha mipango ya afya ya umma katika nchi za Kiafrika ili kuondoa magonjwa na milipuko ambayo ni mzigo mkubwa kwa nchi za Kiafrika.

Mikutano na viongozi wa Afrika:

Rais El-Sisi alianza ziara yake katika nchi za Afrika mnamo mnamo  Februari 9, kwa ziara ya kihistoria katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, ambayo ilishuhudia akichukua nafasi ya urais wa Umoja wa Afrika, akiongoza kazi ya kikao cha kawaida cha thelathini na mbili wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika katika shirikisho, na katika muktadha huu, Rais El Sisi alianza tarehe saba mwezi wa Aprili ziara ya nje iliyojumuisha ziara za Guinea, Côte d'Ivoire na Senegal, Ndani ya muktadha wa nia ya Misri ya kuzidisha mawasiliano na uratibu na ndugu zake wa Afrika, ili kuendelea kuimarisha uhusiano wake na nchi za bara hilo katika nyanja mbalimbali.

na kando ya ushiriki wake katika shughuli za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika mwezi wa Septemba, Rais Sisi alishiriki katika mkutano wa wakuu wa nchi tatu uliojumuisha Rais wa Jamhuri ya Somalia, Mohamed Abdullah Farmajo, na Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta, Ili kujadili baadhi ya masuala ya pande mbili za mzozo kati ya pande hizo mbili.

Mnamo tarehe tisa Juni, Rais El Sisi alimpokea Rais wa Nchi ya Eritrea,Rais Isaias Afwerki, Ili kuunganisha ushirikiano wa kimkakati na Eritrea, na Rais alisisitiza umuhimu wa kusonga mbele katika kuandaa mipango mahususi ya kuendeleza miradi ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili katika sekta mbalimbali na kuondokana na vikwazo vyote, na hasa katika sekta za miundombinu, umeme, afya, biashara na uwekezaji, kilimo, mifugo na uvuvi, Mbali na kuimarisha programu za msaada wa kiufundi zinazotolewa kwa upande wa Eritrea kupitia Wakala wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Misri.

Mbali na kukutana na marais na viongozi kadhaa wa bara la Afrika, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Felipe Jacinto Nyusi,na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abi Ahmed, na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, na  Rais wa Chad,na Rais wa Jamhuri ya Comoro, kwa ajili ya kujadili njia za kuimarisha ushirikiano, mashauriano na uratibu kuelekea masuala ya Afrika yenye wasiwasi na juhudi za kupambana na ugaidi, na njia za kuimarisha mahusiano baina ya nchi katika ngazi mbalimbali.

Kutokana na Urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika, viongozi na wakuu wengi wa nchi za Afrika walitembelea Kairo, akiwemo Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika,Moussa Fakih, aliyekutana na Rais El Sisi kando ya Kongamano la Vijana wa Kiarabu na Kiafrika huko Aswan, Akisisitiza umuhimu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika (NEPAD), Kwa kuzingatia ukweli kwamba Misri ni moja ya nchi waanzilishi wa mpango huo, Tarehe 8 Mei, Rais Sisi alipokea Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, na mkutano ulishuhudia maafikiano juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili ili kuunga mkono mipango ya NEPAD inayolenga kuendeleza na kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kikanda barani Afrika.

Hitimisho:

Misri imetimiza kile ambacho Rais Abdel Fattah el-Sisi aliahidi katika hotuba yake katika mkutano wa kilele wa Afrika, uliofanyika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, na Misri ilichukua nafasi ya urais wa Shirikisho, Itafanya kazi kwa bidii ili kuendeleza njia ya mageuzi ya kimuundo na kifedha ya shirikisho na kukamilisha mafanikio yameyopatikana ili kuunganisha umiliki wa nchi wanachama wa Jumuiya yao ya Bara na kutafuta kukuza zana na uwezo wa Muungano na tume zake ili kukidhi matarajio ya watu wa Kiafrika, na kuimarisha mifumo ya maendeleo endelevu ili kutoa nafasi zaidi za kazi kwa vijana wa Kiafrika.

Misri imepata matokeo mengi ya kuvutia katika ngazi ya kikanda na kimataifa, yaliyosifiwa na nchi wanachama wa Umoja huo na maafisa wakuu wa muundo wake wa kiutawala,Kwa kuwa, Misri ilithibitisha tena kanuni na malengo ya Umoja wa Afrika katika kukuza amani, usalama na utulivu katika bara hilo, na Rais Sisi hakuondoka kwenye kongamano la kimataifa bila kushiriki, akiwa amebeba wasiwasi na matumaini ya watu wa bara hilo kwa maisha ya staha na kupata haki yao ya maendeleo endelevu na fursa za ajira, Mbali na mwaliko wake kwa wafanyabiashara na makampuni makubwa ya kimataifa kuwekeza barani Afrika, Kwa sababu ya fursa na faida zake zisizo na mwisho, pamoja na maliasili na wafanyikazi.

Pamoja na kuendelea kuimarisha nafasi ya wanawake wa Kiafrika kama moyo mkuu wa jamii zao na mwanga wa mabadiliko yao ya kiuchumi na utulivu wake, Mbali na kuimarisha uhusiano wa kitamaduni na ustaarabu kati ya watu wake, na kuunganisha utambulisho wa Mwafrika na kudumisha kanuni za mshikamano wa Kiafrika.

Orodha ya Marejeleo:

Kwanza: Marejeleo kwa Kiarabu:

Fatima Hassan, "Mavuno ya 2019..Urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika", Mamlaka ya Kitaifa ya Vyombo vya Habari, inapatikana kwenye kiungo kifuatacho www.maspero.eg

Urais wa Umoja wa Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, inapatikana kwenye kiungo kifuatacho www.mfa.gov.eg

"Urais wa Umoja wa Afrika unaelekezwa Misri kwa mara ya kwanza katika historia ya Shirika hilo", inayopatikana kwa kiungo kifuatacho: www.france24.com

Urais wa Misri wa Umoja wa Afrika 2019, Taasisi kuu ya Taarifa, inapatikana kwa kiungo kifuatacho: www.sis.gov.eg

Pili: Marejeleo kwa Kiingereza:

Diaa Rashwan,” Egypt president of the African Union .. the possible and hoped” (Issue47,2018), Available at: www.africa.sis.gov.eg

“Egypt to Hand African Union Presidency to South Africa in February”, Asharq Al-Awsat, Available at: https://aawsat.com

Christin Roby, “What will Egypt focus on as African Union chair?”, Available at: www.devex.com/new

Amr Mohamed Kandil, “Sisi hands over African Union presidency to South Africa”, Available at: www.egypttoday.com