Mfereji Mpya wa Suez

Imefasiriwa na / Nada Abbas
Mfereji Mpya wa Suez umeanzishwa kutoka Km 60 hadi Km 95 (namba za mfereji), pamoja na kupanua na kuongeza matawi ya Maziwa Makuu na Al-Balah, yenye urefu wa kilomita 37 (jumla ya urefu wa mradi ni Km 72 )
Wazo la kuanzisha Mfereji mpya sambamba na kuongeza Faida kutoka kwa mfereji huo na matawi yake ya kisasa ili kufikia asilimia kubwa ya urudufishaji ili kuendesha meli pande zote mbili bila kusimama katika maeneo ya kusubiri ndani ya mfereji huo na kupunguza muda wa usafiri wa meli zinazopita, na kuongeza uwezo wao wa kupitisha meli kwa kuzingatia ukuaji unaotarajiwa wa kiasi cha biashara ya dunia katika siku zijazo. Na kuhusiana na mradi wa maendeleo katika eneo la Mfereji wa Suez, na kuinua kiwango cha imani katika mfereji kama njia bora ya kimataifa ya usafirishaji, na kupunguza thamani ya mawazo katika mifereji mbadala za ushindani Duniani na kikanda pia kuongeza kiwango cha imani katika utayari wa Misri kwa ajili ya mafanikio ya mradi wa maendeleo katika eneo la Mfereji wa Suez, na yote yaliyo hapo juu yanaonekana katika ongezeko la pato la taifa la Misri kutokana na sarafu ngumu, na inakwenda moja kwa moja kwenye hazina ya serikali pamoja na kutoa idadi kubwa zaidi ya nafasi za kazi kwa vijana wa Misri na kuunda jumuiya mpya za mijini.
Mradi huo unalenga kuongeza pato la taifa la Misri kutokana na sarafu ngumu. Kufikia asilimia kubwa zaidi ya marudio katika mfereji wa Suez na kuongeza hadi asilimia 50 ya urefu wa kozi ya urambazaji. Mbali na kupunguza muda wa usafiri kuwa saa 11 badala ya Saa 18 kwa Msafara wa Kaskazini. Licha ya kupunguza muda wa kusubiri kwa meli kuwa saa 3 katika hali mbaya zaidi badala ya (saa 8 hadi 11), ambayo inaonekana katika kupunguza gharama ya usafiri kwa wamiliki wa meli na kuongeza kiwango cha kuthamini Mfereji wa Suez. kuchangia katika kuongeza mahitaji ya kutumia mfereji kama njia kuu ya kimataifa ya usafirishaji na kuongeza uainishaji wake.
Mradi pia unafanya kazi ya kuongeza uwezo wa kupitisha meli katika mfereji huo ili kukidhi ukuaji unaotarajiwa wa kiasi cha biashara ya dunia katika siku zijazo.
Hivyo ni hatua muhimu katika njia ya mafanikio ya mradi wa mhimili wa maendeleo katika eneo la Mfereji wa Suez na kusukuma mbele uchumi wa taifa la Misri ili kubadilisha Misri kuwa kituo cha biashara na vifaa vya kimataifa.
Marejesho na matokeo ya mradi yanawakilishwa katika kuongeza uwezo wa mfereji kuwa meli 97 za kawaida mwaka 2023 badala ya meli 49 mwaka 2014. Na kufikia usafiri wa moja kwa moja, bila ya kusimama kwa meli 45 katika pande zote mbili, na uwezekano wa kuruhusu meli kuvuka hadi rasimu ya futi 66 katika sehemu zote za mfereji. Mbali na ongezeko la mapato ya Mfereji wa Suez kwa 259% mwaka 2023 kuwa $13.226 bilioni ikilinganishwa na mapato ya kisasa ya $5.3 bilioni, inayoongoza kwa athari chanya ya moja kwa moja kwa pato la taifa la Misri kutokana na sarafu ngumu. Pia itafanya kazi ya kuongeza nafasi za kazi kwa watu wa miji ya Canal, Sinai na majimbo jirani, huku ikiunda jumuiya mpya za mijini.Kuongeza uwezo wa ushindani wa Mfereji na kuutofautisha na njia zinazofanana. Kuongeza uainishaji wa kimataifa wa njia ya meli kama matokeo ya kuongeza viwango vya usalama wa urambazaji wakati wa kupita kwa meli.
Mradi huo ulitekelezwa kwa muda wa miezi 12 (mwaka mmoja), na ulizinduliwa mnamo Agosti 2015.