Taasisi ya kiafrika ya Ustawi na kujenga uwezo

Taasisi ya kiafrika ya Ustawi na kujenga uwezo

Ni taasisi isiyo ya kiserikali na isiyo na faida, ikisajiliwa na Wizara ya Mshikamano wa jamii kwa Na. (11250) kwa mwaka wa 2021, na sehemu yake ya kijiografia ya kazi iko katika ngazi ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri. Mtazamo mkuu wa taasisi ni kuhakikisha ukaribu na kuimarisha viungo vya urafiki kati ya watu kwa njia  inayochangia kuhakikisha maendeleo na ujenzi wa mtu wa Afrika, hivyo ina ishara ya “Misri ni kijiji changu.. Afrika ni mji wangu wa nyumbani”.

Taasisi ya kiafrika inajitahidi kusaidia kutekeleza maoni ya serikali katika kuhakikisha ushirikiano wa Afrika kupitia Mtazamo wa Misri 2030 na Ajenda ya Afrika 2063, pia  kujenga sura halisi ya akili na ufahamu wa kweli kuhusu nchi za kiafrika, pamoja na kuhamasisha kazi ya Diplomasia ya vijana ya kujitolea kati ya vijana wa Afrika kupitia kuratibu kubadilishana kwa wajumbe na ziara kati ya nchi tofauti, mbali na hayo shughuli mbalimbali zinazotufikisha lengo hilo hilo. Taasisi pia ina jukumu la ufahamu kwa kuhamasisha linalojulikana kama Ushirikiano wa Kusini-Kusini kati ya mabara ya Afrika, Asia, na Amerika ya latini.