Misri na Pakistani

Misri na Pakistani

Imefasiriwa na / Abdullah Nasser Farahat

Misri ni nchi ya kwanza katika Mashariki ya Kati ambapo Pakistani imefungua ubalozi mara tu baada ya kupata uhuru.Balozi wa kwanza wa Pakistani nchini Misri aliteuliwa Juni 30, 1948.

Pakistani ilimuunga mkono Abdel Nasser katika mapinduzi ya Julai 1952 na kukuza harakati zake za kufikia uhuru.

Misri ilikuwa na jukumu kubwa katika kusimamisha vita vya India na Pakistani mwaka 1965, ambapo Abdel Nasser mnamo Septemba 8 mwaka huo huo amepeleka ombi kwa serikali za nchi hizo mbili za kusitisha mapigano mara moja, na akaeleza nia yake ya kusaidia na kutoa juhudi zote kwa nchi hizo mbili.

Wakati wa ziara yake nchini Pakistani mnamo Aprili 1960, Abdel Nasser alimkabidhi Rais wa Pakistani Ayub Khan Mkufu wa Nile, na Chuo Kikuu cha Pakistani cha Bakkah kilimtunuku Rais Gamal Abdel Nasser shahada ya heshima ya Uzamivu katika Sheria.