Jenerali Mkuu Osama Rabie… Kutoka Kina cha Bahari hadi Kilele cha Mfereji wa Suez

Jenerali Mkuu Osama Rabie… Kutoka Kina cha Bahari hadi Kilele cha Mfereji wa Suez

Imetafsiriwa na: Omnia Ali Mohamed
Imehaririwa na: Mervat Sakr
Mratibu wa Lugha ya Kiswahili: Mervat Sakr

Katika rekodi yenye mafanikio makubwa ya kujitolea na nidhamu, jina la Luteni Jenerali Usama Rabie linang’aa kama mmoja wa viongozi mashuhuri wa kijeshi nchini Misri, ambapo alitengeneza njia yake kwa uthabiti na ufanisi hadi akafikia kilele cha uongozi katika moja ya taasisi muhimu zaidi za kimkakati za taifa, yaani Mamlaka ya Mfereji wa Suez.

Luteni Jenerali Usama Rabie amezaliwa mwaka 1955, na alianza safari yake ya kitaifa baada ya kuhitimu kutoka Chuo cha Majini mnamo mwaka 1977, kisha akaungana na vikosi vya majini ambapo alipitia nafasi mbalimbali za uongozi, akipata uzoefu wa kivitendo na kielimu uliomwezesha kuongoza vikosi muhimu zaidi vya majini nchini.

Rabie alishikilia nyadhifa nyingi muhimu ndani ya Jeshi la Majini, zikiwemo:
• Kamanda wa Kivukio cha kuondoa mabomu ya majini
• Mkuu wa Shtabu wa Kikosi cha kupambana na mabomu ya majini
• Kamanda wa Kitengo cha Sanaa za Kijeshi katika Chuo cha Majini
• Kamanda wa Kikosi cha kupambana na mabomu ya majini

Pia aliongoza vituo vya majini, kama vile:
• Kamanda wa Kituo cha Majini cha Suez
• Kamanda wa Kituo cha Majini cha Alexandria

Hakukosa pia upande wa kielimu, ambapo aliteuliwa kuwa:
• Mkurugenzi wa Chuo cha Majini
• Naibu Mkurugenzi wa Chuo cha Majini

Aidha, alibeba majukumu ya kimkakati yenye umuhimu mkubwa, kama vile:
• Mkuu wa Kitengo cha Uratibu na Utawala wa Majini
• Mkuu wa Kitengo cha Operesheni za Majini
• Msaidizi wa Kamanda wa Jeshi la Majini
• Mkuu wa Shtabu wa Jeshi la Majini

Mnamo tarehe Aprili 11, 2015, aliteuliwa kuwa Kamanda wa Jeshi la Majini la Misri, mojawapo ya matawi makuu ya Vikosi vya Silaha, na akapandishwa cheo kuwa Luteni Jenerali mnamo tarehe Machi 17, 2016.

Katika hatua muhimu ya maisha yake, Luteni Jenerali Usama Rabie aliteuliwa tarehe Desemba 17, 2016 kuwa Naibu Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mfereji wa Suez, taasisi inayosimamia njia muhimu zaidi ya biashara ya kimataifa. Baadaye akawa Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo, akiongoza juhudi za upanuzi na maendeleo, na akaendelea kutoa mchango wake katika nafasi ya kiraia, isiyo na umuhimu mdogo kuliko kazi ya kijeshi, kwani inahitaji usimamizi wa kiwango cha juu na mtazamo wa mbali wa kimaendeleo.

Rabie alipokea tuzo na medali kadhaa kama heshima kwa huduma yake iliyotukuka, zikiwemo:
• Medali ya Huduma Ndefu na Mfano Mzuri
• Nishani ya Wajibu wa Kijeshi (daraja la pili na la kwanza)
• Medali ya Huduma Bora
• Medali ya Januari 25, 2011
• Medali ya Juni 30, 2013

Luteni Jenerali Osama Rabie anachanganya ukali wa kijeshi na maono ya kiutawala, akiwakilisha mfano wa kiongozi kamili ambaye hakujua njia nyingine isipokuwa nidhamu, akihudumia taifa baharini na bandari, kambini na vitani, hata kwenye kingo za Mfereji wa Suez.

Wakati Luteni Jenerali Rabie akiendelea kuongoza mojawapo ya taasisi kuu za kitaifa nchini Misri, safari yake inabaki kuwa msukumo kwa vizazi vya vijana wanaotamani kulihudumia taifa lao kwa roho ya uzalendo na ufanisi wa hali ya juu.