Siku ya Kimataifa ya Kuzuia Matumizi ya Mazingira Katika Vita na Migogoro yenye Silaha

Siku ya Kimataifa ya Kuzuia Matumizi ya Mazingira Katika Vita na Migogoro yenye Silaha

Imetafsiriwa na/ Enas AbdelBassit
Imehaririwa na/ Nourhan Khaled 

Dhabihu za kimya zililipwa kila mwaka,  ambayo kila mwaka wanalipa gharama kubwa ya vita kwenye nchi, si wanadamu tu  waathirika kwenye vita,  bali karibu asilimia 40 ya migogoro ya silaha inayoendelea sasa ulimwenguni inahusiana na rasilimali za asili, iwe ni rasilimali zenye thamani kubwa, kama vile mbao, almasi, dhahabu na mafuta, au vitu vya nadra kama maji safi na udongo wenye rutuba. Migogoro imechoma mazao, imechafua visima vya maji, imechafua udongo, imeua wanyama, na kukata misitu, katika nchi nyingi kwa faida ya kijeshi.


 Vita vyote hususan vita vya Kwanza na vya Pili vya Ulimwengu,  ghafla vilibadilisha hali duniani,  Kulingana na utafiti uliochapishwa katika jarida la Nature, kuwa asilimia 70 ya hifadhi za asili barani Afrika ziliharibiwa na vita vilivyotokea kwenye bara hilo (1946-2010), na kusababisha kutoweka idadi ya mamalia na ndege wa porini, na makundi mingine hufikia hali ya hatari ya kutoweka. 


Mnamo mwaka 2016, idadi ya migogoro na mizozo yenye silaha ulimwenguni ilifikia kiwango cha juu zaidi, na inakadiriwa kuwa na migogoro 53 inayoendelea katika nchi 37, na asilimia 12 ya idadi ya watu ulimwenguni wanaishi katika maeneo ya migogoro ya kudumu hiyo kusababisha watu milioni 69 kuhamishwa kwa nguvu kutoka nyumba zao kwa athari ya vurugu tangu Vita vya Kidunia vya pili. 


Tukio hilo linachukuliwa kama Wito wa Amani kwa mazingira, jambo ambalo linahusiana sana na afya ya kibinadamu na njia za maisha, linalochangia nchi zilizoathiriwa na migogoro kuchukua hatua nyingine karibu na kufikia malengo ya maendeleo endelevu, ambapo Kuzungumzia uchafuzi unaosababishwa  na vita, migogoro na mizozo mahali pengine ni suala la Usalama wa Kibinadamu wa kiwango cha kwanza, ambao athari zake zinaeneza vizazi vingi vijavyo, hususan ikiwa silaha za nyuklia zinatumiwa wakati wa migogoro, basi ni suala muhimu kwa wanadamu wote.


Kulingana na takwimu za Shirika la Msalaba Mwekundu, leo kuna mabomu ya nyuklia zaidi ya 14,000 ulimwenguni, makumi au hata maelfu ya mabomu hayo yakiwa tayari kurushwa kushtuka, na mengi ya mabomu hayo yana nguvu nyingi kuliko mabomu mawili ya nyuklia yaliyopigwa  katika majiji ya Hiroshima na Nagasaki, yaliyoua karibu watu 109,000 huko nchini Japani.


Mratibu wa lugha ya kiswahili/ Tasneem Hamdy