Mshikamano wa Kimataifa wajadili Athari za Lugha ya Kiswahili kwa Tamaduni na Utambulisho wa Kitaifa kwenye Afrika Mashariki
Imetafsiriwa na/ Mratibu wa Lugha ya Kiswahili "Mervat Sakr"
Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa (Harakati ya Nasser kwa Vijana- Idara ya Lugha ya Kiswahili) uliandaa Kikao cha Pili cha "Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa kilichoitwa "Athari za Lugha ya Kiswahili kwa Tamaduni na Utambulisho wa Kitaifa (mfano ni kwenye Tanzania na Kenya) ". Kikao hicho kilishuhudia ushiriki wa Prof. Dkt. Kinenee Wamutiso, Profesa wa Ushairi wa Kiswahili kwenye Chuo Kikuu cha Nairobi-Kenya, na Prof. Dkt. Ayman Al-Aasar, Profesa wa Fasihi ya Kiswahili katika Kitivo cha Lugha na Ufasiri kwenye Chuo Kikuu cha Al-Azhar.
Kwa upande wake, Prof. Dkt. Kinenee Wamutiso alizungumzia jukumu la lugha ya Kiswahili na uhusiano wake na Kiarabu, akieleza kuwa ushairi wa Kiswahili ulianzia katika herufi za Kiarabu. Alifafanua kuwa Kiswahili kinachozungumzwa na makabila mengi, kiliibuka kutokana na mwingiliano wa kibiashara na kiutamaduni kati ya Waarabu na Waswahili, na kina maneno mengi yanayofanana na Kiarabu, hali inayoakisi mahusiano imara yaliyopo baina ya pande hizo mbili, pia alisisitiza umuhimu wa kuhifadhi Kiswahili kama lugha ya mawasiliano kati ya makabila zaidi ya ishirini Kusini na Mashariki mwa Afrika.
Wamutiso alibainisha jukumu la UNESCO kwenye kukuza Kiswahili kama lugha rasmi ya kimataifa, na akatoa wito wa matumizi yake kama lugha ya mawasiliano kati ya Kiswahili ili kuhifadhi urithi wao wa kitamaduni na lugha. Aidha, amewashukuru Harakati ya Nasser kwa Vijana na taifa la Misri kwa kuvutiwa na lugha ya Kiswahili, akipongeza mchango wa Misri katika kusaidia wanafunzi wa lugha ya Kiswahili kupitia vyuo vikuu vinne vya Misri, vinavyoonesha dhamira ya Misri kwa kukuza lugha za Kiafrika na kuimarisha mahusiano ya kitamaduni na kielimu na bara la Afrika.
Katika kikao hicho, Prof. Ayman Al-Aasar aligusia mada kadhaa, ambapo alisisitiza utambulisho wa pamoja kati ya Tanzania na Kenya kutokana na Kiswahili kuwa lugha ya mawasiliano. Al-Aasar alieleza kuwa lugha ya Kiswahili iliathiriwa na lugha ya Kiarabu kwa asilimia 30 kutokana na kubadilishana kiutamaduni na kibiashara, akibainisha kuwa utamaduni una mila na desturi na kwamba utambulisho ni sehemu muhimu ya lugha hiyo. Akaongeza kwamba asili ya utamaduni katika eneo hili inatokana na Bantu na Uislamu, akibainisha athari ya sasa ya lugha ya Kiingereza kwenye Kiswahili. Pia alieleza kwamba kuna tofauti za lahaja kati ya Tanzania na Kenya, lakini tofauti hizi hazizuii maelewano kati ya watu wa nchi hizi mbili, hivyo kuimarisha umoja wa kitamaduni na lugha.
Al-Aasar pia alishukuru Harakati ya Nasser kwa Vijana na Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa kwa maslahi yake kwenye lugha ya Kiswahili na jukumu la mtafiti Hassan Ghazaly, mwanzilishi wa mipango yote hii, inayofanya kazi ya kukuza na kuhamasisha wanafunzi wa lugha ya Kiswahili na wasemaji, akisifu jukumu la harakati katika kutoa fursa za mafunzo, kujenga uwezo na msaada kwa wanafunzi wa lugha ya Kiswahili, inayochangia kuimarisha taswira ya Misri nje na kuonesha nia yake kwenye duara la Afrika.
Kikao hicho kilisimamiwa na Mfasiri Yasmine Mahmoud Kamal, Mtafiti wa lugha za Kiafrika, Idara ya Lugha ya Kiswahili, na Mratibu wa Kanda ya Afrika Mashariki kwa Harakati za Nasser kwa Vijana.
Katika muktadha unaohusiana, Hassan Ghazaly, mwanzilishi na mkuu wa Mtandao wa Mshikamano wa Kimataifa, alisisitiza nia ya mtandao wa kuwezesha na kujenga uwezo wa makada vijana wa wanafunzi wa lugha tofauti, kusaidia uelewa wao wa masuala ya Ulimwenguni Kusini, na kuunda jukwaa la bure la kuelezea maoni, matarajio, na kubadilishana uzoefu kati ya vizazi tofauti, akibainisha kuwa Mpango wa Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa ni upanuzi wa Mpango wa Mazungumzo ya Raia wa Ulimwengu mzima, uliozinduliwa na mtandao katika 2020, ndani ya miradi ya mtandao, ambayo ina idadi ya miradi 15 kwenye nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari, uongozi, vijana na utamaduni.