Dkt. Sufi Abu Taleb

Dkt. Sufi Abu Taleb

Imefasiriwa na / Abdullah Nasser Farahat

Alizaliwa mnamo Januari 27, 1925, katika Kituo cha Tamiya cha mkoa wa Fayoum, alihitimu kutoka Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Kairo mnamo 1946 , kisha diploma ya sheria kuu mnamo 1947, na alipelekwa huko Ufaransa mnamo 1948.

Abu Taleb alipata shahada ya Uzamivu wa sheria kutoka Paris mwaka 1950, na akapandishwa katika nyadhifa za chuo kikuu hadi akashika nafasi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kairo, na akashinda tuzo ya tasnifu bora ya Uzamivu kutoka chuo hicho hicho, na akateuliwa kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kairo. Mshauri wa Chuo Kikuu cha Assiut.  Dkt.Sufi alipata “Diploma in Mediterranean Laws” kutoka Chuo Kikuu cha Rome mwaka wa 1959.

Baada ya kurudi Kairo, aliteuliwa kuwa mshauri wa Chuo Kikuu cha Kairo mnamo kipindi cha 1967  hadi 1973, kisha kama Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kairo kutoka 1973 hadi 1975, kisha akashika nafasi ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kairo kutoka 1975 hadi 1978  na mnamo kipindi hiki Dkt. Abu Taleb alikuwa mjumbe aliyechaguliwa Katika Kamati Kuu ya Umoja wa Kisoshalisti mwaka 1975, Abu Taliyb pia alishinda uanachama wa Bunge la Wananchi kwa wilaya ya Tamiya-Fayoum mwaka 1976. Na alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu ya Baraza.

Dkt. Sufi alichukua urais wa Bunge la Wananchi mwaka 1978, na aliweza kutoa uamuzi wa Jamhuri wa kuanzisha tawi la Chuo Kikuu cha Kairo, tawi la Fayoum. Chuo cha Elimu kilikuwa chuo cha kwanza kuanzishwa Fayoum, naye alitunukiwa kwa nafasi yake kubwa katika chuo kikuu. Ukumbi mkubwa zaidi katika Chuo cha Elimu ulipewa jina lake, kisha vyuo vilipanuka, hadi kikawa Chuo Kikuu cha Fayoum kinajitegemea. 
Alijulikana kama injini ya mradi wa kuweka kanuni za Sharia, ambapo kamati za Bunge la Wananchi zilifanya kazi mwishoni mwa miaka ya 1970, na alimaliza kabisa mwanzoni mwa miaka ya 1980. Alipigana vita ili kuhakikisha kuendelea kwa “Sharia ya Kiislamu” kama chanzo cha sheria. Katika Kifungu cha 2 cha Katiba, kwa kusukumwa na somo la Sharia alilokuwa akisoma chuo kikuu.

Wakati wa kuuawa kwa Rais Sadat Oktoba 6, 1981, Abu Taleb alikuwa na nafasi ya Spika wa Bunge la Wananchi, na kwa mujibu wa Katiba ya 1971, uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ulifanywa kwa kuchagua Bunge la Wananchi. Jina au mgombea wa kiti cha urais, na kuiwasilisha kwa wananchi kwa ajili ya kura ya maoni juu yake.Bunge la Wananchi, nafasi ya urais wa Jamhuri, endapo nafasi ya Rais wa Jamhuri itakuwa wazi kwa kifo, na. Ikiwa Bunge litavunjwa, Rais wa Mahakama ya Juu ya Kikatiba atalibadilisha, kwa masharti kwamba hakuna yeyote kati yao anayeweza kuteua urais.

Katika kauli yake ya kwanza baada ya kushika kiti cha urais kwa muda, Abu Taleb alitoa wito kwa wananchi kufanya kura hiyo ya maoni akisema, “Kura ya maoni ya leo sio tu kura ya maoni ya kuchagua rais tu, bali ni kura ya maoni juu ya sera ya Misri yote ambayo iliweka misingi ya marehemu Rais Anwar Sadat.

Dkt. Abu Taleb aliondoka kwenye Baraza la Wawakilishi mnamo Februari 1983 baada ya kumalizika kwa muhula wake, baada ya hapo aliendelea na kazi yake ya kitaaluma kama Profesa wa Sharia katika Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Kairo, na kisha kama mjumbe wa Chuo cha Utafiti cha Kiislamu.

Pia alishika nyadhifa nyingine, kama mjumbe wa Baraza la Taifa la Elimu, mjumbe wa Baraza Kuu la Sanaa na Barua, mwandishi wa Kamati ya Historia ya Sheria ya Baraza Kuu la Sanaa na Barua, mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha Uchumi na Sheria, na katibu wa Chama cha Ustawi wa Wanafunzi.

Dkt. Abu Taleb ni mwandishi wa idadi ya vitabu, maarufu zaidi kati yao ni kitabu chake kiitwacho “Misingi ya Fiqh”. 
Alikuwa mwanaharakati na mwenye njia nyepesi ya kujieleza, na aliendelea kukanusha hoja za wale waliopinga kutumika kwa sheria ya Kiislamu, hadi mwisho wa maisha yake.

Alipata tuzo na heshima nyingi wakati wa uhai wake, zikiwemo:

 Mkufu wa Nile kutoka Misri.

Mkufu wa Jamhuri kutoka Sudan.

Nishani ya Heshima kutoka kwa serikali ya Ufaransa mnamo 1977.

Tuzo ya Kuthamini ya Nchi mnamo 1990.


Dkt. Sufi Abu Taleb aliaga Dunia alfajiri  Februari 21, 2008, alipokuwa akishiriki katika mkutano wa tatu wa kimataifa wa Jumuiya ya Wahitimu wa Al-Azhar Duniani kote katika mji wa Kuala Lumpur nchini Malaysia.